Upweke unauma, natafuta mwenza

coco bella

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2016
Posts
305
Reaction score
315
Nimechoka kuwa mpweke Mimi, nimechoka kugalagala peke yangu jamani.

Mimi ni mdada umri miaka 28, kabila Mngoni, mweusi kimo cha wastani.

Natafuta mkaka anayejielewa sina ubaguzi wa dini kabila lolote akiwa Msukuma, Muhaya na Mnyamwezi nitafurahi zaidi.

Awe anajishughulisha kwa chochote, sitaki wanafunzi wa chuo ni wasumbufu aisee. Nahitaji mahusiano ya kudumu aliye serious ani PM.

Ninaishi Mbezi Msakuzi nyumba yangu kubwa nahitaji mwanaume wa kuunguruma jamani.

NB: Muonekano wowote, kilema si ugonjwa
 
Rondom selection could be worth and give answers to your prayers
 
Kwakuwa unahitaji kampani na mtu wa kukutolea upweke, hilo halina shida bi dada
 
Kweli Mungu hamtupi mja wake, ngoja niwahi mapema kabla hii pension ya Coroshow haijaisha.
Na cha kufurahisha zaidi mimi ni chotara wa Kisukuma, Kihaya na Kinyamwezi.
Kubwa zaidi nina uzoefu mkubwa kwenye kukoroma wakati nimelala , hata mbu hawatokusogelea.
Karibu my future wife.
 
Juzi niliandima mahali upweke ni balaa, unasumbua sana, unaudhi sana, vijana wa 25 to 30 wanapitia hii changamoto, kibaya uwe ant social utaumia

Pole sana dada hali yako naielewa, tupo kwenye kapu 1
 
Tegemea kupata waganga njaa tu ,, 🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…