Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Money, Power and Respect
Ndo karma aliyopewa na mwenyez mungu
Bernard_Membe_2009_(cropped).jpg
 
Kila kitisho kinapangiwa mkakati wa kudhibitiwa mapema kwenye awamu hii. Huwezi kuamini kuwa utawala huu unatishwa na hata kauli tu za wapita njia. Hii hofu sijui imetokea wapi ?

Tukianza na wapinzani hasa baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa 2015, mipango ilipangwa kuvuruga nguvu ya upinzani iliyotokana na uchaguzi huo. Kuzuiwa kwa mikutano, maandamano, kuibuliwa kwa migogoro ya vyama (mfano CUF), kuchukuliwa wapinzani kuingizwa CCM kwa njia mbali mbali zikinasibishwa na ufisadi, viongozi wa upinzani kusumbuliwa kwa mashtaka yasiyo kichwa wala miguu n.k ni miongoni mwa mbinu hizo. Lengo ni kudhibiti kitisho cha upinzani

Lengine ni kudhibitiwa kwa vyombo vya habari makini na kupotezwa waandishi makini waliojaribu kuhoji mienendo ya baadhi ya matukio. Na vile vile kupitishwa sheria za maudhui ya mtandao uliokusudiwa kudhibiti taarifa. Utawala huu uliona kitisho cha kupata habari na kuja na mbinu hizo.

Utawala haukuishia hapo, ulikuja na mikakati ya kudhibiti kila aliyehisiwa pengine haendani na matakwa ya awamu hii, kundi hili linajumuisha watu mchanganyiko. Wamo wafanyabiashara mbali mbali, wafanyakazi serikalini, asasi n.k.

UWEZEKANO WA MEMBE KUTEGWA ILI ABWAGWE.

Hilo linawezekana, upepo hauko vizuri kwa waliopigania chama(CCM) na kuwa silaha muhimu za awamu ya nne. Kutajwa mzee makamba, Katibu Kinana, Mama Hawa Ghasia na akina Membe picha inajichora. Utawala huu umebaini makosa au umekosea kwa makusudi. Ni wazi chama kina makundi sasa ingawa hawataki ionekane hivyo.

Joto lililoko ndani linawapa tabu CCM na yumkini linawatia hofu huko mbele ya safari. Watu na makundi yaliyoathiriwa na utawala huu ni wengi wakiwemo wana CCM waandamizi. Kitisho kilichopo yawezekana ni ndani ya CCM wenyewe na sio upinzani. Membe ni alama ya MATUMAINI YA WANA CCM WALIOJERUHIWA. Utawala unaweza kuwa umebaini kuwa kuendelea kumuacha Membe ni kujihatarisha na kuhatarisha chama.

Inawezekana kuna mpango wa kutaka kuondowa kitisho hiki mapema kwa njia za kitaalamu ili kuinisuru CCM kwenye ngwe ya lala salama. Hawataki kurejea makosa yale ya Mh Lowasa yaliyoiathiri CCM mwaka 2015. Kwa mtazamo huo Membe labda ametegwa sasa ili aingie kwenye kumi na nane za hawa watu wanaoogopa kivuli chao. Usishangae ikawa kuna mkakati tayari aitwe, ahojiwe, kuandaliwe maazimio na kumuweka pembeni mapema ili kuondowa kitisho.

Makosa ya awamu hii ni mengi , nchi imechafuliwa taswira yake kimataifa, hali ya umoja wa kitaifa ni mbaya, kuna uadui mwingi , watu wamechafuliwa maisha yao, watu wamepotezwa na wengine kuuwawa na wasiojulikana. Utawala hautaki kurudi nyuma umeamuwa kupambana na vitisho na kusonga mbele. Kwa hali hio haitoshangaza Membe akatoswa. Na labda kinachotakiwa ni kutengenezwa msingi wa kutoswa.

Waamuzi wa yote ni wana CCM wenyewe. Tulisema Uraisi haujaribiwi na kwa mara ya kwaNZA MAJARIBU HAYA YAMEITIKISA TANZANIA NDANI NA NJE.

Utawala huu ni waoga mno, wameshaharibu na kujirekebisha hawawezi. Wanaamini kujirekebisha kuwa ni KUSHINDWA, wanaendelea kuharibu na kuivuruga nchi. Sasa ni zamu ya sulubu kwa upande wa wana CCM , Membe ndio kaanza kwenye kitisho cha uraisi. Ni uwoga tu. Kivuli kinawatisha kwa waliyoyatenda.

namini wengi watakuwa vitisho na tutaona namna yao watakavyodhibitiwa.

Wakati utaamua

Kwa hisani ya watu wa Tanzania

Kishada
 
Yamesemwa mengi sana juu ya hizi sura mbili na ukiona watu wanakusema sana basi ujuwe unakubalika.
Twende sasa na hawa viumbe watatuvusha salama.
FB_IMG_1543828528329.jpeg
 
Mpambano ni mkali na wa kusisismua. Tangu lini tumewahi kuishiwa vituko na matukio katika nchi yetu. La Korosho limepita sasa ni zamu ya katibu wa chama kile, Bwana Ally na kada wao Bernard Membe.

