Hapa nahisi kama napigwa changa la macho, inawezekana gari kutembea kwa tairi tatu pekee? JamiiCheck, na wajuvi wa masuala haya mtujulishe lipi ni lipi
- Tunachokijua
- Magari yenye magurudumu manne lakini yanaweza kwenda kwa magurudumu matatu ni kutokana na kuwezeshwa na Suspension ya Hydropneumatic ambapo Magari kama Citroën DS yana mfumo wa kipekee wa suspension unaoweza kurekebishwa, kuruhusu gari kuendeshwa kwa magurudumu matatu ikiwa tairi limehitaji kubadilishwa au Matumizi ya dharura ambapo Uwezo huu ni kwa hali za dharura, na inashauriwa kuendesha polepole, hasa unapopinda.
Tovuti ya CarScoops inaeleza kuhusu video za magari ya Citroën ya zamani zikiendeshwa kwa matairi matatu. Modeli zilizo na mfumo wa hydropneumatic suspension, kama Citroën DS ya zamani, zina uwezo maalum unaokuwezesha kuinua upande wa gari ili kubadilisha tairi bila kutumia jack.
Ukitafuta kwa haraka YouTube, utapata video nyingi za watu wakiendesha Citroën kwa matairi matatu tu, huku brake drum au disc ya upande ambao tairi limeondolewa ikibaki juu bila kugusa barabara. Hata mchezo huu ulionekana kwenye kipindi cha televisheni miaka ya 1970.
Maonyesho haya kawaida hufanywa kwa mwendo mdogo, kwa sababu ingawa gari linaweza kwenda kwa matairi matatu, haliwezi kuwa thabiti kama lingekuwa na matairi manne.
Tovuti ya Citroenvie inaeleza historia ya mhandisi ambaye alivutiwa na suspension ya Citroën kiasi kwamba aliiondoa mkono wa kulia, akafunga mistari ya breki na kuendesha gari kwa magurudumu matatu hata hivyo alikamatwa mara kadhaa na polisi lakini alishinda mahakamani kwa kukosekana uthibitisho dhidi yake.