Urais 2015 tusimlaumu Zitto: Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa?

Urais 2015 tusimlaumu Zitto: Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa?

mmmh! Pasco umeweka kibomu tena, ila nnachojua Nuru na Giza havichangamani, penye Nuru giza hutoweka, endeleeni kumfagilia zitto, CDM wapo makini.
Mkuu wangu ogopa sana nguvu ya kiza umeshaona jua likipatwa vizuri hasa jinsi unavyojisikia.. Zitto ana makosa yake na hatopendwa hata akila na kulala makao makuu. Ila nina hakika Dr.Slaa leo akisema haya haya watu wanangia barabarani kwa maandamano na kilio kwa CCM wote wakihaha. CCM wanajaribu sana kutugombanisha kama walivyoweza kuivuruga NCCR, CUF kwa nguvu ya kiza baada ya kupata the weakest point..na hakika mtu ukiwa kizani huoni utapapasa tu kutafuta njia ya kutokea..Amini maneno yangu tunakwenda ktk nguvu ya kiza..
 
mkuu Mkandara
ni maajabu kweli, eti watu wa upande wa pili wanakisaidia chama kwa kumbeba zitto. hii sijapata kuisikia popote, hivi zitto hashtuki ni kwanini maadui wa CDM wana msupport??
 
Last edited by a moderator:
mkuu Mkandara
ni maajabu kweli, eti watu wa upande wa pili wanakisaidia chama kwa kumbeba zitto. hii sijapata kuisikia popote, hivi zitto hashtuki ni kwanini maadui wa CDM wana msupport??
Atashtuka vipi ikiwa nyie wenyewe pia mna mashaka naye..Unajua ukisingiziwa sana unaiba inafika mahala unaanza kujiuliza kwa nini nisiwe mwizi kweli?. Walichokifanya CCM ni kuanzisha upinzani baina ya Zitto na Mbowe wakafanikiwa wakaingia hatua ya pili kama walivyoifanya NCCR wakati wa Mrema kumkosanisha na chama na ikakubali. CUF pia imejimaliza yenyewe wakimtumia Maalim Seif watu hawakujua until toolate. CCM wanaweza penyeza kwa Mbowe, Dr. Slaa na mtu mwingine yeyote wakikuhitaji, watazisoma nyendo zako kisha wanakupa kitu na sababu U can't ignore, kisha anakujaza ujinga..

Hapo lazima utabadilika na hii haikutokea kwa Zitto tu wamo watu CDM wanalala na vipanga wa CCM na hawajui wanakopelekwa. All I wonna from my fellas CDM leadership, dude kufikiria mlitoka wapi? hivi relation zenu zilikuwa vipi kabla hamjalishwa sumu hizi za uhasama. UTU na mapenzi yameishia wapi. je ni ushindi mdogo ulowapa kiburi hiki, taratibu mtakuja gundua nguvu ya giza..
 
Wanabodi,

Mara baada ya mazishi ya Mhe. Regia, (RIP), on route back to Dar, nilibahatika kukutana mahali na Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wibroad Slaa akiwa na wife wake, Fina, tuliendesha mazungumzo mafupi, informal, na miongoni mwa maswali niyomuuliza, ni hili la iwapo atagombea tena nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi wa 2015!.

Nayakumbuka vizuri sana majibu ya Dr. Slaa kuhusu swali hilo!. Kwa vile mazungumzo yale hayakuwa rasmi, kuna uwezekano mkubwa, Dr. Slaa alizungumza "off the record", sio busara kuyaleta mazungumzo ya "off the record" kwenye public na kuyaweka "on the record" bila "idhini" ya msemaji.

Kwa vile msimamo wa "Dr. Slaa kuhusu kugombea urais 2015, mimi naujua!, nawashauri, wale wote wanaumlaumu au kumshutumu Zitto, kuonyesha nia ya kuwania urais wa 2015 kwa tiketi ya Chadema, kwa kujenga mazingira "impliedly" not "expressly"!, wasimlaumu bali wamsupport!.

Hivi kuna ubaya gani, kuonyesha nia ya kuwania the highest office?. Wote wanaoutaka urais, huitwa "presidential hopeful", hivi kuna ubayo wowote to aim high?!.