Membe ambaye ni rafiki wa marehemu baba yangu, ameitwa kujieleza pale Lumumba. Ana shutuma nyingi ikiwamo kuhusishwa kugombea urais mwaka 2020 ingawa hajavunja katiba ya chama chao.

Nilicheka nilipoona majibu ya Membe kwa katibu wake. Kuna mahala aliandika neno ‘ugeni’ akimaanisha katibu alikuwa mgeni katika masuala ya kuendesha chama, hakufuata utaratibu.

Hapo ndipo nilipomshangaa. Wakati mwingine asiishi kwa kukariri, kwa jinsi mambo yalivyobadilika Lumumba inawezekana sasa yeye ndiye mgeni na si katibu wake. Kuna mambo mengi ya uendeshaji pale Lumumba yamebadilika.

Chama alichokiacha ni tofauti na kilichopo. Kwa mfano ajiulize hivi aliuacha utaratibu wa sasa wa mwanachama kupokelewa kutoka upinzani kisha anapitishwa moja kwa moja kuwa mgombea?.

Kuna mengi yaliyobadilika ambayo yanamfanya yeye kuwa mgeni. Katibu mkuu aliyepita naye siku hizi ni mgeni. Hata katibu mkuu wa zamani zaidi, baba yake January naye anakuwa mgeni.

Kwa mfano, hili la kugombea mwaka 2020 sio dhambi. Ni utaratibu ambao haupo katika maandishi kwamba rais aliyopo lazima agombee tena baada ya miaka mitano ya kwanza. Zamani aliyekuwa anajiweka kifua mbele kutaka kugombea katika mazingira kama hayo alikuwa anaelezwa kistaarabu kwamba aachane na mpango huo. Kwa sasa inaonekana ni dhambi.

Ndani ya chama kipya ambacho kinamfanya Membe kuwa mgeni ni wazi kwamba hilo ni kosa la kuitwa mbele ya vikao tena kwa mwito wa hadharani bila ya kuandikiwa barua.

Huo ni moto wa watendaji wanaojaribu kukiunda chama kipya ndani ya chama cha zamani.

Hii inawafanya makada wengi wazito wa zamani waonekane wepesi na wageni ndani ya chama chao. Membe aachane na habari ya kudhani katibu ana ugeni. Hapana, yeye ndiye mgeni katika chama kwa sasa.
 
Wote hovyo ni wachumia tumbo hamna mzalendo hapo. Uzalendo wao ni wa porojo tu
 
Kweli hata sura ya Membe walau inaleta matumaini.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Kila kitisho kinapangiwa mkakati wa kudhibitiwa mapema kwenye awamu hii. Huwezi kuamini kuwa utawala huu unatishwa na hata kauli tu za wapita njia. Hii hofu sijui imetokea wapi ?

Tukianza na wapinzani hasa baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa 2015, mipango ilipangwa kuvuruga nguvu ya upinzani iliyotokana na uchaguzi huo. Kuzuiwa kwa mikutano, maandamano, kuibuliwa kwa migogoro ya vyama (mfano CUF), kuchukuliwa wapinzani kuingizwa CCM kwa njia mbali mbali zikinasibishwa na ufisadi, viongozi wa upinzani kusumbuliwa kwa mashtaka yasiyo kichwa wala miguu n.k ni miongoni mwa mbinu hizo. Lengo ni kudhibiti kitisho cha upinzani

Lengine ni kudhibitiwa kwa vyombo vya habari makini na kupotezwa waandishi makini waliojaribu kuhoji mienendo ya baadhi ya matukio. Na vile vile kupitishwa sheria za maudhui ya mtandao uliokusudiwa kudhibiti taarifa. Utawala huu uliona kitisho cha kupata habari na kuja na mbinu hizo.

Utawala haukuishia hapo, ulikuja na mikakati ya kudhibiti kila aliyehisiwa pengine haendani na matakwa ya awamu hii, kundi hili linajumuisha watu mchanganyiko. Wamo wafanyabiashara mbali mbali, wafanyakazi serikalini, asasi n.k.

UWEZEKANO WA MEMBE KUTEGWA ILI ABWAGWE.

Hilo linawezekana, upepo hauko vizuri kwa waliopigania chama(CCM) na kuwa silaha muhimu za awamu ya nne. Kutajwa mzee makamba, Katibu Kinana, Mama Hawa Ghasia na akina Membe picha inajichora. Utawala huu umebaini makosa au umekosea kwa makusudi. Ni wazi chama kina makundi sasa ingawa hawataki ionekane hivyo.

Joto lililoko ndani linawapa tabu CCM na yumkini linawatia hofu huko mbele ya safari. Watu na makundi yaliyoathiriwa na utawala huu ni wengi wakiwemo wana CCM waandamizi. Kitisho kilichopo yawezekana ni ndani ya CCM wenyewe na sio upinzani. Membe ni alama ya MATUMAINI YA WANA CCM WALIOJERUHIWA. Utawala unaweza kuwa umebaini kuwa kuendelea kumuacha Membe ni kujihatarisha na kuhatarisha chama.

