Upwork : Sababu 4 kwanini unakosa kazi (from verified member with 90%+ job success rate)

GLOBAL CITIZEN

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2014
Posts
767
Reaction score
1,657
Peace JF Masssive 🤜🏾

Kipindi hiki cha covid 19 watu wengi sana wamekuwa wakitatufa njia zakuingiza side income angali wakiwa home. Na niseme tu baada ya kuandika uzi huu

Watu wangi wamechangamkia fursa kufanya kazi kama freelancers lakini ni wachache tu ndiyo wanafanikiwa kwenye platform ya UpWork.

Sasa hili jambo linaleta hasira sometimes. Unaweza dhani Upwork wanakufanyia hujuma [emoji2].

Kwa kawaida UpWork wapo na standards za juu sana. Wanataka top freelancers ili walinde hadhi yao. Kumbuka UpWork client ni kama mfalme. UpWork wanawatoza pesa nyingi kwahiyo client nayo wanategemea kupata Freelancers wenye ujizi usio wakubabaisha.

Hapo ndipo tatizo linapoanzia.

Sababu ya kwanza kwanini unakosa kazi kama beginner.

1 • Iwapo utafanikiwa kutuma maombi na kukubaliwa, basi kwasababu wewe ni beginner profile yako haitokuwa inaonyeshwa kama inavyotakiwa kwa clients wanaotafuta freelancers wenye Skills kama zako. Hii inaathiri hadi unapotuma maombi. Kwenye rank unakuwa wamwisho. Sasa hadi client aje kusoma proposal yako amekuwa mvumilivu sana kupitia proposal zote. Most clients never go through all the proposals. This is the reason you never get to hear from them. Unaandika proposal lakini hata kujulishwa umekosea kazi hujulishi ☹

Upwork wanafanya hivi kwasababu wanafahamu beginners wengi hawapo serious na pia ni ngumu kufahamu kama kweli wanaujuzi wanaosema wanao.

2 • UpWork is very competitive

Mazee, Upwork ni noma sana. Freelancers wengi wakubwa wanafahamu UpWork kuna pesa kwahiyo ukiwa una apply gig fahamu una apply na experienced freelancers wengi ulio lingana nao ujuzi au wamekupita kwa mbali.

Inabidi ujipange.

Pia uwe mjanja kuapply kazi zile tu ulizo na competitive advantage.

3 • Skills ulizonazo Freelancers wengi wanazo lakini pia hufahamu jinsi yaku “standout” katika kundi.

Hii inaendana kiaina na point ya competition.

Kuitazama kwa namna nyingine Hii point ni hivi. Inawezekana Skills ulizonazo zina demand (mfano virtual assistant ni skill yenye demand all the time na kila mtu anaweza kuwa VA) Sasa hapa kinachotokea ni kwamba beginner hawafahamu mbinu yakujitofautisha ili client akiwa anatafuta Virtual Assistant awaache wengine akuchague wewe. Umeshajiuliza kwanini experience freelancers inakuwa rahisi kupata gigs? We understand something beginners don’t. Maneno gani yakutumia wakati wakuandika proposal etc.

4 • You are too lazy, even to respond to client's messages.

Unajua nini?

Baadhi ya freelancers wanakosa kazi kwa sababu rahisi tu wao ni wachelewaji wa kila kitu.

Inabidi uwe haraka kama train ya umeme.

Kwa mfani jioni hii client amejibu proposal niliyotuma sasa akanitaka nijubu maswali machache kuhusu kazi husika na niseme tu kwangu haichuki muda.




Hii kazi pengine na mimi nitampatia mtu mwingine anisaidie. Ni kazi nzuri and the money is not bad.

This is $14 per Hour, 4 - 8 hours a day for 5 days.

Unaona kazi ina demand time kimtindo. Na mimi binafsi napenda creative work itakayonipatia muda mwingi wakuwa free. Lakini kwa sababu ya [emoji383] hizi kazi tuna-apply kwasababu the money is good Pia ni long time project.

Alright, naomba niishie hapa. Maneno yameisha 🤩

Cheers 🥂
 

Habari mkuu naomba ushauri wako, mimi ni mgeni kwenye hii kazi ya freelancer. Jana kuna client mmoja aliniomba nieleze jinsigani nitaifanya kazi yake, nilimjibu fasta halafu akaniambia naomba tuwasiliane kwa email. nikamtumia email.

