Urahisi wa upatikanaji wa kondomu

Urahisi wa upatikanaji wa kondomu

M-bongotz

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Posts
1,736
Reaction score
408
Jana katika pitapita nikakutana na hii

Hii ni mashine ya kununulia condom...kinachofanyika unaweka hela kama Tsh 100 hivi kwa juu kuna kitobo cha kuingizia pesa unazungusha kitufe fulani halafu condom inatoka kwa chini unaendelea na mambo yako...

Hayo ni maelekezo namna ya kununua

Mzigo unatokea kwa hapo....

Sasa hivi tushindwe sie tu kutumia hii kitu maana mzigo tunawekewa hadi msalani.

Kondom ni uasherati katika sura nyingine - acheni zinaa jamani. Kama huna mwenzi subiri, kama unaye ni yeye pekee mpaka umauti utakapowakuta
 
Kondom sio uasherati, ila watu ndio waasherati. Condom ni kinga dhidi ya magonjwa na mimba zisizotarajiwa. Unaweza kutumia condom na mkeo au mpenzi wako mmoja mnaeaminiana.
 
sasa wangeweka rafu raidaaz!...hizo za mia mia wakauze namtumbo huko
 
Kondom sio uasherati, ila watu ndio waasherati. Condom ni kinga dhidi ya magonjwa na mimba zisizotarajiwa. Unaweza kutumia condom na mkeo au mpenzi wako mmoja mnaeaminiana.

Nono the Great:

Mimba zisizotarajiwa ni matokeo ya uasherati
Magonjwa "ya zinaa" ni matokeo ya uasherati
Kutumia kondomu kufanya tendo la ndoa na mke/mume wako ni uasherati
Kufanya tendo la ndoa na mwanamke/mume asiye mke/mume wako ni uzinzi

Bwana akupe nguvu ya kuiepuka kondomu
 
Kondom ni uasherati katika sura nyingine - acheni zinaa jamani. Kama huna mwenzi subiri, kama unaye ni yeye pekee mpaka umauti utakapowakuta

Ingekua ni rahisi kiivyo kama unavyosema basi toka Dini ianze kuhubiriwa watu wangekuwa wote watakatifu! Kondom inasaidia kwa wale ambao wameshindwa hizo njia nyingine! Hapa inabidi tutenganishe Iman na reality!!
 
Nono the Great:

Mimba zisizotarajiwa ni matokeo ya uasherati
Magonjwa "ya zinaa" ni matokeo ya uasherati
Kutumia kondomu kufanya tendo la ndoa na mke/mume wako ni uasherati
Kufanya tendo la ndoa na mwanamke/mume asiye mke/mume wako ni uzinzi

Bwana akupe nguvu ya kuiepuka kondomu

Nasubiri apology kabla sijakufikisha kwa pilato! Mimi na my wife wangu tunatumia kondomu kila siku. Ndoa yetu alifungisha Askofu na miongoni mwa mashuhuda walikuwa ni watakatifu kibao. Pia hatujawahi kuviruka viapo vyetu. Hebu changamka usafishe hali ya hewa, vinginevyo nitakung'ang'ania mpaka kieleweke!
 
Nono the Great:

Mimba zisizotarajiwa ni matokeo ya uasherati
Magonjwa "ya zinaa" ni matokeo ya uasherati
Kutumia kondomu kufanya tendo la ndoa na mke/mume wako ni uasherati
Kufanya tendo la ndoa na mwanamke/mume asiye mke/mume wako ni uzinzi

Bwana akupe nguvu ya kuiepuka kondomu

??????????
icon13.gif
 
Tutumie kondomu jamani, achane mizaha! Kila mmoja wetu ni shahidi amezika wangapi kutokana na ugonjwa huu.
 
weweeeeeeeeeeeeeeee uhuruuuuuuuu wakuongeaaaaaaaaa
tumia kinga
 
Nono the Great:

Mimba zisizotarajiwa ni matokeo ya uasherati
Magonjwa "ya zinaa" ni matokeo ya uasherati
Kutumia kondomu kufanya tendo la ndoa na mke/mume wako ni uasherati
Kufanya tendo la ndoa na mwanamke/mume asiye mke/mume wako ni uzinzi

Bwana akupe nguvu ya kuiepuka kondomu
Big up kwa mbogo aliye lamba hii tenda (ni mshkaji flani, mambo ndo hayo!)

Pili, huyo Enock ulimpata kimakosa!! huruhusiwi kumleta kiumbe duniani kama ww mwenyewe you cant think using your own brain!!
 
Nono the Great:

Mimba zisizotarajiwa ni matokeo ya uasherati
Magonjwa "ya zinaa" ni matokeo ya uasherati
Kutumia kondomu kufanya tendo la ndoa na mke/mume wako ni uasherati
Kufanya tendo la ndoa na mwanamke/mume asiye mke/mume wako ni uzinzi

Bwana akupe nguvu ya kuiepuka kondomu

Sio ajabu kuendelea kuamini kuwa dunia ina nguzo zilizoishikilia. Tatizo ni kuwa mkishakuwa na imani fulani basi mnatupilia mbali akili na uelewa hata wa mambo mepesi. Ndio maana hadi kesho vifo vingi vya watoto na kina mama afrika tunaendelea kuamini kuwa Bwana aliwapenda zaidi. This is shame! Tunapaswa kuyakabili mazingira yetu na sio kumsingizi Mungu hata yale yatupasayo.
Uzaza uko palepale wakati wowote, njia za kuuzuia ni pamoja na condom. Labda inaweza kuwa tafsiri zaidi kwako wewe kuwa unaweza kufanya uasherati na mkeo ila sio kwa wengine.

"Haya mafundisho mengine, noma sana"
 
Back
Top Bottom