Uraia pacha/dual nationality, tunakwama wapi kama taifa?

Idimi

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2007
Posts
15,328
Reaction score
11,192
Kwa miaka kadhaa sasa, kumekuwa na mijadala kadhaa Tanzania kuhusu uwezekano wa Watanzania kuwa na uraia pacha.

Serikali imekuwa na woga wa kutoa uraia pacha kwa hoja kwamba itaongeza hofu ya usalama (security issues), kwamba mtu anafaya kosa Tanzania kwa uraia wa Tanzania then anakimbilia nje kwenye uraia wa pili.

Hoja hii mie naipinga sana kwa sababu kuna utaratibu wa kimataifa wa kukabiliana na uhalifu (cross border crime controls) kuna ushirikiano wa kipolisi kimataifa (Interpol).

Tunapoteza vingi sana kwa kutokua na uraia pacha, hasa kimapato. Tulijadili sana hili suala kwenye katiba pendekezwa miaka ile, ila likapingwa na wajumbe wa bunge la katiba.

Ningeomba serikali ilione hili kwa macho marefu, iruhusu uraia pacha.
 
..Uraia pacha unatisha.

..wapewe Permanent Residency ambapo watakuwa na haki za kawaida, lakini hawaruhusiwi kupiga kura, na kuajiriwa serikalini.
 
Mkuu mbona Kenya, Rwanda, Uganda na nchi nyingi za Africa zimehalalisha hii kitu bila matatizo yoyote, sisi TUNAKWAMA WAPI!?

..historia na safari yao ktk masuala hayo ni tofauti na ya Watanzania.

..mitizamo yetu kuhusu uraia ni tofauti na mitizamo ya Wanyarwanda, Wakenya, au Waganda.

..naamini status ukaazi wa kudumu ni compromise ambayo itakubaliwa na Watanzania na wenye dhamana ya kufanya maamuzi kuhusu suala hilim
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Tumepoteza nini? Uraia pacha una manufaa kama nchi yako tajiri au kama una watu wengi nje ya nchi ambao wana kipato kikubwa sasa wabongo wengi ambao wako nje ni vibaka na wabeba boksi tu watatuletea nini cha faida?
 
Lakini all in all sisi ni sehemu ya jamii pana ya kimataifa, we are not an island. Kuna watu wanashindwa kuja kuwekeza Tanzania kwa sababu waliokana uraia wa Tanzania ili kusaka maisha abroad, lakini bado nafsi zao zinaikumbuka nchi yao. Sasa watu kama hawa tunapowanyima haki ya kumiliki ardhi kwa kuwa wana uraia wa nje (wa kugawiwa) sio haki sana
 
..ndio maana nimependekeza status ya ukaazi wa kudumu.

..mhusika ana haki zote isipokuwa kupiga au kupigiwa kura, na kuajiriwa serikalini.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Nadhani gavo wanafikiria diaspora wote ni chedema🥵🥵
 
Hapana Mkuu huna haki zote kuna baadhi ya nchi huwezi kupata kazi Serikalini kama si RAIA. Na sheria katika nchi hizi zinaweza kubadilika wakati wowote ule.
..ndio maana nimependekeza status ya ukaazi wa kudumu.

..mhusika ana haki zote isipokuwa kupiga au kupigiwa kura, na kuajiriwa serikalini.
 
Ccm Katu haiwezi ruhusu uraia pacha hofu ya kuondoka madarakani,sasa diaspora awaathiriki na moshi wa mwenge
 
Tumepoteza nini? Uraia pacha una manufaa kama nchi yako tajiri au kama una watu wengi nje ya nchi ambao wana kipato kikubwa sasa wabongo wengi ambao wako nje ni vibaka na wabeba boksi tu watatuletea nini cha faida?
Lugha yako nyepesi sana.
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Mkuu mbona Kenya, Rwanda, Uganda na nchi nyingi za Africa zimehalalisha hii kitu bila matatizo yoyote, sisi TUNAKWAMA WAPI!?

Akili za wenye mamlaka bado zipo 19 century sasa ukiuliza swala hili utapewa majibu hayohayo
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hapana Mkuu huna haki zote kuna baadhi ya nchi huwezi kupata kazi Serikalini kama si RAIA. Na sheria katika nchi hizi zinaweza kubadilika wakati wowote ule.

..diaspora wapewe haki zote isipokuwa kupiga au kupigiwa kura, na kuajiriwa ktk serikali kuu na taasisi zake.

..kwa maana nyingine wawe na status maalum lakini sio uraia kamili, na wanapokiuka masharti wanyang'anywe status hiyo.

