Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Vipi? Unafanya kazi ya kufufua wafu? Akili bomu , huyo!
 
Unaongea na mimi ama unaongea na simu? hah hah buyu la asali tamu sana wewe! Nani ataacha!?
 
Jamani watanzania wenzangu mtaacha lini ndoto za mchana? Raisi tunaye tayari labda wazeni mgombea wa uraisi wa 2025 hadi 2030.
 

Jamaa hajui kuwa CCM wameshabadiri taratibu na ni lazima mihula miwili, kuna mgombea mwingine 2020.
 
Jamaa hajui kuwa CCM wameshabadiri taratibu na ni lazima mihula miwili, kuna mgombea mwingine 2020.
jamaa hafuatilia siasa za nchi hii kabisa...ki ufupi amekurupuka
 
Niwazi kuwa kuna watu watatoka mapovu kwa ushauri huu, lakini hakuna jinsi dawa hata kama ni chungu ili tupone hatuna budi kuimeza, ukweli ni kwamba mh B C Membe ni mwanadiplomasia aliye bobea sana katika nchi yetu , ni kiongozi anayeweza kurudisha heshima yetu kama watanzania katika sura yake ile ya zamani.
Kulingana na hali ilivyo na hakuna asiyejua kuwa wananchi wana mhitaji MTU atakaye waletea faraja na kuwafuta machozi ambayo kila mmoja Amelia kwa njia zake wengine sasa imebaki na michirizi mashavuni mwao huku wakiwa wamekata tamaa kwani haijui hatma ya kesho yao, bomoa bomoa imeliza wengi , wanafunzi katika vyuo vikuu wamebaguliwa kwenye mikopo, ajira imekuwa nikilio kisicho koma kila kukicha, wakulima ndo usiseme hawajui hatma yao nini ukianzia kwenye pembejeo hadi kwenye masoko kwao ni giza tu, wafugaji hawana maskani katika nchi yao kila wanapo hamia kwa ajili ya kulisha mifugo wanaonekana kuwa maadui wanafukuzwa wamebaki kutanga tanga ndani ya nchi yao,wavuvi ndo usiseme nyavu zimechomwa kwa kile kinacho itwa nyavu haramu bila ya kuonyesha mkakati wa kuzileta hizo nyavu bora, wafanyakazi wamesha nyanyaswa mpaka basi, mishahara haipandi , madaraja hawapandishwi, wafanya biashara ndo usiseme wamebanwa na mfumo wa kodi usio kuwa rafiki na biashara zao. Yapo mengi sana.
Na ndio maana mwanadiplomasia makini kama Membe ana hitajika, awe ndani ya CCM au hata nje ya CCM , umefika muda muafaka sasa jitokeze 2020 watanzania wakupe kura za kutosha na bado nasema Membe unatosha sasa kuingia ndani ya gari letu ,funga mkanda, shika usukani, washa gari safari mpya ianzwe.
 
Hali ya kama zamani ni zamani gani yaani ya raisi gani?

Alafu kwa nini huyo membe hakuonekana wakati magufuli naye anamkakati wa kuwa raisi?

Lau kungekuwa na yeyote anayefaa kabla ya magufuli pasi angewekwa huyo kabla ya maagufuli.

Ila atakaekuwa raisi 2025(2020 ashajulikana)ni huyu majaliwa kassim
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…