My Take.
Kwa vile mchakato wa kuwania urais wa 2015 bado haujaanza rasmi kwa vyama vyovyote, lakini tunashuhudia "presidential hopefuls" wa vyama mbalimbali wakijenga mazingira kupitia mikakati mbalimbali, nawaombeni wapenda demokrasia ya kweli, tuwe open minded kuhusu watu hawa, tusianze kuwanyooshea vidole vya kuwashutumu bali tunapaswa kuwaunga mkono kwa nguvu zote ili at the end of the day, tumpate mgombea bora kabisa!,

Mfano hakuna ubishi kuhusu uwezo wa Zitto katika masuala ya organization na mass mobilization!, hakuna ubishi kuhusu nguvu ya Zitto katika ushawishi na kujenga hoja na kusimamia utekelezaji. Kama ni kweli Zitto ni "presidential hopeful" ndani ya Chadema na sasa anajenga mtandao wa kuandaa mazingira hayo, this is very healthy kwa Chadema, kwa sababu by the time muda wa mchakato rasmi unawadia, na Chadema ikampitisha Dr. Slaa kupeperusha tena bendera ya Chadema, huo mtandao wa Zitto ndio utakuwa an added advantage kwa ushindi wa kishindo wa Chadema, na Zitto ndio atafaa zaidi kwa post ya Waziri Mkuu, kama alivyofanya Obama na Hillary Clinton!.

Kufuatia mimi kuufahamu msimamo wa Dr. Slaa, lets support Zitto or anybody else!,

Mhe. Zitto, just follow your dreams, "Sky is the limit!".

I wish Zitto all the best!.

Wasalaam.

Pasco. (wa jf).

NB. Pasco wa jf, sio mwanachama, mshabiki au mkereketwa wa chama chochoite cha siasa, bali ni muumini wa demokrasia ya kweli.

Ubaya hakuna tatizo ni zitto na ccm wanataka kutumia mbinu chafu kubadili umri ktk katiba wa kugombea urais ushuke ili wapate kumwaribia Dr.
 
Wanabodi,

............................NB. Pasco wa jf, sio mwanachama, mshabiki au mkereketwa wa chama chochoite cha siasa, bali ni muumini wa demokrasia ya kweli.
aa waapi!!!
usitudanganye.
 
Pasco,
Kwa mtazamo wangu hakuna ubaya mtu kutangaza nia yake ya kuongoza.
Hiyo ni haki yake kikatiba na ni haki ya msingi. Kwa upande wa kisiasa hiyo pia ni haki yake ndani ya chama chake kwa kufuata taratibu za chama chake n.k.

Tatizo ninalo liona ni lile la kujificha na kufanya mambo tena ya hatari sana halafu kujiosha ili kuonekana mzuri.
Kuna nyuzi nyingi kuhusu Zitto na yaliyotokea Kigoma.
Hapa nitaongozwa na ukweli. Zitto kama kiongozi ana uwezo wa kujenga hoja na ku-mobilize jamii.

Mara zote amekuwa ni sehemu ya utata kuhusu mitazamo yake kisiasa. Tumewahi kumueleza lakini ana tatizo la kutosikiliza akiamini kuwa ana uwezo wa kila jambo. Kauli zake hazilingani na matendo yake.

Nikiacha yale ya nyuma( nikitakiwa niyaweke hapa nitafanya hivyo) hili lililotokea Kigoma majuzi lina maswali na mashaka mengi na sasa linaenda kuharibu kabisa 'political ambition' ya kijana.

1. Kuna ushahidi usio na shaka kuwa anataka urais kwa tiketi ya Ujana. Very wrong Zitto! hatuhitaji kijana wala mzee tunahitaji mtu atakayetutoa katika lindi hili la matope ya umasikini, ujinga na maradhi.
Hatuangalii jinsia wajihi, tunachoangalia ni wasifu wake kijamii na kitaaluma.
Tiketi ya ujana anayoitumia Zitto ni ya hovyo sana! Nitty gritty

2. Kafulila kasema walikuwa na kikao Sinza, hakuna shaka kuwa ni kikao cha kumpigia kampeni Rais mtarajiwa kijana.
Ukiangalia orodha ya waalikwa kule Kigoma utaona wazi kuwa Zitto anajenga mtandao wa vijana.
Sidhani kuwa Zitto anahitaji kuwa kijana ili awe Rais! JK alikuwa ni kijana na aliingia kwa gia hiyo leo umma umetambua makosa.Zitto ajinadi kwa hoja na si tiketi chafu, dhaifu na hovyo ya ujana vs uzee

3. Maneno ya Kafulila kuwa Kigoma lazima itoe Rais, ndiyo yale yale aliyosema CDM ni chama cha kikabila.
Wakati akisema hayo kulikuwa na kuhusishwa kwake na Zitto katika harakati za uchaguzi.
Sasa karudia tena akimhusisha Zitto, ni wazi kuwa hiyo ndiyo ngao ya ZZK kwenda Ikulu.
Yaani ukanda na ukabila. Hakuna shaka yoyote kuwa ndiyo maana hakumuunga Slaa mkono wakati wa uchaguzi.
Tatizo ni anapotanguliza Ukanda ya kwamba anataka awe Rais kwasababu anatoka Kigoma kama alivyothibitisha tena Kafulila. Hatuhitaji Rais wa Kigoma au Mtwara, Mwanza au Mbeya, tunataka Rais wa Tanzania! period

4. Zitto anauhadaa umma kuwa hakuandaa tamasha, wakati inajulikana kuwepo kikao cha Sinza.
Anasema mratibu alikuwa Mwasiti Almasi, wakati huo huo anasema 'tulitaka liwe tukio la Kigoma', alitaka na nani? Hatukuta picha sasa za kwenye blog! sasa zitaonwa na Wakigoma tu? Nina maana ya kuwa asijifiche kwenye chaka, yeye atoke na kusema tu tamasha lilikuwa lake kwa maandalizi yake.

