Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 520
- 2,930
Hii naomba Serikali kupitia @wizara_elimutanzania , @owm_tz @ormipango_uwekezaji waone hili.
Nchini Tanzania sasa hivi kuna tatizo kubwa sana la upungufu wa Accomodation Hostels kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu. (Nyumba za Malazi kwa Wanafunzi). Hii ina maana ya kwamba vyuo vingi nchini vina upungufu mkubwa wa Hostels za Wanafunzi kutokana na idadi yao kuongezeka kila Mwaka.
Tatizo hili ni la muda mrefu lakini Mwaka baada ya Mwaka,tatizo hili linazidi kuwa kubwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi katika vyuo mbalimbali nchini vya umma hata binafsi. Mfano ,awali vyuo vingi nchini vilikuwa na uwezo wa kutoa Malazi kwa wanafunzi wa Mwaka wa kwanza wote wakapata kutokana na ugeni wao wa mazingira,na rooms zingine zinazobaki wanapewa watu wenye uhitaji Maalumu na wanafunzi baadhi wanaoendelea.
Upungufu ukazidi kuwa mkubwa kiasi cha kwamba Mwanafunzi wa Mwaka wa pili na wanaoendelea (Continuous Students) wakawa hawapewi tena accommodations isipokuwa kwa wenye mahitaji Maalumu tu.
Hivyo, inafanya Wanafunzi wote wakiingia Mwaka wa Pili tu wanatafuta vyumba /nyumba za Kupanga nje ya chuo, ikawa wanaokaa Hostels za chuo ni Mwaka wa Kwanza na watu wenye mahitaji Maalumu.
Hali ilivyo sasa katika vyuo vingi Tanzania ni hali mbaya sana (it is the worst ). Hata wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza na Wanafunzi wenye uhitaji Maalumu sasa hivi wengi wanakosa Hostels,kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya wanafunzi vyuoni. Hali hii utaikuta @udsmofficial , @sokoineuniversity na vyuo vingine vingi nchini. Angalau @udomtheofficial wao hawapatii changamoto hii sababu wana Hostels za kutosha.
Ni wazi huko mbele kutakuwa na ongezeko kubwa sana la wanafunzi kwenda vyuo vikuu ,ni lazima serikali iwe na mikakati na mipango ya kuongeza hostels za wanafunzi katika vyuo hivyo.Sio lazima serikali ijenge ,ila serikali isaidie kutafuta wawekezaji wa ndani au wa nje wajenge.
Mfano UDSM wana ardhi kubwa pale ni suala la kupata muwekezaji tu kujenga ili Wanafunzi waondokane na changamoto ya Kupanga nje ya Chuo (Off-campus) sababu ni gharama kubwa , mazingira ya usalama, vishawishi kwa Dada zetu huko mtaani , pia ina punguza focus ya masomo kwa Wanafunzi.
Mamlaka walione hili .
Abdul Nondo.