Upuuzi wa Masoud Kipanya

Mkuu nilimuona akiitambulisha TBC1 ni kali kinoma mi naitafuta kwa udi na uvumba pia alisema ukiuziwa zaidi ya 3,000 kashitaki. Kuhusu maisha plus ni kila baada ya miaka 2 so mwakani kitu hewani.
my take: kile kichwa ni noma kinaona mbali na kufahamu mengi na makubwa sikuwahi kufikiria.
 
wakuu! tunatakiwa tuone kilichomo ndani ndo tutoe maoni! yeyote anayejua kinapatikana wap atujulishe hapa...
 
Mi namkubali sana huyu jamaa,lazima kijitabu chake nikitie mkononi.
 
Yeh, he is a guy emboded with exceptional intellectual ability and creativity. Is extra genius!!





[h=3]PRESS RELEASE YA KUZINDUA DOCUMENTARY YA ''UPUUZI WA MASOUD KIPANYA''[/h]

UPUUZI WA MASOUD KIPANYA its a 47 minutes documentary ambayo Masoud himself recorded since mwaka juzi katika mazingira ya kijiji kilichotumika kurekodia MAISHA PLUS.....guese you know wat i mean.....



In his own words,KP says ''Mfumo nilioutumia ni kuongelea mambo mengi mchanganyiko na ili kuondoa uchovu wa kunitazama nikiongea, nimechanganya footages za videos, illustrations na animation (katuni) kuchagiza yale ninayokuwa nayazungumzia.

Ujumbe wa dvd hii ni nadharia ya vipande 26 vya keki. nikatengeneza MFANO wa uwepo wa idadi hiyo ya vipande vya keki ambavyo mara baada ya kuwekwa mbele ya watu (watanzania), kundi hilo la watu likataka kutoana roho ili kila mmmoja apate kipande cha keki hiyo, bahati nzuri wakatokea werevu (viongozi) ambao waling'amua kuwa kumbe idadi ya vipande vya keki (26) ni sawa kabisa na idadi ya watu waliokuwepo ambao walikuwa wanakaribia kutoana roho.

Werevu hawa wakawaambia watu hawa kuwa hatuna haja ya kung'oana meno wakati idadi yetu ni sawa kabisa na vipande vilivyopo, ukatengenezwa uataratibu wa kupanga foleni ili kila mmoja apite mbele achukue KIPANDE chake. baada ya kukubaliana hilo, bado werevu wakaona ni vema foleni hii iangalie walio dhaifu ili wawe mbele wawahi kupata keki kuchelea kuanguka kwa njaa.

Wakati vipande hivi vya keki vilipoanza kugawiwa, hawa viongozi, (watatu) wakaamua nao kwa kuwa ni sehem ya watu 26 kuchukua VIPANDE VYAO MAPEMA, bahati mbaya baadhi yao kutokana na kuwa karibu na meza ya keki na kutokana na ULAFI, wakaamua kuchukua zaidi ya kipande kimoja cha keki hali iliyopelekea watu wa mwishoni katika foleni ile kukosa vipande vyao.Dvd hii pia imeingia ndani kwa mafumbo kiasi kuangalia sababu inayopelekea watu kutaka kujipendelea zaidi kiasi cha kupelekea kudhulumu wengine, ikajaribu pia kuangalia dawa inayoweza kutumiwa kuepuka hali hii ya uchu na tamaa inayosababishwa na hofu ya kujiuliza nitapata lini na woga wa kuhofia kupoteza kidogo alicho nacho mkononi.


Kwanini umeitwa upuuzi? Masoud Answers ''kwa sababu ya tabia na hulka za binaadam kupenda kupuuza kila kitu, ni hili nalo limetengenezwa ili ulitazame kisha ulipuuze....''
Concept: Ni documentary yenye sauti na picha za video pamoja na katuni mnato na katuni mtembeo (still cartoons and animation)

Main Characters: Masoud Kipanya himself

Imeingia sokoni jana jumanne tarehe 15-11-2011 na inasambazwa na UMOJA AUDIO VISUAL.
Bei: Shilingi buku 3,000 tu.

Running time: Dakika 47

Sponsors: Hakuna mdhamini.

Future plans: Ni matayarisho ya upuuzi mwingine "WENYE NGUVU NA WAPAGAZI"

Nashukuru kwa ushirikiano wenu na mungu awabariki sana

Regards,
MASOUD KIPANYA.


 
Ukiwa mbunifu hulali njaa hapa mjini, haya Kipanya tutakuunga mkono japo copy 2 tutanunua....
 


Wasiwasi wangu ni hivi vidole.
Asije akasababisha machafuko na upotevu wa amani.
 
Ametuma ujumbe gani kwa Serikali na CHADEMA kwa cover yake hiyo?
 
Nae si member humu atuambie wamatumbi wa ugaibuni watapataje hii DVD
 
Nae si member humu atuambie wamatumbi wa ugaibuni watapataje hii DVD

NI kweli mkuu maan ainaonekana tumesahauliwa!! Maana hizi ladha za kibongo ni adimu!! Haya ma-drama ya wazungu yamechosha sasa!!
 
Na ndiyo maana clouds walishindwana naye, hicho kichwa wakuu. Wakaamua kubaki na magumegume ya magamba hadi leo, wanaelekea kuzimu. wehu sana clouds
 
jamaa amelenga soko ktk wakati muafaka, hadhira sahihi. safi masoud kipanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…