Inawezekana kuna mpango wa kutaka kuondowa kitisho hiki mapema kwa njia za kitaalamu ili kuinisuru CCM kwenye ngwe ya lala salama. Hawataki kurejea makosa yale ya Mh Lowasa yaliyoiathiri CCM mwaka 2015. Kwa mtazamo huo Membe labda ametegwa sasa ili aingie kwenye kumi na nane za hawa watu wanaoogopa kivuli chao. Usishangae ikawa kuna mkakati tayari aitwe, ahojiwe, kuandaliwe maazimio na kumuweka pembeni mapema ili kuondowa kitisho.

Makosa ya awamu hii ni mengi , nchi imechafuliwa taswira yake kimataifa, hali ya umoja wa kitaifa ni mbaya, kuna uadui mwingi , watu wamechafuliwa maisha yao, watu wamepotezwa na wengine kuuwawa na wasiojulikana. Utawala hautaki kurudi nyuma umeamuwa kupambana na vitisho na kusonga mbele. Kwa hali hio haitoshangaza Membe akatoswa. Na labda kinachotakiwa ni kutengenezwa msingi wa kutoswa.

Waamuzi wa yote ni wana CCM wenyewe. Tulisema Uraisi haujaribiwi na kwa mara ya kwaNZA MAJARIBU HAYA YAMEITIKISA TANZANIA NDANI NA NJE.

Utawala huu ni waoga mno, wameshaharibu na kujirekebisha hawawezi. Wanaamini kujirekebisha kuwa ni KUSHINDWA, wanaendelea kuharibu na kuivuruga nchi. Sasa ni zamu ya sulubu kwa upande wa wana CCM , Membe ndio kaanza kwenye kitisho cha uraisi. Ni uwoga tu. Kivuli kinawatisha kwa waliyoyatenda.

namini wengi watakuwa vitisho na tutaona namna yao watakavyodhibitiwa.

Wakati utaamua

Kwa hisani ya watu wa Tanzania

Kishada
Wakina Membe wako wengi ndani ya chama Bernard ni curtain riser tu.....watajitokeza wengi time will tell....
 
Wanajamvi
Salaam;

Nakumbuka kuna mtu anaitwa Dr.Bashiru Ally ambaye aliteuliwa kuwa Katibu mkuu wa CCM-Taifa,baada ya uteuzi wake aliahidi kuwa hatafanya Siasa za majukwaani kwa sababu nafasi hizo zina watu wake.

Na akaongeza kuwa yeye ni mtendaji mkuu wa Chama,hivyo atashughulika zaidi na kazi za utendaji na watendaji walio chini yake. Kwa ufahamu wangu nilijua atatumia nafasi hiyo kuwa ofisini zaidi kutoa maelekezo kwa watendaji wa chini yake. Na ki msingi mimi binafsi nilimuelewa sana..kwa sababu hata katika ngazi ya Taifa bado kuna Katibu wa Siasa na uenezi.

Lkn nashangaa kwa sasa kuna mtu anatrend sana kwenye vyombo vikubwa vya habari hapa nchini na kwenye mitandao ya kijamii akiwa Jukwaani akieleza na kufafanua mambo ya Chama na kuwatisha wanachama walio kinyume na mawazo yake na Mwenyekiti wake. Nimebaki najiuliza,hivi aliyekataa Siasa za majukwaani ndo huyu kweli!??

Bahati mbaya aliyesema hataki Siasa za majukwaani sikubahatika kuona sura yake,lkn huyu wa sasa nimemuona. Halafu huyu wa majukwaani anaonekana mkali sana,amemuita kujieleza hata mwanadiplomasia Ndugu Bernad Membe. Hebu nisaidieni kunijuza,huyu ni mtu mmoja au wapo wawili!??

Nawasilisha...
 
Mwanasiasa nguli wa CCM, na raisi ajaye ndugu Bernard Membe, uhusiano wake na Clinton umeanza kuwatia kiwewe watawala.

Inasemekana Membe ananguvu kubwa kutoka US na Ulaya, swali ni ndugu Membe kuna wakupambana naye nje na ndani ya CCM ?

Cheki hawa watu afu linganisha na marafiki kutoka Uganda na Rwanda.
IMG_20181203_122819.jpeg
IMG_20181203_122935.jpeg
 
Wakina Membe wako wengi ndani ya chama Bernard ni curtain riser tu.....watajitokeza wengi time will tell....

Na ndio itazidisha chungio la kuchekechea kuwa kali kwa watakaopitishwa kwenye CC na NEC, hapo ndio utajuwa hicho kitisho kilivyo cha juu sana
 
Kwann hii kampeni imeshika kasi sana baada ya Bashiru kumuita?

Je, wamekoleza moto?
 
Mkuu unatest kina cha maji na mguu, tafuta fimbo 🙂
 
Back
Top Bottom