Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,601
- 34,760
Mkuu Pasco,
Kama umenisoma vema nimesimama katika hoja ya kuwa kutangaza nia ya urais si kosa. Ni haki kabisa na kwa namna yoyote ile inabaki kuwa haki ya mtu. Lakini usisahau kuwa kila kitu kina mipaka na taratibu. Sijui taratibu za CDM ila kwa mkakati wa kisiasa kuna mambo mtu anaweza kufanya na kubomoa hata kama amedhamiria kujenga.
Ninasimamia ukweli na wala sifungamani na ushabiki unazi au upenzi. Kwa hili sakata la Kigoma nimeweka wazikuwa video ipatikane ili tuitathmini na kufikia conclusion kadri ya kila mmoja wetu.
Maana yangu ni kuwa Zitto asihukumiwe kwa kauli za wengine. Tunachotaka hapa ni kuondoa unafiki na mimi nasema ikidhihirika vinginevyo tutawaambia wahusika wote bila haya wala soni.
Historia inaonyesha kuwa Zitto hajawahi kukemea ukabila, udini na umri. Anavyozidi kukaa kimya huku akifungamanishwa na makudi ya kina Kafulila inatupa picha na habari nyingine zaidi ya tuzijuazo.
Kwa vile msimamo wangu ni demokrasia ya kweli, natumaini watu wote wa vyama vyote watapewa fursa sawa katika kuwania nafasi za uongozi. Lakini sitakaa kimya hata siku moja kwa kiongozi anayetaka uongozi kwasababu ya kabila, dini, umri au jinsia. Huyu nitamkana hadharani bila aibu wala kificho.
Sikubaliani na dhana ya ujana au kubadalishana uongozi kwa misingi ya dini. Hatuchagui masheikh wala maaskofu.
Ninashangaa kuona India nchi iliyokuwa inamilikiwa na Hindu kwa miaka dhahari imevuka mipaka na kuweka kiongozi wa Ki-Singh, Mamohan Singh. Angalia jinsi nchi inavyopaa.
China hawana viongozi wa kiislam wala kikristo, angalia nchi inavyopaa.
Hata huko Marekani kuna viongozi katika bunge wadini zisizokuwa rasmi. Sisi tumeng'angania udini.
Ndipo ninaungana na Mkuu Mkandara kuwa zamu za uongozi ni upofu uliotopea na hatua inayofuata ni ujinga. Nitty gritty!
Kuhusu endapo watu wanajua kilicho moyoni mwa Dr Slaa, hakika hakuna ajuaye kama tulivyokuwa hatujui ya Mwinyi, Mkapa au JK. Nadhani muhimu ni kuangalia kiongozi anasimamia nini na anatetea sera gani kwa hoja na si kwa dhana.
Hakika hakuna ambaye tunaweza kujua dhamira yake.
Na mwisho nikumbushe kuwa katika uongozi kuna mambo mengi sana yakuzingatia.
Baadhi ya vitu vinavyomtengeneza kiongozi ni kama Charisma(haiba), popularity(umaarufu), intellectual (weledi) n.k.
Ukicheza karata vema kwa vitu hivyo unaweza kufanikiwa katika siasa.
Muhimu sana ni 'intellectual' ambayo si degree tu, bali kiongozi anavyoweza kuji-present, present his or her ideas, communication, emotion nk.
Lakini pia katika siasa kuna kitu wanasema ni 'political strategy' mkakati wa kisiasa na huu hufungamana sana na timing
Unaweza kuwa na vitu vyote lakini ukashindwa kufikia matamanio kwakukosa kitu kidogo tu, political strategy.
Sijui kama nimeeleweka!