Upinzani watangaza mapambano 2008

Swali jingine ni kwamba...Atokee mtu kama Kingunge Ngombale Mwiru...Kama kawaida yake ampe Mungwana mawaidha mabovu!
Say for instance...amwambie kuwa kuitoa ripoti sasa hivi kutaiua CCM!
Atamsikiliza Kingunge ama atawasikiliza wapinzani?
 
Swali jingine ni kwamba...Atokee mtu kama Kingunge Ngombale Mwiru...Kama kawaida yake ampe Mungwana mawaidha mabovu!
Say for instance...amwambie kuwa kuitoa ripoti sasa hivi kutaiua CCM!
Atamsikiliza Kingunge ama atawasikiliza wapinzani?

Kamanda,
Unapoamua kumdharau Mhe. Kingunge ni sawa na Kuidharua CCM, mbaya zaidi ni kumdharau Mhe. JK
Kimsingi unasahau kuwa ni CCM ambao wapo madarakani, hivyo kitkachoamuliwa ni kwa manufaa ya Nchi na sio kwa manufaa ya vyama vya upinzani au matakwa yako binafsi. Serikali haipo madarakani kuwatumikia vyama vya upinzani, bali wananchi wake kwa ujumla. Usijisahau sana...
 
Unayaamini unayoandika au...........? ili mradi tu!
 

Mkuu,

Mimi siamini kama kila wanachoamua CCM ni kwa manufaa ya taifa, CCM wamefanya mengi ambayo sio kwa manufaa ya taifa bali kwa manufaa yao wachache tena na si manufaa ya wanaccm wote, wanatanguliza zaidi ibara ya 15:1 kabla ya masirahi ya taifa na ndo maana taifa linakwenda halijojo.

Wananchi wanapoata mateso ya kutosha na CCM wanatumia hayo mateso kama njia ya kupata kura mwaka 2010, kwa kuwadanganya wanchi kuwapatia maisha bora wakati sio kweli na hawawezi kuwapatia hayo maisha kama mwenendo ndo huu.
 
na dhani kweli wewe kweli kama si mtu wa miaka ya 47 huko basi hapa nafikiri hapakufa "SHY" mana utatolewa kweli niSHY na point zako, kama huoni kama kuna mabadiliko kakita siasa za bongo basi wewe sio mtu kamili.

u need more shule wake up ndugu
 

Naona umeshajibiwa maswali yako yote isipokuwa hili nami nimeona nikujibu ili kukuweka sawa. Kwanza, nami nikubaliane nawe kwamba mimi ni kati ya watu wanaoamini kwamba Zitto ni kati ya watanzania (nafikiri wengi) wanaoamini kwamba JK anaweza kufanya mabadiliko. Kwa hiyo ukimsikiliza kwa makini Zitto amekuwa mzito kumrushia makombora JK kama anavyowarushia wana CCM wengine. Sasa kama hii ni kweli au sio kweli yeye anajua zaidi kuliko sisi, sisi tunahisi tu kutokana na maneno yake. Hata hivyo, sioni kama hili ni tatizo. Hii ni kwa sababu kwenye siasa tunatofautiana misimamo na mikakati. Kwa mfano, mimi binafsi msimamo wangu ni kwamba CCM kama chama kimepoteza sifa ya kutawala na siamini kwamba kuna mtu anaweza kuibadilisha CCM ikawaweza kutoa uongozi tunaohitaji katika nchi, si Kikwete si nani. In fact, kwangu mimi ni bora Mkapa aliweza kuitikisa CCM ikabadilika, to worse or better, I am not sure. Kikwete ame-prove kwamba ni mtu asiyekuwa na style yeyote ya uongozi-yaani hata udikteta hauwezi! Kwa hiyo kwangu mimi kinachotakikana kwa sasa, as a first step to real change, ni kuwashawishi wananchi kuachana na CCM na kuing'oa madarakani.

Sasa kuna wengine wanaamini kwamba inawezekana tukaleta mabadiliko hata kupitia CCM tukiwa na watu kama akina Kikwete. Sasa hatuwezi kuwasuta au kuwalaumu watu wenye mawazo ya namna hii. Ni swala la kutofautiana mtizamo tu. Kwa hiyo sioni kasoro yeyote kwa Zitto kuonyesha uzito wa kum-criticise JK au hata kum-mind! Inawezekana yeye ni kati ya watanzania malioni waliopagawishwa na wanaoendelea kupagawishwa na Kikwete!
 

Angalau wewe umeongea objectively....
 
