Upishi wa Biskuti za Tangawizi

Jade_

Senior Member
Joined
Apr 19, 2015
Posts
122
Reaction score
214
Habari zenu wakuu, natumai mnaendelea vizuri. Jumamosi iliyopita niliwaletea mapishi ya wali, samaki wa nazi na mboga. Wiki hii nitapika Biskuti za Tangawizi.

Biskuti hizi zinaweza kuliwa na maji, chai, maziwa, kahawa, juisi nk. Usipomaliza kuzila muda huo unaweza kuzihifadhi kwenye kontena sehemu isiyo na jua.

Ukipenda kuangalia video ya haya mapishi unaweza kuangalia hapo chini. Ukipenda unaweza “kuilike” hiyo video, “kusubscribe” kwenye channel yangu na kuangalia video nyingine.


Mahitaji ya Biskuti za Tangawizi
350g Unga wa Ngano
1 tsp (kijiko cha chai) Magadi Soda
2 tsp tangawizi ya unga
115g siagi
175g sukari
4 tbsp (kijiko cha chakula) Golden Syrup
1 yai lililopigwa

Tunaanza kwa kuchekecha unga, magadi soda na tangawizi kwenye bakuli.


Unga wa ngano

Magadi Soda


Tangawizi


Nikichekecha unga, magadi na tangawizi

Baada ya hapo unaweka siagi iliyolainika, na kuichanganya mpaka mchanganyiko ufanane na chenga za mkate. Tunamalizia mahitaji makavu kwa kuchanganyia sukari.

Siagi laini


Nikichanganyia siagi


Nikiweka sukari

Tunaweka Golden Syrup (hii nilinunua supermarket) na yai liliopigwa na kuukanda mchanganyiko wetu kwa muda kidogo.

Golden Syrup


Nikipiga yai


Nikikanda unga


Baada ya kukanda unga wetu, tunausukuma kama chapati na kukata vipande kwa maumbo mbalimbali.

Nikisukuma mchanganyiko wetu


Nikitumia kikombe cha bati kukata vipande


Maumbo ya duara


Nikikata umbo kama mtu

Baada ya hapo, tunachukua vipande vyetu na kuviweka kwenye tray lililopakwa mafuta au siagi kwa ajili ya kuoka.

Nikiweka vipande kwenye tray


Vipande vikiwa kwenye tray tayari kwa kuoka

Ukioka kwenye oven, biskuti zitatumia dakika 10-12 hadi ziive kwenye joto la 190 C. Muda utakaotumia kuoka utalingana na namna unavyopenda biskuti zako ziive. Mimi nimependa zangu ziive zaidi na zitakaa muda mrefu zaidi.

Biskuti zikiwa kwenye oven


Biskuti zikiwa zimeiva


Biskuti za tangawizi


Biskuti za Tangawizi kwa ukaribu


Biskuti ya tangawizi kwa ndani
 

Attachments

  • Pic 04.jpg
    84.8 KB · Views: 74
Yasitokee tu mangumbaru yakaanza kusema eti una mikono mizuri...
 
Reactions: EEX
Mimi huku Maneromango nazipataje?Nataka za 10 elfu
 
Aisee!? Ipo vizuri
Nanikitaka vibiskuti lain kama vya etisamo naviandaeje
 
Iyo mikono yako ilivyo misafi nimetamani kula ivyo vidude
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…