Sasa mtu anayetafuta uongozi kwa hila na ghilaba ni hatari sana! Nasema ZZK ni hatari kwa mustakabali wa chama chake na nchi. Mtu anayejiandaa kuligawa taifa kwa jinsia, umri, ukanda na ukabila ni mtu hatari sana!
 
Pasco,

Mimi ni muumini wa Demokrasia ya Kweli. Ni kweli CHADEMA haina mgombea urais hadi 2015.

Dr. Slaa hajatangaza nia ya kugombea urais.Mwaka 2010 hakuna aliyemjua mgombea urais wa CHADEMA hadi Dakika za mwisho. Jambo la msingi ni kwamba chama chetu kinatakiwa kuendelea kujenga umoja.

Pasco,Mara kadhaa hapa umehusishwa kuwa Mfuasi wa aspirant mmoja ndani ya CCM.Unadhani kama chadema itagawanyika itakuwa easy ride kwa huyo aspirant?

Muumini mzuri wa demokrasia ni mfuasi mzuri wa nadharia za siasa na hasa demokrasia yenyewe.Mchakato wa kumpata mgombea urais unaratibiwa na Taasisi ambayo ni chama cha siasa.Taasisi hiyo ni lazima iwe Imara ili ipate mgombea bora na ilani bora itakayoshindanishwa na wagombea kutoka vyama vingine

CHADEMA kina kazi nzito zaidi kuliko CCM.Kwanza inacheza siasa kama mchezaji tegemeo(Rooney/Messi) ambaye anapata pressure ya mashabiki kuivusha timu to the next level.Tunahitaji kuweka nyumba yetu in order.Watanzania wana matumaini makubwa na CHADEMA.Mbiyo za Urais hazitakiwi kutugawa,tumeshavuka level hiyo.

Pasco,Kutangaza nia ya Urais siyo jambo baya lakini ni lazima tuli-handle in a very smart way.Siasa zetu ni tofauti na Kenya.Raila Odinga amezindua kampeni zake late kwa kuwa alitaka kufanyia kazi mgawanyiko ndani ya chama chake na pia kuunda aliiance kulingana na weakness za aspirant wengine

Binafsi napenda mchakato wa Urais 2015 ndani ya chadema uwe na mchuano.Lakini ni lazima tuaandae mazingira ya kujenga chama kwanza.Tujenge taasiasi imara kwanza ili tupate mgombea imara na ilani bora.

Wale wanaotegemea kuona migogoro waendele kusubiri.We'll defeat you

Abraham Lincolin alisema 'you can not make a man strong by weakening another man'. na pia huwezi kuongeza kiwango cha utajiri wa maskini kwa kumuangamiza Tajiri'

Mkuu Ben Saanane, kwanza lazima nikiri wazi kuwa wewe uu miongoni mwa hazina kubwa ndani ya Chadema kutokana na genuinity na objectivity ya majibu yako kwenye hoja hii.

Niliwahi kusema humui kuwa chadema-haijajipanga nilishambuliwa sana. Wapenzi wa Chadema hawakusoma hoja zangu wakaishia kumjadili mtoa hoja!.

Kuna siku nilisema humu jinsi ccm imechokwa mpaka basi!, nikimaanisha there is an opportunity to be seized!.

Siku nyingine niliwaambia chadema, 2015 Ikulu njia nyeupe ila mjipange!, ni wachache waliojibu kwa makini!.

Hiyo siku nilipokaa na Dr. Slaa, nilimweleza reservations zangu kuhusu sio tuu mgombea urais wa Chadema, bali nilieleza kuhusu udhaifu mkubwa wa Chadema katika kuwapata wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uongozi nje ya chama!.

Kwenye Chadema haijajipanga niliwaambia kuwa kuna baadhi ya maeneo, watu wameichoka CCM mpaka basi kiasi kwamba hata kama Chadema ingesimamisha jiwe, hilo jiwe lingepita!. Hii inamaanisha kama Chadema ingesimamisha wagombea kila jimbo, saa hizi mngekuwa na wabunge wengi zaidi ya hawa waliopo!.

Miongoni mwa ushauri wangu kwa Dr. Slaa, Chadema isishobokee wagombea maarufu wala kusubiria makapi ya CCM!, good leaders are made and not born!. Nikashauri, Chadema ifanye incouragement kwa wanachama wake wenye nia mbalimbali za kugombea, wajitanabaishe tangu sasa ili wawe groomed kuja kugombea mara wakati utakapo wadia na sio kusubiria kipenga cha NEC kipulizwe, the time left will be too little too late!.

