Upishi wa Pilau ya Nyama na Kachumbari

Jade_

Senior Member
Joined
Apr 19, 2015
Posts
122
Reaction score
214
Hali zenu wana mapishi, natumai mpo salama. Wiki iliyopita nilionyesha namna nilivyopika biskuti za tangawizi. Leo nawashirikisha namna ya kupika pilau ya nyama na kachumbari. Hiki chakula kilisindikizwa na white sauce niliyopika h a p a.

Ukitaka kuangalia video ya haya mapishi unaweza kuangalia hapo chini. Ukipenda unaweza “kuilike” hiyo video, “kusubscribe” kwenye channel yangu na kuangalia video nyingine.

Turudi kwenye mapishi yetu.
Pilau
Nilianza kupika pilau kwa kukaanga vitunguu kwenye mafuta ya mzaituni (olive oil) mpaka vilivyoanza kunyauka. Baada ya hapo niliweka kitunguu saumu kilichotwangwa nikakangaa kidogo na baadaye nikaweka tangawizi na nikaendelea kukaanga.

Nikianza kukaanga vitunguu kwenye mafuta


Nikiweka kitunguu saumu


Nikiendelea kukaanga vitunguu baada ya kuweka tangawizi

Baada ya vitunguu kupata rangi, niliweka viungo vya pilau (pilau masala), nikakaanga kidogo na nikaongeza vitunguu vingine ili kuzimua harufu na ladha ya vitunguu visivyoungua. Nikakaanga kidogo halafu nikaweka vipande vya nyama vilivyopikwa na chumvi, nikakaanga tena.

Nikiweka viungo vya pilau


Nikiongeza vitunguu vingine


Nikiweka vipande vya nyama vilivyopikwa

Nilivyomaliza kuzikaanga nyama, niliweka maji ya moto nikafunika mchanganyiko mpaka ukachemka. Ulivyochemka niliweka majani ya bay (bay leaves) na nikaacha ichemke mpaka vitunguu vyote vikalainika. Niliweka maji ya moto ya kutosha nikaacha mchanganyiko uchemke tena.

Mchanganyiko baada ya kuweka maji ya moto


Nilivyoweka majani ya bay

Maji ya pilau yalivyochemka nilitoa majani ya bay na nikaweka mchele wa kawaida (sio basmati) ukachemka mpaka ukaiva.

Nikiweka mchele


Mchele ukichemka


Pilau imeiva

Kachumbari
Nilianza kutengeneza kachumbari kwa kuchanganya vinegar, olive oil chumvi na mnanaa (mint) uliyosagwa wenye sukari, nikaweka pembeni. Kwenye chombo kingine niliweka kitunguu na nyanya na baadaye nikamiminia mchanganyiko wetu tuliyotayarisha nikachanganyia.

Mchanganyiko wa vinegar, olive oil, chumvi na mnanaa wenye sukari


Mchanganyiko wa nyanya na vitunguu


Nikichanganya viungo vyote vya kachumbari


Pilau, kachumbari, na kwenye bakuli ni white sauce


Pilau, kachumbari na white sauce kwa ukaribu
 
karbu nkufundishe pilau la nyanya nikikupikia huitaji hata kachumbali kwa utam
 
Natamni nipike sikumoja pilau ya nyanya sijawah jaribu
Hutaacha ukilianza na walaji wataona utofauti. Lina ladha yake ya kipekee, huo mchanganyiko wake kabla ya kuweka mchele, ni kama roast fulani. Mtu akiliona mwanzoni hatojua unapika pilau, akila sasa 😋😋😋😋
Jaribu siku dear sophy27 utanipa mrejesho.
 
Nyanya ni tomato paste au za kawaida ndio nzuri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…