Shy,
Ndugu yangu yote hayo ya nini? Zitto kuenda Marekani na kupokelewa au kukutana na watanzania kuna tatizo gani? Hivi kuwa chama cha upinzani maana yake ni kuwa maadui? Je, unajuaje kuna wengine aliosoma nao, aliokuwa anawafahamu kabla na in general whats wrong kwa watu walio mbali na nyumbani kumfurahia mtanzania mwenzao awapo kwenye anga zao? Lazima kuna lingine la ziada hapa, kwani hata WIVU tu peke yake hautoshelezi hoja zako za chuki.

Nimesoma michango yako mingi hapa JF, lakini kwa nililosoma leo nimeishiwa na nguvu. Hivi kweli unawezaje kusema serious issues ambazo hazijapatiwa majibu ni mambo yaliyopitwa na wakati? Kama wewe kwa uelewa wako unaweza kusema hivyo hivi yule ambaye hana information kama uliyonayo wewe atasemaje?

Kwa maoni yako umedai upinzani unahadaa jamii. Je, CCM wanafanya lipi tofauti na hao upinzani na wao wangali madarakani? Na ni hadaa ipi unyozungumzia? Isingekuwa upinzani hata haya machache yaliyojitokeza na wananchi wakayashupalia yasingefikia hapa, sasa iweje uite ni wahadaaji wa jamii?

Ni vizuri na sahihi mtu kutoa maoni yake, lakini inapendeza zaidi watu wakitoa maoni yenye mlengo wa kujenga na sio blah blah. Ni vizuri watu wakatoa na mifano hiyo ya hadaa kwa jamii na sio tu kusema.

Binafsi yangu sioni kama kuna yoyote anayefanya la maana kati ya upinzani na hao CCM kwa wananchi wanaojidai wanawakilisha, lakini huenda ni makosa ya set up nzima ya nci ya Tanzania na watu wake. Ubabaishaji ni mwingi kuliko utendaji. Pamoja na hayo bado hatujachelewa na hatuzuiwi kutoa maoni yenye lengo la kuleta mabadiliko na maendeleo
yanayokusudiwa.

Hapa JF naona kuna mawazo mazuri tu na yenye mwelekeo, hivyo ni wajibu wetu kuliona hilo na kulifanyia kazi na sio kuvuruga vuruga mazungumzo kama wendawazimu. Watanzania kama wamehisi au wameona wameibiwa basi naamini wana haki ya kutaka kujua kulikoni na nini hatma ya wezi hao. Kama jibu halijatolewa ujue hilo halitapitwa na wakati kamwe na hasa ukizingatia tumeumia kiasi gani kimaendeleo na kimaisha. Ni lazima tupate majibu ya EPA, IPTL, rada, Kiwira na mengineyo. Na kwavile vianzo vipo, basi hatuna budi tupewe hadithi nzima na nani anahusika na nini hatma yao. Watanzania wote ni wadau kwenye haya.
 
Karibu JF. Hivi hizi online research unazofanya ndio hizi unazoandika humu?

Wandugu,

Unajua tunatofautiana akili, wengine tunaelewa kidogo kidogo sana. Mpaka sasa sijaona wapi wapinzani walipo wahadaa wananchi. Yaani wapi waliposema uongo au waliposema watafanya hili lakini hawakufanya.

Nimeona tu mijadala ya madini na Zitto na CUF kuwemo madarakani viongozi muda mrefu.

Au mi nasoma sielewi? naomba mnisaidie basi bandugu.

Kuhusu Shy, sina la kusema zaidi ya kuweka wazi kuwa ni kijana mdogo below 30 yrs; na hana uhusiano na Usalama wa taifa wala cheo kwenye CCM, YAP ana undugu na Maro huyohuyo mliemuulizia, PC technician. Hizo researches na kuandika vitabu sijui maana ni vipaji lakini shule ya vingi anavyodai anafanya HANA.
 
Mkuu FD,

wewe ni mkali maana jinsi nilivyokuwa namfikiria Shy ndo jinsi ulivyomdescribe na kumpa sifa zake kama inavyositahiri. chukua tano mkuu.
 
Kwanini asiwa organize watanzania wote hapa ili tuishinikize marekani watukabidhi mtuhumiwa as per agreement?
Ama ni kwasababu ameshapinga urafiki na Kikwete?

Zitto ana utashi wake na anafanya mambo kwa utashi wake unamtuma, sio kukurupuka tu, je kama ana shughuli nyingi. Je nia yake ya kwanza ni kukutana na watanzania huko? anafanya kwanza kirichpmpeleka na kuonana na watanzania ni chaguo si lazima ni mapenzi. Kwani wangapi wamekuja hapo na wahajaonana na watanzania. Usimuonee kijana wa watu, ukitaka kumshauri mwandikie PM, au mpigie simu kwani ariacha namba ya simu. wewe uko HUKO KWA NINI USINGEULIZA HIYO SERIKALI ARIPO BALALI
 

Sasa kama viongozi tunaowategemea kuwa wako upande wetu sisi kina nanihii... hawa rierezei wala kurizungumzia ribarari we unategemea sisi tufikiri vipi? Najaribu kumuuliza hivi sasa na kama hataki then mimi nitakusanya wamarekani hapa tupate "initiative" ya kuwakoma mafisadi!
Hivi kweli mi nimuonee Zitto?
 

