Upo uwezekano mifumo ya bandari inahujumiwa kubariki uwekezaji tarajiwa?

Upo uwezekano mifumo ya bandari inahujumiwa kubariki uwekezaji tarajiwa?

mwanamichakato

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2015
Posts
1,188
Reaction score
1,090
Kwa Siku kadhaa sasa mifumo ya bandari haifanyi kazi hivyo kupelekea wadau ktk Masuala ya forodha kukwama kutoa mizigo mbalimbali.

Mkwamo wa System Kwa muda mrefu huleta usumbufu mkubwa ,hasara kubwa na taswira hasi kuhusu bandari na Taifa Kwa kuzingatia ushindani uliopo ktk ukanda tuna bandari Shindani Beira,Durban,Welvis Bay,Mombasa..

Kama ilivyowahi kulipotiwa kwenye upatikanaji wa shida wa umeme kwama wafanyakazi wa Mabwawa ya kuzarisha umeme walihujumu ujazo wa maji ili wajinuafaishe wao na wengine ktk mnyororo Upo uwezekano pia kutokana na songombingo la Mkataba wa bandari..

Wito,Vyombo vya Siri vya usalama wa nchi vifuatilie na kuchukua hatua kali dhidi ya wote wanaohujumu mifumo na kusababisha hasara Kwa Taifa letu.

Nawakirisha
 
Hii nchi ngumu sana ngoja nitafute mashamba mabondeni huko nilimage tu niwe na chakula nifuge niachane kabisa na mambo ya kitaifa
 
Hii nchi ngumu sana ngoja nitafute mashamba mabondeni huko nilimage tu niwe na chakula nifuge niachane kabisa na mambo ya kitaifa
Ukifanyikiwa tu wanakuja Dubai kukuchukua wewe na bonde lako!SOLD OUT!
 
Si jambo la ajabu mifumo kuchezewa Kwa nia ovu..

Taasisi zetu Za usalama Nina imani zina uwezo wa kudhibiti..

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom