Upotofu!

Upotofu!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba mpya iliyo chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba,imekaribisha maombi ya wananchi wanaohitaji kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Tume ikatoa pia utaratibu wa jinsi ya kuwapata wajumbe hao Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.

Leo,katika mitaa ya Mikocheni B,wanapita 'watu' wakiwa na ujumbe. Wanawataka wananchi wote wapeleke barua za kuomba nafasi ya Ujumbe wa Mabaraza ya Katiba bila ya kukosa. Wananchi wa huku wanaaminishwa kuwa wasipopeleka barua hizo,hawatapiga kura za kuiidhinisha Katiba mpya wakati wake ukifika. Upotofu!

Kuwa Mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ni hiyari ya mtu. Iweje watu walazimishwe? Kuiidhinisha katiba mpya ni haki ya kila mwananchi mwenye akili timamu na mwenye umri wa kupiga kura. Iweje,kukosa kuomba nafasi ya ujumbe kusababishe kukosa haki ya kupiga kura? Upotofu mkubwa!

Wananchi kwanza waelimishwe kabla ya kutakiwa kuandika barua husika. Umbumbumbu juu ya jambo hili la kikatiba unasababisha wengine kuwapotosha wananchi.
 
Back
Top Bottom