Urais 2015 tusimlaumu Zitto: Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa?

Urais 2015 tusimlaumu Zitto: Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa?

Nilipokuwa nikisoma boarding school,mwezi mtukufu wa ramadhani,afya yangu ilikuwa ikijengeka sana kwasababu ya maakuli bora ya mfungo.Mwezi wa Ramadhani ulikuwa ukifika,ilikuwa furaha hata kwa "makafiri" wenye marafiki wakaribu ambao ni waislam kama ilivyokuwa kwangu.We huwa unadowea daku?
J. Mushi, "kafir" ni mtu asiyeabudu kabisa!. Wakristo sio makafiri, hata wapagani, nao wana miungu yao wanayoiabudu!.

Mimi huwa sidewei daku, bali huwa nafuturu kihalali kabisa!. Kuikweli napenda futari! ila sio daku!.
 
PASCO najua unachokijadili hapa,si kingine nilishawahi kukuambia unawania u-Rweyemamu wa 2015.Ila angalizo:CDM ni chama cha watu,wataamua nani apeperushe bendera.
Ni kweli kabisa, niliania sana UDC nilipokosa, sasa nawania kupitia kwa Ziito!.
 
Pasco acha hizo tangu lini wewe umekuwa mshauri wa CDM.
Kumbe ukitoa ushauri wowote humu jf ndio unageuka mshauri wa Chadema?. Mimi kama mwanachi wa kawaida, nikutanapo na hawa viongozi wetu, huwa free kuzungumza lolote, kushauri lolote na kuuliza lolote!. Au kwa vile mimi ni mfuasi wa EL sasa ndio mnashangaa ninavyomsupport Zitto?!.
 
Sijaelewa ni kwanini Pasco amemrukia Dr Slaa? Ni kitu gani hasa kilichomsukama Pasco aone Dr Slaa is fair game kwenye mjadala wa urais toka upande wa Zitto? Why Dr Slaa?
Mkuu FJM, Zitto alipogombea uenyekiti Chadema, yalimkuta haya haya kwa vile kuna wana Chadema wanaabudu watu!, kwao maadam Mbowe ni Mwenyekiti, yoyote atakaye mchallenge huonekana adai na kitendo hicho kinaonekana kama ni usaliti!.

Baada ya uchuguzi wa 2010, tuliaminishwa kuna watu ndio walioshinda kihalali, matokeo yakachakachuliwa, akatangazwa aliyeshindwa!. Kuapishwa kukasusuri na hotuba ya uzinduzi bunge pia ikasusiwa na kauli kali "hatumtambui"!.

Hivi ni viashiria tosho kuwa kwa Chadema, tayari inae mgombea urais wa 2015, hivyo any move from anybody wa Chadema na urais wa 2015, unaonekana ni usaliti!.

Nikawauliza, hivi mnaujua msimamo wa huyo mtarajiwa?!. Kwa vile niliongea nae off the record, naujua msimamo wake!, nawashauri Zitto asimbezwe!.

Amini nawaambieni, harakati hizi zingefanywa na Dr, hakuna yoyote ambaye angetia neno!.
 
Mkuu, Pasco,
Mi nachoona unampigia Zitto kampeni,je kuna hata Dr.Slaa amekuambia kuhusu msimamo wake ina maana hakuna wengine zaidi yake?sielewi maana huu si mda wa kuzungumzia kuhusu urais ila zitto anapoanza hizi kauli inaonyesha kabisa kuna reason behind.
 
Last edited by a moderator:
Pasco,anajua sana anchokifanya......Anatafuta easy ride kwa aspirant wake wa ccm mwaka 2015.Anaelewa tishio la chadema kuwa na unity.CHADEMA itavuka salama.Tutashinda uchaguzi mkuu 2015.

Like a compass that always points in the direction of the magnetic north after every disturbance, so the attitude of its members always assumes the poise of unity after every episode of unrest.

We cannot beat our chests and pride ourselves on the party. We should not rest content with this height that we have been able to carry the party to. The room for self improvement is the largest room in life.

There is ever room for improving ourselves and by extension, our party. I do not believe that what we have attained today is the picture that the founding fathers of our great party projected when they rallied round for its establishment.

Mkuu Ben, ni kweli kwa CCM chaguo la mgombea wa kusimamishwa ni EL mpaka kesho, kana ni kweli afya yake ni mgogoro, then I support Membe!.