Nikatolea mfano wa jimbo la Kinondoni, linashikiliwa na CCM miaka nenda, miaka rudi. Mgombea wa CCM tayari anajulikana, weaknesess zake zinajulikana, kama mimi ni mwana Chadema na nina nia ya kugombea Kinondoni come 2015, nitasema sasa na wote wenye nia wajitangaze ili miongoni mwetu, sote tujue nani ni best kutuletea ushindi, ndipo tumgroom tayari kwa kuiteka Kinondoni na sio kusubiri, CCM itamsimamisha nani!.

Mfano kwa Mwaka 2015, Jimbo Ubungo, CCM itampeleka Nape, Jimbo la Kawe, CCM itampeleka Kipi, na majimbo yote yanayoshikiliwa na wapinzani, CCM itapeleka watu makini, kama mimi ni mwana Chadema, najijua uwezo wangu kuiletea Chadema ushindi kwa jimbo la Kawe ni mkubwa kuliko uwezo wa Halima Mdee kulitetea jimbo la Kawe, nitaonyesha nia sasa kwa kujenga mtandao wa mazingira ya ushindi. Muda kuchukua fomu ukifika, mimi nitachukua fomo kwa jimbo la Kawe, Halima nae atajaza, Ben Saanane nae atajaza na Mzee Mwanakijiji pia atajaza, Chadema kitatupima wote, ni nani mwenye chances kubwa za ushindi, kinampitisha kupeerusha bendera ya Chadema. Baada ya kumuengua Charles Mwera Tarime, niliwaambia makosa yenu na jimbo mlilitoa sadaka bure kabisa kwa kukosa busara!.

Kwa sisi wapenzi wa demokrasia ya kweli, tunaamini hakuna mwana Chadema yoyote, mwenye hakimiliki ya kugombea nafasi yoyote. Nafasi zote za uongozi ndani ya chama na nje ya chama, ni haki ya kila mwanachama mwenye sifa, vigezo na uwezo!. Kama Zitto anazo sifa, vigezo na uwezo, kwanini asigombee?.

Kwenye ule uzi wangu wa Chadema Hamjajipanga, niliwaambia Chadema kinakabiliwa na tuhuma za "udini" na "Ukaskazini", japo tuhuma hizi sio za kweli, likini zipo na sio za kupuuzwa!. Nikawashauri ili Chadema kiaminiwe na Watanzania wote, wa dini zote na maeneo yote, lazima hilo koti lenye harufu ya udini na ukaskazini, livuliwe!. Nikawashauri Zitto ni mtaji mkubwa sana kwenye kwenye kuondoa dhana hizo potofu, utumieni vizuri mtaji mlio nao kujiongezea mavuno!.

Japo haikuandikwa popote, wagombea wa urais kwa CCM, wanapokezana, Muislamu na Mkristo!. Alianza Nyerere, Mkristo, akaja Mwinyi, Muislamu, akafuatia Ben Mkapa Mkristo, sasa ni JK, Muislamu, anayefuatia is more likely, Mkiristo (not necesarily). Prof. Lipumba, aligombea kama boya tuu ili kuhakikisha kura za Waislamu wasioipenda CCM, zisiende Chadema!. Kama 2015 CCM itamsimamisha mgombea Mkristo na Chadema ikamsimamisha Zitto ambaye ni Muislamu, Prof. Lipumba, hatathubuti kutia pua, maanayake boya halitaweza kufanya chochote!. Chadema itajivunia kura zote za ukanda wa Pwani zilizokwenda CUF!. Chadema itavuna kura za Waislamu wote wenye msimamo mkali walioko CCM, Chadema itavuna kura zote za Watanzania walioichoka CCM, Kundi kubwa la vijana, waliokata tamaa na kuamua kutopiga kura klwa sababu ya watu wale wale, chama kile kile na mambo yale yale, wakimuona Kijana mwenzao Zitto, anapeperusha bendera kuelekea magogoni, kwanza watajitokeza kujiandikisha kwa wingi, na watapiga kura kwa vingi kiasi cha CCM kuanguka chali, sio tuu kwa kifo cha mende, balki kipigo cha mbwa mwizi!. Hivio hizi opportunities zote za Zitto wenzangu hamzioni?!.

Kwa vile nilishazema toka juzi, jana, leo na kesho nitasema tena, mimi Pasco wa jf, sina chama!. Lakini kiukweli, CCM ndicho chama tawala kilichoko madarakani, namfagilia sana EL kama atakuwa ndie mgombea wa CCM, na nikasema kama afya yake ni mgogoro kuhimili pilika pilika za uchaguzi wa 2015, then the second best candidate kwa CCM ni Membe!.
 
