Upungufu wa Mvua Nchini: Tuwaulize Wanasayansi au tumtegemee Mungu?

Upungufu wa Mvua Nchini: Tuwaulize Wanasayansi au tumtegemee Mungu?

Mtondoli

Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
70
Reaction score
174
Wananzengo wenzangu tunaotegemea mpini wa jembe kuendesha maisha yetu, leo ni tar 23 desemba huku kwetu rukwa na katavi hatujaonja mvua. Nimejaribu kuwauliza wazee wameniambia haijawahi tokea mpaka tarehe hizi mvua hamna, wakati dar kulikuwa mvua kubwa mpaka mafuriko rukwa haijanyesha bado

Jambo hili lina mitazamo mingi.wengine wanadai nchi inapaswa kutubu kwa maana hiyo tuwaite mitume, manabii, wachungaji, mashekhe wafanye maombi ya pamoja au wanasayansi waje watuambie kisayansi hii maana yake Nini? Naamini Kuna Jambo linatakiwa lifanyike
 
Zama huwa zinabadilika sio Jambo la ajabu Sana kivile hivyo tufungeni mikanda mwaka ujao kifupi tutatafutana
 
Haya ni mabadiliko huwa utokea kila baada ya mda.
Wa kulaumiwa ni sisi wa kutegemea kilimo cha kizamani cha mvua,
 
Pia mabadiliko ya tabia ya nchi yanachochea.ongezeko za joto linafanya mgandamizo kubadilika hivyo msukumo unapokuwa haupo ni tatizo
 
Tumuulize Lowassa anaweza kutusaidia kutengeneza mvua.
 
Back
Top Bottom