Kwa mtu asiye na chama kama mimi, I just wish to get the best for this nation. EL ndie the one and only best of the best wa CCM!. Zitto is of of the best Chadema has!. Najua wengi wenu mna mtu wenu!, if you cant get what you want, just take what you get!.

Kama unataka kutoka point A kwenda point B, na ulipanga lazima uruke kwa helcopter, isipokuja, na usafiri uliopatikana ni gari, wewe panda gari safari eiendelee!. Na taka gari ikikosekana, ikapatikana bajaj, wee panda, hata boda boda wee panda, hata baiskeli, panda tuu au vikikosekana vyote, tembea hata kwa miguu!, ili mradi ufike safari yako!.

Huyo mgombea wako ndio ile choper au gari, Zitto ni kibajaj, mimi ninazo taarifa za choper, nawashauri mpande hicho hicho kibajaj ili mfike 2015!.
 
Mkuu, Pasco,
Mi nachoona unampigia Zitto kampeni,je kuna hata Dr.Slaa amekuambia kuhusu msimamo wake ina maana hakuna wengine zaidi yake?sielewi maana huu si mda wa kuzungumzia kuhusu urais ila zitto anapoanza hizi kauli inaonyesha kabisa kuna reason behind.
99 Problemaa, nimpigie Zitto kampeni ya nini?, mimi si nafahamika wazi mgombea wangu ni nani na ni wa chama gani?.
Huu ni ushauri nimewapa watu wa Chadema!. Kama kuna na wengine si na wao wajitokeze, washindanishwe!.
 
Inafamika mgombea wako ni EL,kwanini hujiulizi maadui wa CDM ndo wanaompenda Zitto?kwanini Zitto anapata support nje ya CDM?hapo ndo sehemu maadui wa CDM wanataka kupenyeza iliwa wasambaratishe CDM maana wanajua Zitto akisimamishwa itakuwa rahisi wao kufanikiwa na ndoto ya kuendelea kukaa kwenye mamlaka itatimia
 
J. Mushi, "kafir" ni mtu asiyeabudu kabisa!. Wakristo sio makafiri, hata wapagani, nao wana miungu yao wanayoiabudu!.

Mimi huwa sidewei daku, bali huwa nafuturu kihalali kabisa!. Kuikweli napenda futari! ila sio daku!.
Mkuu una uhakika na unayoyasema?ebu tummulize ndugu Mkandara kama wewe ukiwa mkristo ama huna dini basi wewe ni mkafiri,pengine nimekosea,niko tayari kusahihishwa.
 
Kwa vile nilishazema toka juzi, jana, leo na kesho nitasema tena, mimi Pasco wa jf, sina chama!. Lakini kiukweli, CCM ndicho chama tawala kilichoko madarakani, namfagilia sana EL kama atakuwa ndie mgombea wa CCM, na nikasema kama afya yake ni mgogoro kuhimili pilika pilika za uchaguzi wa 2015, then the second best candidate kwa CCM ni Membe!.

Mwenye masikio na asikie!.

Pasco.
12:24 am

Hawa ni aina mbili tofauti kabisa ya viongozi in character, experience and positions on issues; kutokana na hili, ni dhahiri kwamba iwapo wote watafikia hatua ya kuingia kwenye top five katika uchaguzi wa ndani CCM iwapo watagombea na hivyo kupata wasaa wa kujieleza mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa, tofauti hizi zitaonekana bayana kabisa kwani kwa mfano, kila mmoja atakuwa na msimamo tofauti kabisa juu ya wapi anadhamiria kuipeleka nchi yetu kimaendeleo, nini viwe vipambele vya sasa, muda wa kati na muda mrefu in terms of domestic issues and foreign policy kisiasa, kijamii na kiuchumi; kutokana na hili, ndugu Pasco, ningependa kujua, je:

1. Ni vigezo gani unavyotumia kujenga hoja kwamba best candidate ni Lowassa and Membe as the second best candidate?

2. Na kwa vile inaonyesha kwamba unaona Zitto pia can make a good presidential candidate, ni kigezo gani unatumia kujenga hoja yako, hasa ikizingatiwa kwamba Zitto, Membe na Lowassa ni aina tatu tofauti kabisa ya viongozi based on hoja yangu ya msingi hapo juu?
 
