kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Chama kinachojibainisha kama kikuu cha upinzani kimekuwa kinalizungumzia suala la katiba kama vile bado halijashughulikiwa. CHADEMA wamekuwa wanataka wapate aina fulani ya Katiba ambayo itawanufaisha wao kisiasa na labda kimapato kwa viongozi wao wala siyo katiba itakayokubalika na wengi kama ilivyotokea kwenye Bunge la Katiba.
CHADEMA sio siri. Wanataka katiba itakayoweka serikali tatu kama ilivyokua inadaiwa na cuf ya maalim seif. Ukaribu na usiri kati ya maalim seif na mbowe kabla ya bunge la katiba inaonyesha njama ya mbowe kumpa maalim seif alichokua anakitaka kwa udi na uvumba.
Tunachojua sasa katiba pendekezwa iko mezani ila wanachotaka chadema ni kuanzwa upya zoezi hilo kwa matumaini ya kupata kile walichokikosa. Hawajali gharama na muda uliyotumika kupata katiba pendekezwa.
Kwa ufupi chadema ni wapinga maendeleo wakubwa 'reactionnaries' . Agenda zao ni za kupotezea muda nchi. Badala ya nchi kujishughulisha na agenda za maendeleo nchi ipoteze muda kwa porojo na kubishana huku mabeberu wakipata muda kuhujumu na kuteka uchumi wa nchi.