Kwenye Serikali kuwatumikia wananchi wake kwa ujumla hapo ni urongo mtupu!
Kama that was the case then hata Wapinzani wasingepata umaarufu walionao hiv sasa!
 

Kwanini hakupewa uwaziri mkuu ama something ambayo ataweza kuwatumikia wananchi ipasavyo kimaamuzi?
Ye anakubali vipi kuwa cheap kiasi hicho?
Kwa nini yeye ndio amsikilize Kikwete tu kila siku!?
Je Kikwete naye keshawahi kumsikiliza hata siku moja?
Je atamsikiliza this time around?
Kwanini ajitoe mzima mzima kussapoti mambo amabyo bado hatujaona umuhimu wa kuyasapoti kwasababu ya namna wananvyodili na mafisadi?
Je Zitto amepinga urafiki na Kikwete kiasi cha kujipindua kiasi hicho?
JE ANAAMINI KUWA MABADILIKO HAYO YATAHUSISHA KUWAKWIDA MAFISADI KAMA BALALI NA CHENGE?
Ama they still share the same ideas with His Excellence kuwa wasijali kuitwa mafisadi?
 
Jmushi, hivi unatoka na mawazo tu bila kufikiria au unauliza alimradi uulize?

Kwanini hakupewa uwaziri mkuu ama

Hivi unajua nani anaweza kuwa Waziri Mkuu Tanzania, au Waziri Mkuu anapatikana vipi!?

something ambayo ataweza kuwatumikia wananchi ipasavyo kimaamuzi?

Tayari anawatumikia wananchi, amechaguliwa hawezi kusubiri kupewa dezo dezo!
Ye anakubali vipi kuwa cheap kiasi hicho?

Cheap kwa kipimo cha nani?

Kwa nini yeye ndio amsikilize Kikwete tu kila siku!?
Wangapi wanamsikiliza na kwanini asimsikilize kama wengine wakati JK ndio Rais? Hata wewe unamsikiliza hata kama hukubaliani naye!

Je Kikwete naye keshawahi kumsikiliza hata siku moja?

Hili ni swali la Kikwete au muulize Salva!

Je atamsikiliza this time around?

So umeassume hajawahi kumsikiliza?

Kwanini ajitoe mzima mzima kussapoti mambo amabyo bado hatujaona umuhimu wa kuyasapoti kwasababu ya namna wananvyodili na mafisadi?

Umejuaje kajitoa mzima mzima?

Je Zitto amepinga urafiki na Kikwete kiasi cha kujipindua kiasi hicho?

Kajipinduaje?

JE ANAAMINI KUWA MABADILIKO HAYO YATAHUSISHA KUWAKWIDA MAFISADI KAMA BALALI NA CHENGE?

Imani yake inahusiana vipi na yale yaliyo halisi? Kila mtu anaweza kuwa na imani fulani;

Ama they still share the same ideas with His Excellence kuwa wasijali kuitwa mafisadi?

Kwa hiyo katika mawazo yake umeamua kumuita Zitto naye fisadi kwa vile umeshindwa kutafuta majibu ya maswali yako?
 
 
Jmushi,

Unajichanganya sana kwenye posts zako hadi inakuwa vigumu kukujibu. Kuwa na kitu kimoja specific unachotaka kujibiwa na utajibiwa (if any). Unajichanganya sana mkuu hadi inatisha.
 
Ukweli ni kwamba upinzani hawana nyimbo kabisaaa wala game plan ya maana.

Halafu Mwanakijiji unaumwa au? Naona umebonyeza thanks mfululizo humu, sasa sijui kibao cha mall kimekufanya trigger happy?

Nzokanhyilu,
Tembelea websites za vyama vya siasa au hata ofisi zao upate kuona sera na strategic plans za vyama hivyo ili iwe uthibitisho wa madai yako. Kisha labda uje na criticism kama utaona policy na plans zao zina mapungufu ya haja. Usikubali kuendelea kula sumu hii na kuiambukiza kwa wengine, ati vyama havina cha maana. Endapo utakuwa na uthibitisho kwamba ni kweli havina, timiza basi wajibu wako kwa taifa kwa kutunga wewe mwenyewe kile unachoona kinalifaa taifa lako,kisha tafuta fursa ukiweke katika utekelezaji iliuliondolee taifa aibu ya ufukara,utegemezi na ufisadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…