Akanipa terms na conditions za kazi yake lakini kuna kitu kikanishtua yaani ananiambia kabla hajanipa kazi hiyo natakiwa nimtumie hela $30 ili aweze kuniamini halafu nitarudishiwa.

Nikahisi huyu ni tapeli, kwanini anasema nitoe $30 ambayo nitarudishiwa baadaye baada ya kumaliza kazi. Nikamjibu nipo tayari kufanya kazi hadi mwisho halafu akate hiyo amount anayotaka itakayobaki anilipe lakini sina hela ya kumpa kama sehemu ya uaminifu wa kazi hiyo.

Je kuna baadhi ya clients huu ndio utaratibu wao wa kuomba hela kabla hujafanya naye kazi??

Naomba kueleweshwa zaidi katika hili mkuu.
 

He wants to scam you.

Usitoe pesa.

Bila shaka ulikutana naye Freelancer.com

Ngoja nikuambie kutu. Huyo jamaa anafahamu wewe ni beginner kwahiyo anajaribu kutake advantage. Huu mchezo upo sana freelancer.com ndiyo maana nasisitiza sana kufanya kazi kwenye elite platform kama UpWork.

Mkuu, nakushauri report hiyo issue achukuliwe hatua.

Cheers 🥂
 
Ni kweli, huyu nilikutana naye freelancer.com. Asante sana kwa angalizo hili ubarikiwe, ngoja ni sign up kwenye upwork
 
Naomba namba mkuu nahitaji unielekeze maana mie ndo nataka kuaanza
 
Daniel ntakutafuta, nna email na namba yako ya simu pia. Sema naendekeza kazi zangu binafsi sana.
 
ok
 
Nyuzi za hivi hukuti wabongo ila zile za kudownload pesa bila kufanya kazi ndo wamejaa huko. Haki ya nani tunashida mahali.
 
Nyuzi za hivi hukuti wabongo ila zile za kudownload pesa bila kufanya kazi ndo wamejaa huko.
Haki ya nani tunashida mahali.
Nadhani badala ya kuwalaumu na kuwasema vijana wa kibongo. Ni vizuri mtoa mada angeeleza in details ili ata mtu wa kawaida ambae ni first time kusikia kuhusu hii opportunity aelewe.

Maelezo yake mazuri ila yanamfaa mtu mwene prior knowledge. Tunashindwa ata kushare hii thread na vijana majobless kwa sababu watatoka kapa.
 
Utakuwa hufuatilii thread za mtoa mada la sivyo wewe ni mgeni jf.Hajaacha hata nukta kwenye huu uwanja.
 
Kifo cha upwork kiko njiani UBER mwaka jana mwishoni waliajiri watu 1,000 engineers, UX Designers, business developers, product managers wajifungie ili waje na UBER WORKS...

Nathan wote tunajua UBER walivyo serious na mambo yao Dara Khodorkovsky yule jamaa he is very genius
 
View attachment 1520402
GLOBAL CITIZEN Hiki ndio kitu hawa waxenge wamenitumia! Maana nitume tena profile wanijubu baada ya miezi 6 ama? Hawawezi kuwa serious.

Mkuu kama nilivyosema,

Upwork wanakubali tu freelancers watakaonyesha bila shaka wao ni weledi katika skills wanazosema wanazo. Sasa hapa inabidi ukubali ukweli application yako ilikuwa chini ya kiwango mkuu. Inabidi ufahamu ni kwa namna gani unaweza kuboresha hii.

Ukitaka kukubaliwa kwa urahisi ingia freelancer.com.
 
Ni kwamba kwenye hizo kazi za Upworks inabidi uwe na
1.Ujuzi/Fani husika kwa kitu kinachohitajika mfano mtu wa Tafsiri awe na vyeti vya Course za Lugha au kazi za tafsiri alizowahi fanya
2.Uzoefu wa Kazi za Upworks nje ya hapo mambo ni magumu
 
Mkuu sasa unatusaidiaje kuhusu hili la kuongeza ujuzi kuna madarasa online mtu ajibrush kidogo then ndo arudi kuapply au ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…