Urais 2015 tusimlaumu Zitto: Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa?

what you dont know is that the world has shifted beneth you!. Dr Slaa alijaribu ngwe yake.. hakubahatika. what we need is one young and energetic. Kitu tutakachokosea ni kumchagua Dr Slaa tena 2015 kupeperusha bendera yetu. We know, perhaps not much known to many of you that Slaa hakubaliki tena. tusije jikuta tunafanya uamuzi kama wa CUF....ambao wamekuwa wamemweka Prof. kila mara bila kujua kuwa muda wake umepita......their efforts ended in vain. Someni presidential histories za Marekani....mtalielewa hili kuwa Slaa hawezi tena kutupeleka ikulu. Lets think some one else, Zitto among the hopefuls. Tusifanye ushabiki ktk hili.... lest tutaendelea na magamba. wake up guys!
 

Wee bwana Pasco acha hizo. Unataka kuudanganya umma wa JF hapa kuwa eti ulifanya interview na Dr Slaa na akakueleza kuwa anataka kugombea urais. Hicho ndicho unachokisema ili ku-justify support yako kwa power-monger wako Zitto.

Sikiza bwana. Uraisi ni utumishi na utumishi watu hawaombi, bali huombwa - just like ilivyotokea kwa Dr Slaa 2010!
Raisi mtarajiwa anatakiwa awe modest and humble - attributes which Zitto doesnt possess!
 
Mwambie Zitto aoe kwanza ndo aje kutangaza nia, Hatutaruhusu Rais kapera.

Makes sense. Zitto is good. Nadhani anahitaji kuwa na ndoa kabla ya kugombea uraisi. Ofcourse ndoa sio mandatory lakin inaonyesha kuwa committed man or woman. Kama upo committed kwa familia yako definetly utakua committed kwa nchi na wanacnhi yako. Kwa hiyo, Zitto asawazishe swala la ndoa kwanz. Hili ni wazo langu naweza kutokua sahihi.
 


Nipo pamoja nawe tatizo sio Zitto kugombea uraisi ila ni tactic anazotumia.
Nami nakubali tactic anazotumia sio nzuri wala sio sahihi.
Ninachojua ni kuwa rais lazima aandaliwe au ajiandae maana hata huo ubunge tu watu washaanza kasikasi majimboni. Mnataka akurupuke tu 2015. Ni wakati sasa wa kuwapima kwa kila angle hatutaki kuwasikia wakitoa ahadi wakati wa kampeni kwangu Mimi naona itakuwa too late.
Hebu jamani tuwe na muda basi wa kuwapima wagombea wote kwa vyama vyote. Sio dakika za majeruhi mwisho tunaokota koroma.
 
Pasco, my take ya nini tena hapo wakati kila kitu umeongea wewe? Najua Dr Slaa hana tena mpango wa kuwania urais awamu ijayo, na ndio maana ukaandika uliyoandika. Kiufupi yawezekana kabisa kuwa cdm wanapima upepo kupitia Zitto. Siasa wanaijua wanasiasa. Sie tunazijua nadharia.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kifupi Zitto hana uwezo wa kuwa Rais ila anatumiwa kutokana na tamaa yake ya cheo na utajiri. Chadema muwe makini na mtu huyu (Zitto) anatumiwa na CCM kutaka kuivuruga Chadema, mumpuuze ila muwe makini naye.
 


Mkuu upo sahihi kumsupport Zitto.
Pia maudhui ya thread yako yanaonyesha kuwa Dr. Slaa hatagombea Urais 2015.
Vinginevyo ulitakiwa tu umuunge mkono Zitto bila kumtaja Dr. Slaa.

Pili, Zitto halaumiwi na mtu yeyote, kinachomtafuna ni undumila kuwili pamoja na kutumia migongo ya watu wengine kupresent hoja zake tata.

Kama anaamini kuwa anafaa kuwa raisi kwa nini asisimame kwa miguu yake na aeleweke hivyo ili tuweze kumsupport???
Badala ya kutengeneza hoja tata kila mara kupitia migongo ya watu wengine na kuja kukanusha baadaye???
 
Sidhani kama wazee wa chama watafurahishwa na nia ya Zitto

Mkuu usiwawakee watu maneno mdomoni. kwa nini wasifurahishwe??? zitto ni mwanachama na kiongozi wa CDM hivyo ana haki zote kikatiba. Kinachosumbua mbinu zake za kubomoa chama katika kuutafuta huo uraisi.
 


PASCO,

Concern yetu ni kwamba kwa nini Zito autake Urais kwa udi na Uvumba?????

Just imagine incidence mbili nazokumbuk.

1. Wakati wa Uchaguzi wa 2015, Zito aliwahi kusema safari ijayo hagombei ubunge bali Urais wa JMT, ile hali anajua ishu iliyoko mbeleni ni kuhakikisha mgombea aliyekuwepo anashinda.

2. Jambo lingine ni wakati wa uchaguzi wa Arumeru, Zito anakuja na hoja ya kuutaka Urais embu fikiria haya yote yanapangwa na Zito au CCM....


NB: ZITO anauhusiano wa karibu sana na watu wa TISS, kupitia jack anayefanya CCM iendelee madarakana kwa miaka 50 mingine..... Na kwa sasa atakayevuruga CDM au upinzani ni ZITO na kama ikitokea hata ndani ya chama akasema Urais anautaka kwa lengo la kuivuruga CDM badhani anajua ni jinsi gani alivyo mwepesi kama shibuda kama uatakumbuka mkutano wa jangwani wa CDM last time...

