Gwappo Mwakatobe
JF-Expert Member
- Nov 22, 2019
- 1,730
- 2,230
Natoa ushauri kwa mtu yeyote aliye katika hali ya kupitia machungu (bitterness), kutelekezwa au kukataliwa (rejection), msongo wa mawazo (stress) au mfadhaiko/upweke (depression), aanze kufanya au kufikiria lolote lililo zuri, lolote lililo safi, lolote lenye haki, lolote lenye staha, lolote lenye sifa njema, lolote lenye ukweli, lolote lenye kupendeza na lolote lenye heshima.
Inaweza kuwa ni kufanya usafi, kusikiliza nyimbo au muziki aupendao, kufanya mazoezi au kutembelea mandhari nzuri kama milima, misitu au fukwe. Aidha, atazame picha, michezo au filamu anazopenda, au aangalie ndege na wanyama wampendezao. Ila yote hayo yanatuliza tu machungu kwa muda mfupi sana. Ni suluhisho la muda mfupi.
Kwa suluhisho la kudumu, anza kumshukuru Mungu kwa kukupa uhai na uzima ulionao sasa, ambapo unapumua vizuri wakati wengine wamelazwa hospitalini au wameishakufa. Mungu kakuongezea siku ya leo ili utimize kusudi lake alilokuleta duniani, ikiwemo kumwabudu Yeye pekee katika roho na kweli.
Baada ya hapo, tubu kwa Mungu makosa yako na tubu kwa uliowakosea kama wapo karibu au unaoweza kuwasiliana nao. Aidha, malizia kwa kuwasamehe wote waliokukosea.
Kisha, kwa kumaanisha moyoni mwako popote ulipo sema hivi: "Yesu Kristo karibu moyoni mwangu uniokoe niwe mwana wa Mungu kwa kuzaliwa upya rohoni na kuongozwa na Roho Mtakatifu." Amani utakayoipata moyoni mwako ni ya pekee sana! Mpe Mungu utukufu, sifa, heshima na shukrani.