Naona umeshajibiwa maswali yako yote isipokuwa hili nami nimeona nikujibu ili kukuweka sawa. Kwanza, nami nikubaliane nawe kwamba mimi ni kati ya watu wanaoamini kwamba Zitto ni kati ya watanzania (nafikiri wengi) wanaoamini kwamba JK anaweza kufanya mabadiliko. Kwa hiyo ukimsikiliza kwa makini Zitto amekuwa mzito kumrushia makombora JK kama anavyowarushia wana CCM wengine. Sasa kama hii ni kweli au sio kweli yeye anajua zaidi kuliko sisi, sisi tunahisi tu kutokana na maneno yake. Hata hivyo, sioni kama hili ni tatizo. Hii ni kwa sababu kwenye siasa tunatofautiana misimamo na mikakati. Kwa mfano, mimi binafsi msimamo wangu ni kwamba CCM kama chama kimepoteza sifa ya kutawala na siamini kwamba kuna mtu anaweza kuibadilisha CCM ikawaweza kutoa uongozi tunaohitaji katika nchi, si Kikwete si nani. In fact, kwangu mimi ni bora Mkapa aliweza kuitikisa CCM ikabadilika, to worse or better, I am not sure. Kikwete ame-prove kwamba ni mtu asiyekuwa na style yeyote ya uongozi-yaani hata udikteta hauwezi! Kwa hiyo kwangu mimi kinachotakikana kwa sasa, as a first step to real change, ni kuwashawishi wananchi kuachana na CCM na kuing'oa madarakani.
Sasa kuna wengine wanaamini kwamba inawezekana tukaleta mabadiliko hata kupitia CCM tukiwa na watu kama akina Kikwete. Sasa hatuwezi kuwasuta au kuwalaumu watu wenye mawazo ya namna hii. Ni swala la kutofautiana mtizamo tu. Kwa hiyo sioni kasoro yeyote kwa Zitto kuonyesha uzito wa kum-criticise JK au hata kum-mind! Inawezekana yeye ni kati ya watanzania malioni waliopagawishwa na wanaoendelea kupagawishwa na Kikwete!