..naamini hiyo ni WIN-WIN kwa wanaotaka uraia pacha na wanaopinga uraia pacha. Kila upande unatoka ukiwa umepata kitu fulani.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kwa miaka kadhaa sasa, kumekuwa na mijadala kadhaa Tanzania kuhusu uwezekano wa Watanzania kuwa na uraia pacha.

Serikali imekuwa na woga wa kutoa uraia pacha kwa hoja kwamba itaongeza hofu ya usalama (security issues), kwamba mtu anafaya kosa Tanzania kwa uraia wa Tanzania then anakimbilia nje kwenye uraia wa pili.

Hoja hii mie naipinga sana kwa sababu kuna utaratibu wa kimataifa wa kukabiliana na uhalifu (cross border crime controls) kuna ushirikiano wa kipolisi kimataifa (Interpol).

Tunapoteza vingi sana kwa kutokua na uraia pacha, hasa kimapato. Tulijadili sana hili suala kwenye katiba pendekezwa miaka ile, ila likapingwa na wajumbe wa bunge la katiba.

Ningeomba serikali ilione hili kwa macho marefu, iruhusu uraia pacha.

Tuwe na subra kidogo Mama na waziri wanatengeneza sera ya diaspora ni mwanzo mzuri. Tusubiri kuiona Mimi kwa mawazo yangu cha maana ni haki muhimu kama mzawa diaspora wana mabibi na mabubu wamezikwa huko huwezi kuwalinganisha na wazungu baki!
 
Mkuu Serikali inawahitaji wataalamu mbali mbali katika sekta zote. Hivyo mimi sikubaliani nawe Diaspora wawekewe vizingiti vyovyoye. Pale TPDC kuna Mataragio huyu jamaa alirudi baada ya kushawishiwa na Kikwete. Na ni mtaalamu hasa katika sekta hiyo. Hivyo kwangu mimi sioni sababu yoyote ile ya Tanzania kuendelea kupinga uDC.
..diaspora wapewe haki zote isipokuwa kupiga au kupigiwa kura, na kuajiriwa ktk serikali kuu na taasisi zake.

..kwa maana nyingine wawe na status maalum lakini sio uraia kamili, na wanapokiuka masharti wanyang'anywe status hiyo.

..naamini hiyo ni WIN-WIN kwa wanaotaka uraia pacha na wanaopinga uraia pacha. Kila upande unatoka ukiwa umepata kitu fulani.
 
I heard this song before when Kikwete was still in office and Membe tried his level best to make sure that DC is approved in Tanzania but Kikwete’s support was lacking as he was scared of maccm.
Tuwe na subra kidogo Mama na waziri wanatengeneza sera ya diaspora ni mwanzo mzuri. Tusubiri kuiona Mimi kwa mawazo yangu cha maana ni haki muhimu kama mzawa diaspora wana mabibi na mabubu wamezikwa huko huwezi kuwalinganisha na wazungu baki!
 
Mkuu Serikali inawahitaji wataalamu mbali mbali katika sekta zote. Hivyo mimi sikubaliani nawe Diaspora wawekewe vizingiti vyovyoye. Pale TPDC kuna Mataragio huyu jamaa alirudi baada ya kushawishiwa na Kikwete. Na ni mtaalamu hasa katika sekta hiyo. Hivyo kwangu mimi sioni sababu yoyote ile ya Tanzania kuendelea kupinga uDC.

..nayaheshimu mawazo yako ya kuunga mkono uraia pacha.

..pia nayaheshimu mawazo ya wasiotaka uraia pacha.

..sababu hizo ndio zimenifanya niunge mkono status ambayo ni WIN-WIN kwa pande hizo mbili.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mkuu Serikali inawahitaji wataalamu mbali mbali katika sekta zote. Hivyo mimi sikubaliani nawe Diaspora wawekewe vizingiti vyovyoye. Pale TPDC kuna Mataragio huyu jamaa alirudi baada ya kushawishiwa na Kikwete. Na ni mtaalamu hasa katika sekta hiyo. Hivyo kwangu mimi sioni sababu yoyote ile ya Tanzania kuendelea kupinga uDC.
Uko sahihi mkuu, JK kawatumia sana diaspora. Kuna yule dada alikuwa DG wa Tanzania Investment Centre (TIC), alitumbuliwa na JPM. Yule aliletwa pale na JK akitokea Afrika Kusini ili aje atengeneze mazingira ya uwekezaji Tanzania. The same to Profesa Muhongo.
 
Back
Top Bottom