Pasco ukishanijulisha kama umegunduwa kuwa wewe ni kafiri,naomba pia unijulishe kama na wewe hudowea daku.Mimi nimekiri nilidowea licha ya kuwa kafiri,pointi yangu hapa ni kuonyesha kwamba tulikuwa tukiishi side to side bila wasiwasi kama sasa.
 
Wakuu kwanza lazima nikiri wazi kuwa baadhi ya wapenzi wa Chadema mliojibu uzii huu uu miongoni mwa hazina kubwa ndani ya Chadema kutokana na genuinity na objectivity ya majibu yenu makini kwenye hoja hii.

'Genuinity' ndiyo nini?
 
Hawa ni aina mbili tofauti kabisa ya viongozi in character, experience and positions on issues; kutokana na hili, ni dhahiri kwamba iwapo wote watafikia hatua ya kuingia kwenye top five katika uchaguzi wa ndani CCM iwapo watagombea na hivyo kupata wasaa wa kujieleza mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa, tofauti hizi zitaonekana bayana kabisa kwani kwa mfano, kila mmoja atakuwa na msimamo tofauti kabisa juu ya wapi anadhamiria kuipeleka nchi yetu kimaendeleo, nini viwe vipambele vya sasa, muda wa kati na muda mrefu in terms of domestic issues and foreign policy kisiasa, kijamii na kiuchumi; kutokana na hili, ndugu Pasco, ningependa kujua, je:

1. Ni vigezo gani unavyotumia kujenga hoja kwamba best candidate ni Lowassa and Membe as the second best candidate?

2. Na kwa vile inaonyesha kwamba unaona Zitto pia can make a good presidential candidate, ni kigezo gani unatumia kujenga hoja yako, hasa ikizingatiwa kwamba Zitto, Membe na Lowassa ni aina tatu tofauti kabisa ya viongozi based on hoja yangu ya msingi hapo juu?
mchambuzi,kuwaamini ccm kutatoka wapi?Labda hili swali ni specific kwa Pasco,kama ni pa kuipeleka nchi kuna slogan bora kutoka ccm kama ile ya "maisha bora kwa kila mtanzania"?Kwa wengine wetu,hakuna watakachosema ccm tukawachukulia serious,so tatizo mnalo chama kizima.
 
Na ndio maana ningependa kujua vigezo ambavyo vinamfanya pasco kuona best candidate in Lowassa and Membe ni best alternative.
 
'Genuinity' ndiyo nini?

Nadhani ni typo tu...na alimaanisha "ingenuity" - kwamba wapenzi wa Chadema humu wana portray inventiveness and skills katika kuchambua mambo na kujenga hoja kuhusu discussions husika. Vinginevyo katika lugha ya wenzetu ya kiingereza, hakuna neno "Genuinity".
 
Hivi nyie mnaompinga Zitto mnafahamu maana ya demokrasia? Katiba ya nchi mnaijua kweli kama ana haki ya kuongea chochote ilimradi asivunje sheria?
 
pasco unapenda misifa,.eti msimamo wa slaa unaujua wewe!na mbona signature yako inafanana na msimamo wa paschal mayalla alioutoa alipokuwa anamhoji le mutuz le baharia ze big show @ kivukoni,dsm city,.are you one and the same person as jf members have always suspected?
 
Pasco my brother, sasa umeanza kutuonesha rangi yako, ki ukweli sijajua locus stand yako, kama leo atajulikana mgombea wa CDM vipi kuhusu wana CCM wanaoutaka uraisi kupitia CDM na watakaohamhia kipindi cha uchaguzi tutawapata? kama leo kila jimbo litamjua mgombea wake mapema iko wapi demokrasia iliyotukuka CDM?Pasco Mbona hili usiliongelee kwa kupitia CCM? ama kwa kuwa wana nec yao? Kazi ya WASILA haitatimia kamwe, mitandao imetusaidia sana, ni ngumu sana...., feedback imeongezeka ktk jamii yetu.
 
kuna mtu kasema watu wengi wa cdm hawatasupport zito kugombea the issue here is, zitto umri wa kuigombea bado anao ila dr. wa ukweli anakubalika kwa sana sasa Pasco na wenzenu mnamuhofia, watu wenye sifa za kugombea urais cdm watatajwa muda ukifika.
 
Back
Top Bottom