Nipo pamoja nawe tatizo sio Zitto kugombea uraisi ila ni tactic anazotumia.
Nami nakubali tactic anazotumia sio nzuri wala sio sahihi.
Ninachojua ni kuwa rais lazima aandaliwe au ajiandae maana hata huo ubunge tu watu washaanza kasikasi majimboni. Mnataka akurupuke tu 2015. Ni wakati sasa wa kuwapima kwa kila angle hatutaki kuwasikia wakitoa ahadi wakati wa kampeni kwangu Mimi naona itakuwa too late.
Hebu jamani tuwe na muda basi wa kuwapima wagombea wote kwa vyama vyote. Sio dakika za majeruhi mwisho tunaokota koroma.
tatcic aliyoitumia siyo nzuri kwake wala kwa chama chake,so huwa nashangazwa hadi nafikira mara mbili maneno ya watu humu kuhusiana na yeye,ie anatumiwa or ni usalama nk...it's as if to say anamwaga both mboga na ugali at the same time.
 
Pasco,Zitto angekuwa na nia ya urais kiukweli,asingeweza kuact kihivi.Unless na yeye keshaingia kwenye mtego wa magamba wa kuinsult intelligences zetu hapa!Huwezi ukacheza michezo hii ukategemea kuwa rais kama unataka sapoti ya wenye akili timamu.This is just a political suicidal,ni kama tukose wote kwasababu I can't see how chadema watamteuwa kugombea urais akiwa ana act this way,anajuwa kabisa akitaka kushida kuteuliwa,basi ni lazima awin hearts and minds za wanachama wa chama chake.

Kuhusiana na hitaji la mgombea muislam tokea chadema,hilo ni sawa,however,huwezi kusema kwasababu ccm watamsimamisha mkristo,basi chadema watashinda kwasababu wamemsimamisha muislam,it doesn't make any sense kwa hao watanzania unaosema wamezoea rais muislam and then mkristo,ulichokisema kitaleta conflict kwenye theory yako,hence unapplicable.Kama tukishasema kwa uhakika kabisa kuwa udini umeshaota mizizi,then wazo lako sidhani kama ndo solution.Ila ndugu Zitto angekuwa na busara,basi alikuwa na nafasi hiyo,but now it is waay too polarising...
 
Pasco,
Kwa mtazamo wangu hakuna ubaya mtu kutangaza nia yake ya kuongoza.
Hiyo ni haki yake kikatiba na ni haki ya msingi. Kwa upande wa kisiasa hiyo pia ni haki yake ndani ya chama chake kwa kufuata taratibu za chama chake n.k.

Tatizo ninalo liona ni lile la kujificha na kufanya mambo tena ya hatari sana halafu kujiosha ili kuonekana mzuri.
Kuna nyuzi nyingi kuhusu Zitto na yaliyotokea Kigoma.
Hapa nitaongozwa na ukweli. Zitto kama kiongozi ana uwezo wa kujenga hoja na ku-mobilize jamii.

Mara zote amekuwa ni sehemu ya utata kuhusu mitazamo yake kisiasa. Tumewahi kumueleza lakini ana tatizo la kutosikiliza akiamini kuwa ana uwezo wa kila jambo. Kauli zake hazilingani na matendo yake.

Nikiacha yale ya nyuma( nikitakiwa niyaweke hapa nitafanya hivyo) hili lililotokea Kigoma majuzi lina maswali na mashaka mengi na sasa linaenda kuharibu kabisa 'political ambition' ya kijana.

1. Kuna ushahidi usio na shaka kuwa anataka urais kwa tiketi ya Ujana. Very wrong Zitto! hatuhitaji kijana wala mzee tunahitaji mtu atakayetutoa katika lindi hili la matope ya umasikini, ujinga na maradhi.
Hatuangalii jinsia wajihi, tunachoangalia ni wasifu wake kijamii na kitaaluma.
Tiketi ya ujana anayoitumia Zitto ni ya hovyo sana! Nitty gritty

2. Kafulila kasema walikuwa na kikao Sinza, hakuna shaka kuwa ni kikao cha kumpigia kampeni Rais mtarajiwa kijana.
Ukiangalia orodha ya waalikwa kule Kigoma utaona wazi kuwa Zitto anajenga mtandao wa vijana.
Sidhani kuwa Zitto anahitaji kuwa kijana ili awe Rais! JK alikuwa ni kijana na aliingia kwa gia hiyo leo umma umetambua makosa.Zitto ajinadi kwa hoja na si tiketi chafu, dhaifu na hovyo ya ujana vs uzee

