Upofu na uoni hafifu

Upofu na uoni hafifu

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha uwepo wa watu takriban bilioni 2.2 wenye changamoto za macho zinazohusisha upofu na uoni hafifu.

7029A3D3-18C9-4BE2-85DC-154E6B9698F4.jpeg


Kwa kiasi kikubwa, changamoto hizi zinaweza kuepukika kwa kushughulikia vizuri magonjwa yanayoweza kudumaza afya ya macho mfano kisukari na shinikizo kubwa la damu pamoja na kupata haraka msaada wa uchunguzi na tiba inayohusisha changamoto zote za macho.

Aidha, mlo huwa na mchango mkubwa katika kuboresha afya ya macho pamoja na kuzuia kutokea kwa upofu na uoni hafifu.

Vyakula vyenye Vitamini A kama vile karoti, mafuta ya samaki, maini ya wanyama na mayai pamoja na vyakula vyenye vitamini E mfano parachichi, vyakula jamii ya karanga, broccoli na spinachi hufaa kwa kazi hii.

Changamoto nyingi za macho hutibika kirahisi pindi zinapogunduliwa mapema. Wahi kituo cha afya pasipo kusubiri unapohisi kuwa macho yako hayapo sawa.

Chanzo: WHO
 
Back
Top Bottom