Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Watanzania always huwa tunafikiri the next is better than the prev, wakuu, huyu mkwere mm simfagilii hata kidogo, kwanza ni mdogo wake na mkwere yule aliyepita, hivyo tunarudi kulekuleeeeeeee, picnic za majuu kila weekend na mtaanza kulalamika soon kwamba afadhali jiwe angeendelea tu, kitu ambacho mtakuwa mmechelewa miaka miamoja. Binafsi jiwe angeendelea kwa miaka mingine 20 ingekuwa poa sana sababu naona kabisa nchi inajongea na maendeleo yanaonekana kwanmacho.
Wewe usituharibie pozi ukitaka kuongozwa miaka 20 na hiyo shida yako iombe ihamie nyumbani kwako ikuongoze hatumtaki
 
"......... ..ikulu ni mzigo mzito........ukimuona mtu anakimbilia/kutafuta urais kwa njia yoyote ile na anatoa fedha ili kufanikisha.....huyo hatufai kabisa... na muogopeni kama ukoma.... .....
.........." mwlm JK
 
Hakuna watu WAPUMBAVU kama % fulani ya wabongo, yani mmekaa wanaume na map.umbu yenu kusapotiana vitu vya kusadikika?,Kama Lowassa alichemsha na kubaki kuwa raisi wa mitandaoni huyo Membe sio 2020 tu hata 2025 hawezi kuwa kiongozi wa nchi hii.Sana Sana mnamtafutia matatizo naye apigwe Parkinson Disease aanze kutetemeka tu.Tatizo ni pale mnapo undersetimate Serikali ya Tanzania, achana nayo kabisa msiichukulie kama Jamii Forums ambapo mtu anaota ndoto mchana anaamka anaileta humu na waotaji wenzake Kama yeye wanampa likes.
 
Ni mtazamo binafsi lakini wenye kuakisi ukweli... CCM inaandaliwa kuingia kwenye wakati mgumu tena, ni mtifuano wa ndani kwa ndani
. Urais 2020
. CCM asili dhidi ya CCM makinikia(mabaki)
. CCM kindakindaki dhidi ya CCM maslahi (wakuja)
Bernard Camilius Membe diplomat na jasusi wa muda mrefu, mshindwa wa kinyang'anyiro cha urais ngazi ya chama bado hajakubali kushindwa, bado ana ndoto ileile ya kukalia kiti kikubwa na amekamia hasa
Haiba ya Membe ni reincarnation ya haiba ya Kikwete (carefree) ni tofauti kabisa na haiba ya mzee baba KUKAZA hasa.... Membe ni expert mzuri sana kwenye mahusiano ya kimataifa, na pengine kwenye ushushushu lakini si kwenye siasa tena kukalia kiti kikubwa
Kipindi kile wakati wa kutafuta nafasi ya kuteuliwa, hakuonesha tofauti na wanaccm wengine, hakuongea cha ziada, wote walifanana... Hakutupa dira na maono ya tulipotoka, tulipo na tunapoelekea.. Wote katika ujumla wao ndani ya CCM walifanya mahubiri ya kisiasa
Akiwa shina moja na JK, ana sehemu kubwa ya lawama nchi ilipokuwa imefikia kipindi kile, kumpa usukani na kuendelea kuchanja mbuga kuelekea maporini

Sasa basi kwanini nasemwa asibezwe?! Huyu ni tarumbeta ya kupaza sauti ya wanaccm wengi wanaougulia kimyakimya na kushindwa kuongea kwa uwazi, kwa sauti
Huyu ni sauti ya manung'uniko ya wanaccm wengi ambao hawaridhishwi kabisa na mwenendo wa chama kwenye kila kitu lakini kubwa kuliko yote ni kule kuwapa wahamiaji (haramu) madaraka na nafasi za upendeleo... Wanapatwa na hisia kuwa kuna CCM mpya inaundwa taratibu ndani ya CCM halisi (CCM ya mwenyekiti dhidi ya CCM ya wote)
Ni kupitia hayo kwa uchache ndani ya mengi chamani, Membe ananijenga kwa kasi ya ajabu, na harakati zake hizo zilianza mara baada ya uchaguzi mkuu.... Membe ana kundi kubwa nyuma yake.. Ni vigumu kumdhibiti kama walivyodhibitiwa kina Makamba Jr, Lameck, Nape nk.. Huyu ni kada mzoefu chamani na wa muda mrefu... Ametumwa...!!

