Kila kitisho kinapangiwa mkakati wa kudhibitiwa mapema kwenye awamu hii. Huwezi kuamini kuwa utawala huu unatishwa na hata kauli tu za wapita njia. Hii hofu sijui imetokea wapi ?
Tukianza na wapinzani hasa baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa 2015, mipango ilipangwa kuvuruga nguvu ya upinzani iliyotokana na uchaguzi huo. Kuzuiwa kwa mikutano, maandamano, kuibuliwa kwa migogoro ya vyama (mfano CUF), kuchukuliwa wapinzani kuingizwa CCM kwa njia mbali mbali zikinasibishwa na ufisadi, viongozi wa upinzani kusumbuliwa kwa mashtaka yasiyo kichwa wala miguu n.k ni miongoni mwa mbinu hizo. Lengo ni kudhibiti kitisho cha upinzani
Lengine ni kudhibitiwa kwa vyombo vya habari makini na kupotezwa waandishi makini waliojaribu kuhoji mienendo ya baadhi ya matukio. Na vile vile kupitishwa sheria za maudhui ya mtandao uliokusudiwa kudhibiti taarifa. Utawala huu uliona kitisho cha kupata habari na kuja na mbinu hizo.
Utawala haukuishia hapo, ulikuja na mikakati ya kudhibiti kila aliyehisiwa pengine haendani na matakwa ya awamu hii, kundi hili linajumuisha watu mchanganyiko. Wamo wafanyabiashara mbali mbali, wafanyakazi serikalini, asasi n.k.
UWEZEKANO WA MEMBE KUTEGWA ILI ABWAGWE.
Hilo linawezekana, upepo hauko vizuri kwa waliopigania chama(CCM) na kuwa silaha muhimu za awamu ya nne. Kutajwa mzee makamba, Katibu Kinana, Mama Hawa Ghasia na akina Membe picha inajichora. Utawala huu umebaini makosa au umekosea kwa makusudi. Ni wazi chama kina makundi sasa ingawa hawataki ionekane hivyo.
Joto lililoko ndani linawapa tabu CCM na yumkini linawatia hofu huko mbele ya safari. Watu na makundi yaliyoathiriwa na utawala huu ni wengi wakiwemo wana CCM waandamizi. Kitisho kilichopo yawezekana ni ndani ya CCM wenyewe na sio upinzani. Membe ni alama ya MATUMAINI YA WANA CCM WALIOJERUHIWA. Utawala unaweza kuwa umebaini kuwa kuendelea kumuacha Membe ni kujihatarisha na kuhatarisha chama.
Inawezekana kuna mpango wa kutaka kuondowa kitisho hiki mapema kwa njia za kitaalamu ili kuinisuru CCM kwenye ngwe ya lala salama. Hawataki kurejea makosa yale ya Mh Lowasa yaliyoiathiri CCM mwaka 2015. Kwa mtazamo huo Membe labda ametegwa sasa ili aingie kwenye kumi na nane za hawa watu wanaoogopa kivuli chao. Usishangae ikawa kuna mkakati tayari aitwe, ahojiwe, kuandaliwe maazimio na kumuweka pembeni mapema ili kuondowa kitisho.
Makosa ya awamu hii ni mengi , nchi imechafuliwa taswira yake kimataifa, hali ya umoja wa kitaifa ni mbaya, kuna uadui mwingi , watu wamechafuliwa maisha yao, watu wamepotezwa na wengine kuuwawa na wasiojulikana. Utawala hautaki kurudi nyuma umeamuwa kupambana na vitisho na kusonga mbele. Kwa hali hio haitoshangaza Membe akatoswa. Na labda kinachotakiwa ni kutengenezwa msingi wa kutoswa.
Waamuzi wa yote ni wana CCM wenyewe. Tulisema Uraisi haujaribiwi na kwa mara ya kwaNZA MAJARIBU HAYA YAMEITIKISA TANZANIA NDANI NA NJE.
Utawala huu ni waoga mno, wameshaharibu na kujirekebisha hawawezi. Wanaamini kujirekebisha kuwa ni KUSHINDWA, wanaendelea kuharibu na kuivuruga nchi. Sasa ni zamu ya sulubu kwa upande wa wana CCM , Membe ndio kaanza kwenye kitisho cha uraisi. Ni uwoga tu. Kivuli kinawatisha kwa waliyoyatenda.
namini wengi watakuwa vitisho na tutaona namna yao watakavyodhibitiwa.
Wakati utaamua
Kwa hisani ya watu wa Tanzania
Kishada