Upishi wa Wali, Samaki wa Nazi na Mboga

Jade_

Senior Member
Joined
Apr 19, 2015
Posts
122
Reaction score
214
Habari za Jumamosi wakuu, natumai mpo salama. Leo nawaletea mapishi ya wali, samaki wa nazi na mboga.

Ukipenda kuangalia video ya haya mapishi unaweza kuangalia hapo chini. Ukipenda unaweza “kuilike” hiyo video, “kusubscribe” kwenye channel yangu na kuangalia video nyingine.
Turudi kwenye mapishi yetu.

Wali
Nimeanza kwa kuchambua na kuosha mchele. Nimetumia mchele wa kawaida, sijatumia basmati kwa sababu siupendi kwa kutokua na harufi wala ladha yake yenyewe.


Kuchambua mchele


Kuosha mchele


Baada ya mchele kuwa safi nimeuweka kwenye sufuria na maji ya wastani. Nimetia mafuta, chumvi, nimekoroga na kuanza kuupika.


Mchanganyiko wa wali ukiwa jikoni

Baada ya muda maji yamekauka na wali wetu umeanza kuiva. Nimeugeuza ili uive kote na nimeongeza maji ya moto kidogo sana ili mvuke uusaidie wali kuiva. Nimefunikia mpaka umeiva kabisa.


Nikigeuza wali wangu



Nikiongeza maji kidogo sana ya moto


Wali ukiwa tayari



Samaki

Samaki aina ya sato


Nimemtayarisha samaki aina ya sato kwa kukwangua magamba yake, kuondoa mapezi (wengine wanayaacha au wanayatoa na kuyakaanga pembeni) na ute kwenye kichwa.


Nikikwangua magamba ya samaki


Nikiondoa mapezi na ute


Samaki akiwa msafi

Baada ya hapo samaki wangu nimempaka chumvi ya kutosha na kumkaanga kwenye mafuta kidogo yaliyopata moto hasa. Baada ya muda nimegeuza vipande vyangu vya samaki mpaka vimeiva vizuri. Nimetoa samaki jikoni na kuweka pembeni


Nikipaka vipande vya samaki chumvi


Naanza kukaanga samaki kwenye mafuta kidogo


Nikigeuza samaki


Samaki zimeiva


Nimeanza maandalizi ya mchuzi wa samaki kwa kukatakata vitunguu na nyanya

Nikikata nyanya na vitunguu


Kwenye kile chombo nilichokaangia samaki nimeanza kukaanga vitunguu. Baada ya kupata rangi kidogo nimeweka chumvi na kitunguu saumu na kukaanga kwa muda kidogo.

Nikikaanga vitunguu


Nikiweka kitunguu saumu


Baada ya hapo nimeweka nyanya na kuziacha mpaka zimelainika kabisa na kuwa mchuzi. Nimehamishia mchuzi wangu kwenye sufuria nyingine ili inirahisishie mapishi.

Nimeongezea nyanya kwenye vitunguu


Mchuzi wangu ukiwa tayari na kwenye sufuria nyingine

Nimekorogea tui la nazi taratibu kwenye mchuzi na nimeendelea kukoroga mpaka umechemka. Ulivyochemka, nimeweka vipande vya samaki nilivyokaanga na nimekamulia limao. Nimeacha imechemka kidogo ndio nikatoa jikoni.

Nikikorogea tui la nazi kwenye mchuzi wangu


Nikiweka vipande vya samaki vilivyokaangwa kwenye mchuzi


Nikikamulia limao


Mchuzi ukiwa tayari


Mboga

Kwa pishi la leo mboga tunazotumia ni mchanganyiko wa “chinese” na “spinach”. Unazikatakata na kuzichanganya kwenye sufuria pamoja na mafuta.

Nikikatakata mboga


Mboga zikiwa jikoni



Zikianza kuiva katia kitunguu na ukorogee kwenye mboga pamoja na chumvi. Acha mchanganyiko ukae jikoni mpaka vitunguu viive kidogo alfu utoe motoni.

Mboga na vitunguu jikoni


Mboga ikiwa tayari


Upakuaji

Nikipakua wali kwenye sahani


Nikiweka samaki na mchuzi wake juu ya wali


Nikiweka mboga kwenye sahani
 
Ila lakini anayekata mboga za majani na anayepakua wali ni watu tofauti. How hapo?
Macho yako kama yangu. Nadhani ni bibi na mjukuu wanafanya mapishi.

Kongole kwao
 
All in all chakula kinaonyesha ni kitamu, usafi umezingatiwa...
Binafsi ni mpenzi wa kupikia nazi, hapo umenifikisha.. hongera
 
Kwa huu uzi na mida hii, tayari nishasikia njaa ngoja nitoke sasa nikatafute msosi
 
Hongera sana , nimepata hamu ghafla. Bila shaka faza hausi anafurahia sana mapishi ya nyumbani kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…