Wanabodi,
Mara baada ya mazishi ya Mhe. Regia, (RIP), on route back to Dar, nilibahatika kukutana mahali na Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wibroad Slaa akiwa na wife wake, Fina, tuliendesha mazungumzo mafupi, informal, na miongoni mwa maswali niyomuuliza, ni hili la iwapo atagombea tena nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi wa 2015!.
Nayakumbuka vizuri sana majibu ya Dr. Slaa kuhusu swali hilo!. Kwa vile mazungumzo yale hayakuwa rasmi, kuna uwezekano mkubwa, Dr. Slaa alizungumza "off the record", sio busara kuyaleta mazungumzo ya "off the record" kwenye public na kuyaweka "on the record" bila "idhini" ya msemaji.
Kwa vile msimamo wa "Dr. Slaa kuhusu kugombea urais 2015, mimi naujua!, nawashauri, wale wote wanaumlaumu au kumshutumu
Zitto, kuonyesha nia ya kuwania urais wa 2015 kwa tiketi ya Chadema, kwa kujenga mazingira "impliedly" not "expressly"!, wasimlaumu bali wamsupport!.
Hivi kuna ubaya gani, kuonyesha nia ya kuwania the highest office?. Wote wanaoutaka urais, huitwa "presidential hopeful", hivi kuna ubayo wowote to aim high?!.
My Take.
Kwa vile mchakato wa kuwania urais wa 2015 bado haujaanza rasmi kwa vyama vyovyote, lakini tunashuhudia "presidential hopefuls" wa vyama mbalimbali wakijenga mazingira kupitia mikakati mbalimbali, nawaombeni wapenda demokrasia ya kweli, tuwe open minded kuhusu watu hawa, tusianze kuwanyooshea vidole vya kuwashutumu bali tunapaswa kuwaunga mkono kwa nguvu zote ili at the end of the day, tumpate mgombea bora kabisa!,
Mfano hakuna ubishi kuhusu uwezo wa Zitto katika masuala ya organization na mass mobilization!, hakuna ubishi kuhusu nguvu ya Zitto katika ushawishi na kujenga hoja na kusimamia utekelezaji. Kama ni kweli Zitto ni "presidential hopeful" ndani ya Chadema na sasa anajenga mtandao wa kuandaa mazingira hayo, this is very healthy kwa Chadema, kwa sababu by the time muda wa mchakato rasmi unawadia, na Chadema ikampitisha Dr. Slaa kupeperusha tena bendera ya Chadema, huo mtandao wa Zitto ndio utakuwa an added advantage kwa ushindi wa kishindo wa Chadema, na Zitto ndio atafaa zaidi kwa post ya Waziri Mkuu, kama alivyofanya Obama na Hillary Clinton!.
Kufuatia mimi kuufahamu msimamo wa Dr. Slaa, lets support Zitto or anybody else!,
Mhe. Zitto, just follow your dreams, "Sky is the limit!".
I wish Zitto all the best!.
Wasalaam.
Pasco. (wa jf).
NB.
Pasco wa jf, sio mwanachama, mshabiki au mkereketwa wa chama chochoite cha siasa, bali ni muumini wa demokrasia ya kweli.
Leo nimeamua kuutembelea huu uzi huku nikujiuliza mara mbili mbili, nilimsupport ZZK alipoonyesha nia, ila sisuport kitendo cha ZZK kuitangaza nia hiyo hadharani na kumfanya yeye ndie kuwa mpiga ngoma ya ngoma yake mwenyewe!, alipaswa kazi ya kupiga ngoma, awaachie wengine, na yeye aingie kucheza!.
Support yangu kwa ZZK ni kuonyesha nia ya kuutaka urais, 2015, "impliedly", not "expressly"!
Pasco.