2019 hiyoo bado siku chache tu, Membe yuko nje ya nchi anakotuhumiwa kupanga mambo yasiyowapendeza watu fulani.. Huku wengine wakiona ni sawa... Hapa ni swala la mizania.. Nani ana wafuasi wengi zaidi wa hiari...
Membe anarudi kukanusha/kujibu tuhuma,.. Anajipanga kisawasawa, ameshaanza kusafishiwa njia na timu zake mitandaoni .... Ni yeye tu ndio anasikika na kujadiliwa... Na kwa sehemu kubwa akisemwa vizuri na akitabiriwa vema... Hivi vitu havifanyiki kwa bahati mbaya... Ni mipango inayosukwa kwa ustadi sana..

Hivyo basi pamoja na kwamba hatoshi kukalia kiti kikubwa, lakini ni tishio kubwa... Akiamua (kwa nguvu ya wapambe wake) ataiteka December yote.... Atavuruga hasa... Atawavuruga.... Na CCM itaingia 2019 ikiwa mapande makubwa matatu
. CCM mwenyekiti
. CCM Membe
. CCM wengine
Ujumbe huo wa Nape unabeba siri kubwa nyuma ya kinachoendelea sasa chamani... Muda utasema..
IMG-20181201-WA0141.jpeg
 
Hahaahh hamna inafichwa. Kati ya bilioni 600 alizoahidi hajalipa hata bilioni Moja.unaambiwa wakulima wanaogopa kujtokeza ukisema una gunia mia ya korosho unaambiwa tupeleke shambani ulipolima tuone kama kuna uwiano. Masharti yaliyopo mkuu acha mi nimepigiwa simu na jamaa yangu ni mfanyabiashara ya kororosho huko kusini
Ahh mbona inasemekana wakulima wanapokea cash money ya korosho mkuu!

Ova
 
Kama kawaida njaa zinaendelea kutikisa vichwa vya watu[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Ndoto
Roho yangu inaniambia, Novemba 2020 tunamwapisha Cammilius kuwa raisi hapo uwanja wa Taifa Dar es salaam.

Iwapo hili litakuwa naamini haya ndiyo mambo kumi na sita ya awali kabisa ambayo rais Membe atatakiwa kufanya ndani ya siku 100 za kukaa ofisini

1. Kuhuisha mchakato wa katiba mpya, Watanzania tunataka katiba mpya, iliyobora, yenye kuchukua mengi ya rasimu ya Jaji Warioba. Bila Katiba mpya nzuri tutaendelea kupiga mark time bila kusogea kama Taifa.

2. Kurekebisha sheria ya Habari na Makosa ya mitandao, hakuna taifa linaloweza kuendelea kwa kulimit uhuru wa watu wake kutafuta na kupashana habari, hata hiyo China wanayoitolea mfano, ni baada ya kiongozi shupavu Deng Xiaoping kuifungua China iliyokuwa imefungwa na sera za Mao ndo wachina wakaanza kuerevuka na kuona ulimwengu hasa wa west unaendaje na hivyo na wao kusonga mbele

3. Kuhakikisha ndani ya siku 100 kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, itakayohusisha vyama vyote, hili likiwa ni kuliponya Taifa lililogawanyika kutokana na sera za kibabe za utawala uliomtangulia

4. Kuomba msamaha kwa niaba ya serikali wale wote waliovunjiwa nyumba, waliobambikiziwa kesi, juu ya waliopotea na kuhakikisha anatangaza Fidia kwa wale wote waliokumbwa na kadhia hii, na kuahidi kuwa havitatokea tena

5. Kutangaza kuwa serikali haitaingilia wakulima kwenye kujitafutia soko bora la mazao yao, na kwamba serikali itakuwa tayari kutumia ofisi zake za kibalozi duniani kote kuwatafutia masoko Wakulima kama amvavyo Kassim Majaliwa alifanikiwa kuwatafutia wakulima wa Korosho masoko, lakini wazo lake hilo likakataliwa dakika ya mwisho na bosi wake mbele ya Kadamnasi

6. Kurekebisha sheria ya takwimu, kuondoa vikwazo vya kufanya tafiti na kuirudisha Tanzania kwenye mikataba ya kuendesha nchi kwa uwazi

7. Kutangaza mara moja kuuza ndege zote zilizonunuliwa katika utawala huu, na badala yake kupeleka pesa kwenye kutengeneza Liganga na mchuchuma ili kiwanda hicho kitoe chuma kitakachojenga SGR badala ya kutumia mamilioni ya Dola kuagiza chuma kutoka nje

8. Pamoja na kwamba kutakuwa na serikali ya umoja wa Kitaifa, atangaze kuheshimu demokrasia, uhuru wa mawazo, kukosoa na kukosolewa.

