Kwa wasiojua, Mwendazake aliona watu wanajipanga kuelekea 2025 mara tu baada ya uchaguzi. Waziri mmoja (Mr. February Maropes), wa miti na mifuko ya plastiki, alikuwa akizunguka nchi nzima akihimiza mambo ya mazingira huku akiweka mizizi yake kwenye mashina nchi nzima. Mwenda zake alipogundua hili linafanyika, akiwa njiani kuelekea Lindi, alimpigia simu Bw. Maropes akiwa njiani na kumuonya kuhachana na huo ujinga mara mara moja. Baada ya muda kidogo, akatimuliwa na uwaziri
Baada ya hapo, hawa vijana na mwingine ambaye alifanyiwa mambo pale St. Peter’s, (Mbunge wa Ulezi) waliungana nguvu kuanza kujenga kundi kubwa ndani ya chama, wakijinasibu kama chaguo la watanzania kuelekea 2025. Cha ajabu kama siyo mtego wa Mama ili waharibu, basi ni fursa kwao kwa maana huyu Bw. Maropes, anajaribu kusuka shirika la solar, akiweka watu ambao ni wazuri kwenye fitna watakaomsaidia kwenye kampeni zake kuelekea 2025. Nadhani mama ameshagundua mchezo mzima wa Bw. Maropes unaofadhiliwa na CCM-Asilia. Kwa mfano, Mr. Gachuma ni mafia wa kanda za ziwa. Huyo mzee siyo mchezo. Tunamjua mchechu na Mafuru. Tunamjua mama Maajar…….Hii ni Kampeni ya 2025 Ndg. Marope kasuka kwa ustadi