3. Maneno ya Kafulila kuwa Kigoma lazima itoe Rais, ndiyo yale yale aliyosema CDM ni chama cha kikabila.
Wakati akisema hayo kulikuwa na kuhusishwa kwake na Zitto katika harakati za uchaguzi.
Sasa karudia tena akimhusisha Zitto, ni wazi kuwa hiyo ndiyo ngao ya ZZK kwenda Ikulu.
Yaani ukanda na ukabila. Hakuna shaka yoyote kuwa ndiyo maana hakumuunga Slaa mkono wakati wa uchaguzi.
Tatizo ni anapotanguliza Ukanda ya kwamba anataka awe Rais kwasababu anatoka Kigoma kama alivyothibitisha tena Kafulila. Hatuhitaji Rais wa Kigoma au Mtwara, Mwanza au Mbeya, tunataka Rais wa Tanzania! period

4. Zitto anauhadaa umma kuwa hakuandaa tamasha, wakati inajulikana kuwepo kikao cha Sinza.
Anasema mratibu alikuwa Mwasiti Almasi, wakati huo huo anasema 'tulitaka liwe tukio la Kigoma', alitaka na nani? Hatukuta picha sasa za kwenye blog! sasa zitaonwa na Wakigoma tu? Nina maana ya kuwa asijifiche kwenye chaka, yeye atoke na kusema tu tamasha lilikuwa lake kwa maandalizi yake.

Sasa mtu anayetafuta uongozi kwa hila na ghilaba ni hatari sana! Nasema ZZK ni hatari kwa mustakabali wa chama chake na nchi. Mtu anayejiandaa kuligawa taifa kwa jinsia, umri, ukanda na ukabila ni mtu hatari sana!
Mkuu Nguruvi3, kwa heshima na taadhima, siwezi bishana na wewe kwa lolote, kwa sababu uu miongoni mwa ma great thinkers wetu wachache wa ukweli humu jukwaani!, ila nakuomba sana ujipambanue kati ya washabiki, wapenzi na wafuasi!. Humu kuna wafuasi wengi wa Chadema ambao wanaabudu 'watu' na kuona nafasi fulani ni za hati miliki za watu fulani fulani tuu, wa dini fulani na ukanda fulani!.

Zitto ni rafiki yangu na tatizo lake kubwa ni "ego" tuu!. Pale mwanzo alipogombea uenyekiti kumchalleng Mbowe, nilimweleza wazi, aseme sabu za msingi za kugombea, na sio tuu kusema eti ni haki yake kikatiba!. Alipojitoa, nikamsisitiza aseme sabu za kujitoa!, hakusema!. That was a mistake!. This time, kama atautaka urais, lazima atasema na sababu zitatolewa!, anachofanya sasa ni kujenga tuu mazingira!.

Natoa wito kwa wapenzi wote wa Chadema, wenye nia njema, onyesheni interest zenu wazi wazi na mapema kuonyesha majimbo mnayoyataka ili mpitishwe kwenye chekecheke na tanuru la moto, mkitoka ni mmewiza na kuwa wagumu kama chuma cha pua!.
 
Nadhani issue hapa ni timing tu; kwa vile yuko active katika politics, timing yake kutangaza nia ya kuwania urais ndilo tatizo kubwa. Timing is everything.

Zito siyo mwislamu pekee ndani ya CHADEMA - iwapo kweli politics za nchi yetu ni za udini kiasi hicho. Hata kama ni hivyo, kuna mambo yanayotakiwa kufanyika kwenye background na yale yanayotakiwa kufanyika waziwazi. Kutangaza nia ya kugombea uraisi leo siyo jambo linalotakiwa kufanyika wakati bado ana majukumu mengine ya kisiasa, kwani kuanzia sasa kila jambo atakalofanya kuna wengi wetu tutajua kuwa siyo kuwa ana uchungu nalo bali ni kwa sababu anataka uraisi wa nchi hii. Ni busara kidogo sana iliyotakiwa hapa kutoka kwa Zitto.
 
Pasco,Zitto angekuwa na nia ya urais kiukweli,asingeweza kuact kihivi.Unless na yeye keshaingia kwenye mtego wa magamba wa kuinsult intelligences zetu hapa!Huwezi ukacheza michezo hii ukategemea kuwa rais kama unataka sapoti ya wenye akili timamu.This is just a political suicidal,ni kama tukose wote kwasababu I can't see how chadema watamteuwa kugombea urais akiwa ana act this way,anajuwa kabisa akitaka kushida kuteuliwa,basi ni lazima awin hearts and minds za wanachama wa chama chake.

