Asante kwa hoja nzuri.
Nipo katika kundi la wasioangalia mtu anayetoa ushauri, bali huangalia ushauri wenyewe, kuupima na kuuchekecha, niukubali au niukatae kwa mantiki za uzuri au ubaya wake bila kujali sana aliyetoa ushauri..
Kwa maana unaweza kupata ushauri mzuri kutoka kwa mtu dhalili, na unaweza kupata ushauri mbaya kutoka mtu jalili.
Hata saa mbovu iliyosimamainakuwa sahihi mara angalaumoja kwa siku.
Hata kichaa anaweza kusema kitumuhimu.
Waswahili walisema "Akwitao usiize, enenda kapulikize. "
Hapana. Kupulizika si kuvuta ulichofikiria.Ni Kiswahili tu.
Nilishawahi kufikiri ingekuwa vipi kama hapa JF watu wote tungekuwa na jina mojahalafu tusome kilichoandikwa tubilakukilinganisha na aliyekiandika.
Kwa upande mmoja ingekuwa vizuri kwa maana ya kwamba tungeangalia dhana tu, badala ya kuangalia watu.
Kwa upandemwingine, kujibizana ingekuwa vigumu zaidi.