Yaonekana Kambona alikuwa bright zaidi kumzidi hata Mwalimu - Aliona mbali mno kiasi akaona ni kheri kuondoka Tanganyika kuepusha shari maana kuishi na mtu mwenye msimamo na asiyetaka kubadilika ni kazi nzito sana.
Yaonekana pia Kambona alikuwa modernised person huku Mwalimu akiwa anataka kuendelea na ujamaa wa kale wa kina Karl Max - kwamba you all move as a group then you share what you get equally - kitu ambacho Kambona aliona hakiwezekani kufikia malengo ya maendeleo kama taifa kwa uharaka.
Mbaya zaidi Historia ya Tanganyika katika harakati za kudai uhuru wetu imemtema Kambona kabisa, anaonekana kama msaliti wa mkubwa wa Taifa hadi leo hii, kitu ambacho si sahihi.