Kuhusiana na hitaji la mgombea muislam tokea chadema,hilo ni sawa,however,huwezi kusema kwasababu ccm watamsimamisha mkristo,basi chadema watashinda kwasababu wamemsimamisha muislam,it doesn't make any sense kwa hao watanzania unaosema wamezoea rais muislam and then mkristo,ulichokisema kitaleta conflict kwenye theory yako,hence unapplicable.Kama tukishasema kwa uhakika kabisa kuwa udini umeshaota mizizi,then wazo lako sidhani kama ndo solution.Ila ndugu Zitto angekuwa na busara,basi alikuwa na nafasi hiyo,but now it is waay too polarising...
Mkuu J. Mushi, kwanza siamini kuwa Zitto anatumiwa!. Ila mpaka hapo alipo, kama kuna wana Chadema genuine ambao Zitto bado haja win their hearts and minds, watakuwa ni wale wale waliovaa lile koti lenye "chawa" ambao hawawezi kumkubali kwa sababu zile zile!. Nakuomba sana Mkuu J. Mushi na wewe usijekuingia kwenye kapu lili lile la wafuasi wa Chadema, wanapabudu watu!.

Hiyo sumu ya siasa za ukanda, ukabila na udini, ipo and it works well na imeisaidia sana aliyeipanda sumu hiyo!, tatizo la sumu, ikishasambaa sana, it works against!. Samaki Sato ndio mwenye asili ya ziwa Victoria, enzi hizo, population ndogo, walizaliana kwa wingi wakawa wanapunguza kasi ya maji ku flow Mto Nile, mzungu akampandikiza Sangala ili awale Sato wapungue!, Sasa Sangala sio tuu kawala Sato wapungue, anawamaliza kabisa!, in few years to come, hakutakuwa na Sato tena!.

CCM ameitumia vizuri sana karata ya udini, ukabila na ukanda to its advantage and it worked very well, "Mikoa ya Kusini ni Ngome Yetu". CUF ni chama cha Kiislamu", na "Chadema ni Cha cha Kikiristo tena cha watu wa Kaskazini"!.
"CCM, ndicho chama pekee ambacho sio cha kidini, kikanda wala kikabila"!. Sasa mbegu hiyo iliyopandwa inamea!. Kanda ya Kaskazini, CCM haina chake tena!, Kanda ya Ziwa ndio wanafuatia!. Zitto akipita kuwa mgombea wa Chadema, unadhani kuna CCM tena?. Mimi namuona Zitto kama ndie mkombozi pekee wa Chadema kulivua hilo koti lenye "chawa"!.
 
Mkuu Nguruvi3, kwa heshima na taadhima, siwezi bishana na wewe kwa lolote, kwa sababu uu miongoni mwa ma great thinkers wetu wachache wa ukweli humu jukwaani!, ila nakuomba sana ujipambanue kati ya washabiki, wapenzi na wafuasi!. Humu kuna wafuasi wengi wa Chadema ambao wanaabudu 'watu' na kuona nafasi fulani ni za hati miliki za watu fulani fulani tuu, wa dini fulani na ukanda fulani!.

Zitto ni rafiki yangu na tatizo lake kubwa ni "ego" tuu!. Pale mwanzo alipogombea uenyekiti kumchalleng Mbowe, nilimweleza wazi, aseme sabu za msingi za kugombea, na sio tuu kusema eti ni haki yake kikatiba!. Alipojitoa, nikamsisitiza aseme sabu za kujitoa!, hakusema!. That was a mistake!. This time, kama atautaka urais, lazima atasema na sababu zitatolewa!, anachofanya sasa ni kujenga tuu mazingira!.

Natoa wito kwa wapenzi wote wa Chadema, wenye nia njema, onyesheni interest zenu wazi wazi na mapema kuonyesha majimbo mnayoyataka ili mpitishwe kwenye chekecheke na tanuru la moto, mkitoka ni mmewiza na kuwa wagumu kama chuma cha pua!.
Pasco samahani kama utakuta like halafu then haipo,nilikupatia like kwasababu ya sentensi ya mwanzo kuhusu Nguruvi wa tatu.Ila niliitoa baada ya kuona kuwa mengine hayakustahili "like",samahani kwa usumbufu,sikuiondoa like kwa ubaya mkuu,Nguruvi wa tatu ni great thinker,period!
 
Japo haikuandikwa popote, wagombea wa urais kwa CCM, wanapokezana, uislamu na Mkristo!. Alianza Nyerere, Mkristo, akaja Mwinyi, Muislamu, akafuatia Ben Mkapa Mkristo, sasa ni JK, Muislamu, anayefuatia is more likely, Mkiristo (not necesarily). Prof. Lipumba, aligombea kama boya tuu ili kuhakikisha kura za Waislamu wasioipenda CCM, zisiende Chadema!. Kama 2015 CCM itamsimamisha mgombea Mkristo na Chadema ikamsimamisha Zitto ambaye ni Muislamu, Prof. Lipumba, hatathubuti kutia pua, maanayake boya halitaweza kufanya chochote!. Chadema itajivunia kura zote za ukanda wa Pwani zilizokwenda CUF!. Chadema itavuna kura za Waislamu wote wenye msimamo mkali walioko CCM, Chadema itavuna kura zote za Watanzania walioichoka CCM, Kundi kubwa la vijana, waliokata tamaa na kuamua kutopiga kura klwa sababu ya watu wale wale, chama kile kile na mambo yale yale, wakimuona Kijana mwenzao Zitto, anapeperusha bendera kuelekea magogoni, kwanza watajitokeza kujiandikisha kwa wingi, na watapiga kura kwa vingi kiasi cha CCM kuanguka chali, sio tuu kwa kifo cha mende, balki kipigo cha mbwa mwizi!. Hivio hizi opportunities zote za Zitto wenzangu hamzioni?!.

