KWELI Upo uwezekano wa funza kuishi kwenye sikio la binadamu na kusababisha ugonjwa wa Myiasis

KWELI Upo uwezekano wa funza kuishi kwenye sikio la binadamu na kusababisha ugonjwa wa Myiasis

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Salama wanajamvi?

JamiiCheck naomba msaada wa kupata uhalisia wa hili kwamba wapo funza wanaoweza kuishi kwenye sikio la binadamu, je, ni kweli? na kama ni kweli kuna madhara gani na tunaepukaje?

1751617848720.png

​
 
Tunachokijua
Kupitia Jukwaa la afya mdau wa JamiiForums alianzisha mada iliyoeleza uwezekano wa Funza kuishi ndani ya sikio la binadamu na kusababisha madhara katika eneo husika, huku akieleza chanzo cha funza kuwa ni mayai ya nzi ambayo baada ya kutotolewa mathalani sikioni hugeuka kuwa funza. Baadaye mdau mwingine kupitia Jukwaa la JamiiCheck alitaka kupata uhalisia zaidi juu ya mada hiyo.


Ufuatiliaji wa JamiiCheck


Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kupitia ripoti za kisayansi umejiridhisha kuwa ni kweli upo uwezekano unaosababishwa na mayai ya nzi ambayo yakitotolewa katika sikio hugeuka na kuwa lava (funza).

Ripoti ya Wiley online library iliyochapishwa katika Maktaba ya taifa ya tiba, nchini Marekani (NIH) Inafafanua Myiasis ya sikio kuwa ni uvamizi wa sikio na funza (hatua ya lava ya nzi). Katika maandiko ya kisayansi, kuna visa vichache tu vilivyoripotiwa kuhusu myiasis ya sikio. Hali hii hupatikana zaidi katika maeneo ya kitropiki, ambako unyevunyevu na hali ya hewa ya joto hutoa mazingira mazuri kwa uvamizi huu.
​
405_2007_535_Fig1_HTML.jpg

Hali hiyo ni kawaida miongoni mwa wanyama wanaonyonyesha. Kwa binadamu, huonekana zaidi katika maeneo ya vijijini ambako watu wako karibu zaidi na wanyama. Ugonjwa huu hutokea pale nzi jike anapoweka mayai, ambayo baada ya muda mfupi husababisha dalili za kiafya kulingana na sehemu ya mwili iliyoathiriwa.

Pia inaweza kutokea endapo vidonda au maambukizi hayatatibiwa ipasavyo. Nzi huvutiwa na harufu ya maambukizi, na huweka mayai yao eneo hilo, ambayo huchanua na kutoa funza (lava), na hivyo kuzidisha zaidi tatizo la maambukizi.

Sababu zinazoongeza hatari ya myiasis kwa binadamu ni pamoja na maambukizi ya sehemu ya kati ya sikio (otitis media) kuogelea katika maji yaliyotuama, kutokuzingatia usafi wa mwili, ugonjwa wa kisukari (diabetes mellitus). Vigezo vingine vinavyoweza kuchangia ni watoto waliotelekezwa, uzee, matatizo ya akili, na usafi duni wa mwili.

Kwa kawaida waathirika wa hali hii wamekuwa wakilalamika kuhusu maumivu ya sikio, kupoteza uwezo wa kusikia, usaha au damu kutoka sikioni, kuwashwa ndani ya sikio, na/au kelele masikioni (tinnitus). Dalili nyingine zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kizunguzungu, udhaifu wa misuli ya usoni na mara nyingi dalili huanza baada ya lava waliowekwa kuanza kulisha tishu zinazowazunguka. Uvamizi huu kwa kawaida hugunduliwa kupitia historia ya mgonjwa na uchunguzi wa kitabibu, ambao utaonyesha kuwepo kwa lava ndani ya sikio. Mara chache sana huhitaji vipimo vya ziada kwa ajili ya utambuzi, kwa sababu lava hupatikana karibu na mfereji wa nje wa sikio, kwani wanahitaji hewa kwa ajili ya kupumua.

Ripoti hiyo inaeleza kisa cha Mvulana wa miaka 12 ambaye aliripotiwa kuwa na maumivu ya sikio upande mmoja kwa muda wa siku tatu. Uchunguzi wa sikio lenye maumivu ulionyesha kuwa na tundu kwenye utando wa sikio (tympanic membrane) pamoja na funza (lava) ndani ya sikio la kati. Funza hao walitolewa kwa kutumia forceps (kifaa cha kushika) na kusafisha sikio kwa upole kwa maji ili kuondoa mabaki yoyote.

Ili kuepuka hali kama hizi ambazo ni nadra lakini hatari zinazapotokea, ni muhimu kudumisha usafi wa masikio na kutafuta matibabu mapema endapo kuna maambukizi ya sikio. Hapa kuna hatua kadhaa za kuzingatia:

Usafi wa Kawaida, Hakikisha masikio yanakuwa safi na makavu, Tiba kwa Wakati, Usipuuze maumivu ya sikio yanayodumu au usaha unaotoka sikioni, kuzingatia ukaguzi wa Mara kwa Mara, Kufanya uchunguzi wa masikio mara kwa mara kunaweza kusaidia kugundua na kutibu matatizo mapema.​

Attachments

  • 1751610972927.png
    1751610972927.png
    4.2 MB · Views: 35
Back
Top Bottom