9. Atangaze vita kali dhidi ya ufisadi, aanzishe mchakato wa kuwafikisha wote mahakamani mafisadi, Siyo apige kelele za kupambana na ufisadi majukwaani, bali atende, tuone ufisadi ukipigwa vita kwelikweli bila kuonea mtu

10. Atangaze kulipa malimbikizo yote ya wafanyakazi, kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa sheria za utumishi, sheria hii ya mafao ya 25% iondoke , watoto wenye mimba waruhusiwe kuendelea na masomo.

11. Kwa Msamaha wa Rais, aamuru wale wote walioondolewa kazini kwa vyeti feki lakini umri wa kukaribia kustaafu umewakuta karibia na kustaafu, basi kwa kuwa wamelitumikia Taifa kwa muda mrefu, tusibeze mchango wao, wapewe stahiki zao!

12. Siku ya kwanza kabisa ofisini autangazie umma kuwa anataka kuona bunge lenye meno makali, lililo live!

13. Atangaze uchunguzi wa Shambulio la Lissu, uchunguzi wa kupotea kwa Ben Saanane, Azory, Kanguye na yeyote yule ambaye hatumjui

14. Kufumuafumua serikali za mitaa, kuondoa ambao siyo wataalamu na kuweka wataalam na Kuzirejeshea Halmashauri nguvu za Kukusanya ushuru kwenye maeneo yao, hususan Ushuru wa mabango etc.

15. Kuunda Serikali yenye sura ya Kitaifa, Serikali yenye uwakilishi wenye sura ya Kitaifa ( Siyo proportionally unateua Waislamu wengi mpaka Wakiristo wanashtuka kulikoni, Au proportionally unateua Wakiristo wengi mpaka waislamu wanaona hapa kuna udini wa wazi, kitu ambacho hakiwakilishi demographic composition ya kitaifa, Au unateua watu wa Kanda ya Kusini wengi mpaka watu wa Ksnda nyingine wanahisi kuna Ukanda hapa). Harmony katika nchi ni muhimu, na lazima serikali iwe na sura ya KITAIFA

16. Kuhuisha Maridhiano huko Zanzibar!

Cammilius uwezo wa kuwa Rais unao, Sababu ya kuwa raisi unayo, na najua nia ya kuwa raisi unayo, HEBU FANYA KWELI BASI!!!

N.B
Katiba inaniruhusu kutoa maoni, na kuwa na mawazo ya kutaka kuona nchi yangu inakuwaje na inaongozwaje, Siyo Uhaini kutaka kumuona mtu fulani anakuwa rais!. HAKI YANGU YA KIKATIBA IHESHIMIWE!
 
Membe ni chama gani?
Kama ni kilekile huo ni upuuzi.
Labda kazi na bata maana hata chadema ni wasanii tu.
 
Stone tangawizi akae pemben, kasababisha chuki za kiitikadi. Ccm wa sasa hv hata mpinzan akipigwa risas wanashangilia huku zaman tulikua tunalia pamoja
 
Hahaahh hamna inafichwa. Kati ya bilioni 600 alizoahidi hajalipa hata bilioni Moja.unaambiwa wakulima wanaogopa kujtokeza ukisema una gunia mia ya korosho unaambiwa tupeleke shambani ulipolima tuone kama kuna uwiano. Masharti yaliyopo mkuu acha mi nimepigiwa simu na jamaa yangu ni mfanyabiashara ya kororosho huko kusini
Duh

Ova
 
MAKAMANDA mna roho ngumu sana mlikuwa na Safari ndefu sana ya Lowasa,sasa hivi mmeanzisha safar ya MEMBE,2020 naiman mtaanzisha safar nyingine,msichoke atafutae hachoki naimani 2050 anagalau mtaisongelea kidooogo Ikulu ya CHAMWINO!
 
Back
Top Bottom