Upweke unauma, natafuta mwenza

Upweke unauma, natafuta mwenza

ID Mpya hizi.
COCO.jpg
 
Kweli Mungu hamtupi mja wake, ngoja niwahi mapema kabla hii pension ya Coroshow haijaisha.
Na cha kufurahisha zaidi mimi ni chotara wa Kisukuma, Kihaya na Kinyamwezi.
Kubwa zaidi nina uzoefu mkubwa kwenye kukoroma wakati nimelala , hata mbu hawatokusogelea.
Karibu my future wife.
Kwahiyo mleta mada nianze kumuita wifi?[emoji6]
 
Wanyamwezi jamaani bahati ya mtende hiyo!!
Nimechoka kuwa mpweke Mimi, nimechoka kugalagala peke yangu jamani.

Mimi ni mdada umri miaka 28, kabila Mngoni, mweusi kimo cha wastani.

Natafuta mkaka anayejielewa sina ubaguzi wa dini kabila lolote akiwa Msukuma, Muhaya na Mnyamwezi nitafurahi zaidi.

Awe anajishughulisha kwa chochote, sitaki wanafunzi wa chuo ni wasumbufu aisee. Nahitaji mahusiano ya kudumu aliye serious ani PM.

Ninaishi Mbezi Msakuzi nyumba yangu kubwa nahitaji mwanaume wa kuunguruma jamani.

NB: Muonekano wowote, kilema si ugonjwa
 
Hakuna siri hapo, ni ukweli ulio bayana[emoji23][emoji23][emoji23]
Wacha weeh, kwaiyo ukaona ntafaidi sana kwenda kuishi Mbezi ukaona uniharibie.
Wewe kile kigezo chako cha "Pesa mbele kama tai" sikiwezi kwakweli.
 
Mungu kaumba aisee hivi MTU unawezaje kupenda mwenye mwonekano wowote? ahaaaa inna nikijipitisha na pande langu LA mwanaume unaanza kunikodolea, never write something under stress, itakucost.

Ila wadada tuna unafiki, si kasema hata kilema sawa ajitokeze uone.

Kukosoa uumbaji wa mungu ni dhambi ushaandika yote hayo sentence ya mwisho ilibidi uachane nayo nina uakika sicho kilicho moyoni mwako.

😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁 nalog off.
 
Back
Top Bottom