Kwa vile nilishazema toka juzi, jana, leo na kesho nitasema tena, mimi Pasco wa jf, sina chama!. Lakini kiukweli, CCM ndicho chama tawala kilichoko madarakani, namfagilia sana EL kama atakuwa ndie mgombea wa CCM, na nikasema kama afya yake ni mgogoro kuhimili pilika pilika za uchaguzi wa 2015, then the second best candidate kwa CCM ni Membe!.
Mkuu wangu haya yatakuwa makosa makubwa sana kwa Chadema kumsimamisha mtu kwa sababu ya uuwiano na mawazo finyu ya watanzania ktk Udini.. Kama CCM huwasimamisha marais wake kwa kufuata utaratibu wa dini - Mktistu kisha Muislaam kwa kila miaka sijui 10 basi siku Chadema nao wakiiga ujinga huu najitoa mapema kwa sababu hatumhitaji rais anayeongoza makundi ya dini. Maadam nchi yetu haina dini ina maana haitamtambua kiongozi na viongozi wetu kwa dini zao.. Hii haikubaliki kabisa isipokuwa nachoweza kusema ni kwamba ili kuondoa dhana ya Udini ndani ya Chadema, viongozi wa Chadema na wanachama wake wanatakiwa kujihadhari sana na mamlaka wanayowakabidhi watu hasa kwa kuzingatia hofu ya watu ktk Ukaskazini na Udini.. Utaweza tu kupiga vita Udini na Ukaskazini kwa kuupiga vita Udini na Ukabila lakini sio kuuwezesha upande mwingine..

Kuna msemo mmoja kuhusu Empowering women usemao kwamba huwezi kumpa mwanamke silaha ya kumuumiza mwanamme as empowering women pia wala sii kumwondolea mwanamme fursa na nafasi alokuwa nazo mwanamme ashuke kama mwanamke isipokuwa kinachotakiwa ni kupokea fikra na mawazo ya wanawake yakaenziwa ili kuwawezesha wanawake wote washiriki sawa ktk maswala yanayohusu maisha yao na jamii kwa ujumla..

Zitto hawezi kuwa ticket ya Waislaam kukipigia kura Chadema, maana chuki yao ni Chadema na sii Zitto. mapenzi yao ni CCM na sii JK maana miaka yote waislaam wamekuwa wapiga kura wazuri sana wa CCM toka enzi za Mwalimu.. Nitasema wazi haijawahi kuttoke mkutano wala sherehe Dar zilzizomwondoa record ya Nyerere ktk mikutano yake yote iwe Karume, uwanja wa Taifa au redioni. Hakuna rais aliyewahi kusikilizwa kwa maanani, kwa mahudhurio makubwa kama Nyerere iwe Dar, Tanga, Kigoma, Songea au Mtwara ama kokote kule nchini..
 
Ndugu Pasco,mara nyingine huwa nashindwa kuiquote post yako directly wakati natumia smart phone.So niwie radhi,ila hili bandiko ni kujibu bandiko lako lililopita ukielekeza kwangu.

Kiukweli,makosa ninayoyaona ya Zitto,ni kutokuonekana akitoa sapoti with all his heart to his party,so maybe inawezekana theory ya ndugu Mkandara kwamba ukishaitwa mwizi kila mara,basi inawezekana ukakubaliana na kuact kama mwizi ni ya ukweli.Nakubaliana naye kwa kiasi fulani tu,kwasababu kwa upande mwingine,sijawahi kusikia busara za Zitto kupinga hilo la udini na ukanda ndani ya chama chake,so kama hafanyi hivyo,nashangazwa ni kwanini hajiondoi kwenye chama hicho na wala hajawahi kupinga kuwa tuhuma za udini na ukabila dhidi ya chama chake ni za uongo.So kimtizamo wa chama,hiyo siyo positive move,kama una koti la chawa,basi unalivua,ama unalianika mchana kweupe kwenye jua ili chawa wakimbie.Ndo maana nikasema ni kama hataki kugombea kupitia chadema na anatafuta wakati muafaka wa kujitoa,kwasababu timing na tactic zake havionyeshi kutaka maelewano na chama,wala kugombea kwa tikiti ya chama hicho,hilo limepelekea mimi kujiuliza kama ni kweli anataka kuwa rais kwa tiketi ya chadema.
 
Back
Top Bottom