Na zito anatakiwa kufahamu Upinzani sasa umejaa vijana wazalendo wenye maslahi na hii nchi na si hao wanaofikiria matumbo yao akicheza karata vibaya mwisho wake kwenye siasa ni 2015.
 
Pasco

tatizo siyo Zitto kuwa na nia ya kugombea au ndoto ya urais, tatizo ni mbinu anazozitumia siyo sahihi na zina udhi. Mkapa wakati wake siyo hakupenda lakini ali cheza karata yake vizuri. lakini mwone Zito kama vile ka tumwa na mganga wa kienyeji kuwa lazima uupate urahisi.
Hoja ya kuwa Dr Slaa labda hata gombea ni hoja dhaifu kwa vile ndani ya CDM wenye uwezo ni wengi kumzidi Zito.

 
Zitto = Shibuda.

Mashaka makubwa ni kwa mtu anaeanza kuhubiri nia ya kugombea uraisi leo,na mbaya zaidi imekuwa ni basic agenda kila anapopata jukwaa la kusemea,najiuliza hivi kuna nini behind the scene?kwani amesahau kwamba tangu anajengwa kisiasa adui mkuu aliekuwa anampigania mazingira ya kumtoa bado hayajakamilika?iweje aanze kutuhubiria uraisi leo badala ya kutuhubiri namna nzuri aliyoipata ya kumtoa adui wa watanzania CCM? NA MAFISADI WAKE?AU kutangaza kugombea uraisi tu tayari CCM wataichia nchi?je ni kweli kuwa Zitto akitangaza nia ya kugombea uraisi tayari ni ushindi?
Nilidhani leo angeibuka na mbinu mpya ya kuhakikisha chama chake kina pata sapoti kubwa kutoka kwa wananchi na akapata dawa ya wachakajuaji wa kura,kisha watu wakampima kwa strategy alizokuja nazo kisha tumpendekeze kuwa mgombea uraisi na kisha ashinde kwa kupewa sapoti na watu aliokwisha waandaa.
Na kwangu mimi napata tabu kuona anaanza kupigia kelele za uraisi leo hivi kwa tamaa hizo anadhani ikulu ni pepesi?
No CDM hatuna utaratibu wa kuzungumzia uraisi na kutengeneza mitandao.PASCO najua unachokijadili hapa,si kingine nilishawahi kukuambia unawania u-Rweyemamu wa 2015.
Ila angalizo:CDM ni chama cha watu,wataamua nani apeperushe bendera.
 
Mtu anaekimbilia ikulu tunapaswa kumwangalia kwa jicho la tatu
 

Kakaa wanamuogopa sana na hao wote wanaompinga sio wengi humu JF hawazidi kumi ila kila mmoja ana ID zaidi ya kumi ndio ukirudi kitaa jamaa wanamkubali sana ingawa kule kaskazini sio sana ila sehemu iliyobaki out of Kaskazin jamaa wanamkubali vibaya
 

suala si tuhuma kibao suala ni tuhuma za kweli?
 
Pasco, mimi nakoma na vijana wa Chadema wakimkomalia mtu hadi utamwonea Huruma..Dr. Slaa amekuwa kikataa kugombea toka mwaka 2010 muda wote alikuwa akisema hatagombea, CCM wakauvaa wakidhani Mbowe wakarusha madongo sana tu mara walotegemea hayakuwa..Wakati wa uchaguzi Dr.Slaa yeye mwenyewe alisema ni rais wa awamu moja tu, na baada ya uchaguzi kasema hayo alosema ukayasikia wewe tu, lakini yote haya nakuhakikishia hakuna ukweli wowote. Anaweza fanya lolote kinyume maana sii kiapo bali tactics za kisiasa

Alisema hatagombea, akagombea angekuwa Zitto nchi nzima ingekuwa kiza kwa laana ambazo angezipata..jamani mweee.. Huu ni wakati muafaka wa wanaChadema kujitambua wao wamesimama wapi na kuna hatari gani za kisiasa ambazo nina hakika watakisambaratisha chama wenyewe kama ilivyokuwa kwa NCCR, CUF na sasa Chadema bila mkono wa CCM direct.. CCM anajua sana kuvimaliza vyama na Chadema iko hatarini kifupi naanza kuhofia kama itafika mwaka 2015 wakiwa pamoja..
 

udi na uvumba kivipi? Yaani kusema anautaka urais ivuruge uchaguzi mdogo wa ubunge!hivi tunatumia bongo au majivu!
 
Msipoteze muda. Anayejua msimamo wa dr slaa ni sisi warz tunaomfahamu kwa maneno na matendo yake. Hata km hataki kugom bea tutamlazimisha awe rais wetu. Na ndio maana dr. Yuko kimya kwasababu hawezi kupoteza muda kumjibu zitto mnafiki badala ya kukazana kukijenga chama.
 
Kakaa wanamuogopa sana na hao wote wanaompinga sio wengi humu JF hawazidi kumi ila kila mmoja ana ID zaidi ya kumi ndio ukirudi kitaa jamaa wanamkubali sana ingawa kule kaskazini sio sana ila sehemu iliyobaki out of Kaskazin jamaa wanamkubali vibaya

ndo maana akisema tu anagombea urais.mara anaharibu uchaguzi mdogo mara hivi mara vile hoja za hovyo hazina hata mashiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…