Nakiomba chama cha mapinduzi, kwa heshima na taadhima, tuleteeni Jina la Bernad Membe kama mgombea wa urais 2020 kupitia chama hicho.
Ninajua kuna utaratibu usio rasmi wa mtu kuwa mgombea vipindi viwiliviwili vya miaka mitano mitano, lakini utaratibu huo uliwekwa makusudi kwa sababu kuu. mbili
(1)Mosi, ili kama raisi aliyeko madarakani ataonekana hatoshi basi wananchi waweze kumuondoa. Hii iliwekwa kwa busara sana kuwa heri nusu shari kuliko shari kamili
(2)Pili, ili kama rais aliyeko madarakani ni mzuri basi apewe miaka mingine mitano aendelee kuwafanyia mambo wananchi.
Sasa kwa muktadha huo ni dhahiri kuwa uongozi tulio nao unaangukia katika nukta ya kwanza hapo juu, uongozi huu wa sasa umefanya Mengi mabaya na machache sana mazuri, Mabaya ni. kama yafuatayo
1. Hali ya umasikini nchini imezidi kuwa mbaya zaidi. Ajira rasmi zimekuwa shida, Wafanyakazi hawajaongezewa nyongeza za mishahara yao iliyohalali kabisa kwa mujibu wa mikataba yao ya ajira kwa miaka minne sasa tunaenda wa tano
2. Kutoheshimu haki za wananchi
chini ya uongozi wa sasa, haki ya mwananchi ya kuchagua na kuchaguliwa inakanyagwa waziwazi, mfano mzuri ni uchaguzi wa juzi wa serikali za mitaa. Wananchi kubambikiwa kesi zisizo na dhamana ili kuwakomoa, kwa mfano kesi za akina zkabendera Tito Ngetti
3. Kutoheshimu sheria za nchi na katiba
Kitendo cha kufanya manunuzi yenue thamani ya matrilion ya pesa bila kupitia bunge kwa mfano manunuzi ya ndege za bombadia za mwanzoni ni jambo ambalo ni kinyume cha sheria
4. Wananchi wana hofu
Hofu ya kupotezwa, kubambikiwa kesi, kutekwa ni hofu ambayo imewagubika watu chini ya utawala huu
5. Udini na ukanda unaonuka
Tumeona katika uongozi huu kukiwa na teuzi ambazo kwa kiwango kikubwa zimekaa kidinidini, watu wa dini moja wanateuliwa utadhani hawapo, ni watu wa kutupiatupia tu kama vile kuzugia, lakini majority ya teuzi zimelalia watu wa dini moja.
6. Ukosefu wa staha katika kauli
Uongozi wa awamu hii unaongoza kwa kauli zisizo na staha kwa mfano "nitapiga mashangazi wenu", "Kwani serikali ndiyo iliyoleta tetemeko, mwafaa", "
Kwa nini Tunamtaka Membe
(1) Ana uzoefu mkubwa wa Uongozi
(2)Hajawahi kuitia nchi hasara katika historia ya maamuzi yake kama kiongozi
(3)Ni mkweli siyo mnafiki
(4)Siyo MDINI na siyo MKABILA
(5)Ana exposure kubwa, ataitengeneza diplomadia yetu na kutuwezesha kunufaika katika diplomasia ya uchumi
(6)Hana viashiria vya Udikteta ni mkarimu, ni msikivu na ni mweledi wa nchi maana kwa nyadhifa alizohudumu kama Kachero mbobezi anaijua hii nchi nje ndani, anajua vizuri watu wake na hali zao, anajua vizuri kuwa sisi ni watu masikini na anajua namna ya kupambana na umasikini.
HITIMISHO
Raisi Magufuli miezi miwili iliyopita aliwaambia wana CCM kuwa CCM ina hazina kubwa ya watu wenye uwezo mkubwa wa kuongoza nchi kuliko hata yeye, Kwa hivyo basi iwapo huu ndo ukweli ulivyo nakisihi sana chama vha Mapinduzi kituleter mgombea mzuri na bora zaidi kuliko Magufuli kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.
Na kwa kweli katika watu wote ambao ni potential ndani ya CCM sioni mtu mwenye sifa na vigezo vya kumzidi BENARD CAMMILIUS MEMBE.
CCM tuleteeni Membe anatufaa zaidi kwa sasa kuliko mtu mwingine yeyote ndani ya CCM