Urais SAUT, Saimon Philibert aibuka kidedea

Urais SAUT, Saimon Philibert aibuka kidedea

Nicholaus Kilunga

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2014
Posts
1,188
Reaction score
570
Urais SAUT, Saimon Philibert aibuka kidedea
Ajizolea kura lukuki

uchaguzi watawaliwa na amani

Ndugu Saimon Philibert mwanafunzi wa mwaka wa pili kutoka katika kitivo cha sanaa ya elimu (BAED 2) ameibuka kidedea katika uchaguzi wa kumtafuta rais wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino tawi kuu la mwanza baada ya kumshinda mpinzani wake ndugu Godfrey Gaston kutoka kitivo cha sheria (LLB 3)uchaguzi uliofanyika juzi 18/03/2014,Akitangaza matokeo hayo msimamizi mkuu wa uichaguzi huo na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi chuoni hapo bwana Bakari ,alimtangaza ndugu Philibert kuwa mshindi wa nafasi hiyo nyeti kabisa chuoni hapo ambapo Philibert alishinda kwa kura 2582 dhidi ya mpinzani wake ndugu Gaston aliyepata kura 1373 kati ya jumla ya kura 4003 zilizopigwa na kura 8 kuharibika.

Mchakato wa kumtafuta rais wa chuo hicho ulianza tangu tarehe 11/03/2014 kwa wagombea takribani 15 kujitokeza kuchukua form za kuwania urais wa chuo na baada ya mchujo uliofanywa na tume ya uchaguzi ya chuo yalibakia majina 4 yaliyoongoza miongoni mwa watu hao 15,majina ambayo kiutaratibu hupelekwa ngazi ya juu ya chuo(senet)kwa ajili ya mchujo zaidi na majina mawili kurudi,wagombea walifanya mdahalo mkubwa siku ya jumatatu jioni katika ukumbi wa M13 uliopo chuoni hapo ambapo wagombea walimwaga sera zao na kuulizwa maswali.
akizungumzia uchaguzi huo mmoja ya wajumbe alisema licha ya zoezi zima la uchaguzi kuendeshwa kwa uwazi,haki na huru lakini zilikuwepo changamoto kazaa za wapambe wa wagombea kuchafuana kwa misingi ya vyama na wanafunzi wachache kujitokeza kupiga kura"unaweza kuona chuoni kuna zaidi ya wanafunzi 12500,lakini waliojitokeza kupiga kura ni wanafunzi 4003"hili si jambo jema na halitoi mwelekeo mzuri kwa taifa letu hasa tukitarajia wao kama wasomi kuwa wakwanza kutimiza haki yao hiyo ya kikatiba ili wakawe mabalozi wazuri huko waendapo pindi wamalizapo chuo.
Mgombea mwenza wa Philibert ambaye kwa mujibu wa katiba ya serikali ya wanafunzi anakuwa makamu wa rais ni bi MerryGoreth Gervaz kutoka kitivo cha sayansi ya jamii (BASO 2) na yule wa ndugu Gaston ni bi Barnabas,uchaguzi chuoni hapo hufanyika kila mwaka,na bwana Philibert anakuwa rais wa 11 tangu chuo kianzishwe ambapo anaenda kumpokea kijiti rais aliemaliza mda wake ndugu Dovakamwene Mcheshi.
picha chini ni rais mpya wa chuo ndugu Philibert

c 1912105_362536063885452_1546923992_n.jpg
pichani ni rais mpya wa chuo cha mtakatifu Augustino (SAUT Mwanza) bwana Saimon Philibert kutoka BAED 2

:wave:
 
Huyu hawezi kuwa kwenye chama cha abakorakamo.
Kwanza ni Mkristo, Pili hatokei UJIJI, tatu sio msukule wa yule mwana msaliti wa Mwandiga
 
Last edited by a moderator:
Hongera kwake na pia atekeleze majukumu yake kiweledi zaidi.
 
Huyu hawezi kuwa kwenye chama cha abakorakamo.
Kwanza ni Mkristo, Pili hatokei UJIJI, tatu sio msukule wa yule mwana msaliti wa Mwandiga

ACT ni chama cha watu wa dini na kabila zote, act sio wabaguzi kama chadema
 
Last edited by a moderator:
ACT ni chama cha watu wa dini na kabila zote, act sio wabaguzi kama chadema

Chama kimeasisiwa Msikitini UJIJI na mkapewa sharti la kutumia Nyota kiwe chama cha dini zote? Salum Mwigamba ni dini gani?
 
Chama kimeasisiwa Msikitini UJIJI na mkapewa sharti la kutumia Nyota kiwe chama cha dini zote? Salum Mwigamba ni dini gani?

chadema kimeanzishwa kanisani kwenye kigango cha katoliki, kinaongozwa na padri alieasi na kupora mke wa mahimbo
 
Chama kimeasisiwa Msikitini UJIJI na mkapewa sharti la kutumia Nyota kiwe chama cha dini zote? Salum Mwigamba ni dini gani?

chadema kimeanzishwa kanisani kwenye kigango cha katoliki, kinaongozwa na padri alieasi na kupora mke wa mahimbo。viongozi wa chadema wote ni wakristo. viongozi waislamu zito na saidi arfi wamefukuzwa kwa amri kutoka kwa mzee mtei. mzee mtei amesema hataki kuona muislamu anaongoza saccos yake
 
Hongera zake but kuna vyuo vingne kama Vya S.A.U.T si muhimu kuwa na viongozi(RAISI),kwani huwa hawana sauti,wanatekeleza majukumu yao kama baraza la maaskofu linavoamuru!
 
Siafadhali ni mwanasheria anayesomea saut,kuliko ww kilaza wa sheria ya MUCCOBS

Hahahah SAUT LL.B wanachukua vilaza ajabu nina rafiki yangu ana iii.17 yuko pale SAUT yaani hiki chuo cha SAUT kinadhalilisha kozi ya LL.B wanachukua wanafunzi vilaza sana yani uelewa wao ni mdogo sana kwenye SHERIA kuna siku nilikuwa MAHAKAMANI kulikuwa na wanafunzi wa SAUT LL.B (wahitimu) ,walikuwa wanajadili general defences against criminal liability walikuwa hawazijui kabisaaa duh nikajiuliza hili swali mbona rahisi sana? nikahisi kama wana certificate kumbe ni degree SAUT(LL.B) duh nikasema kweli SAUT ni chaka la vilaza
 
Siafadhali ni mwanasheria anayesomea saut,kuliko ww kilaza wa sheria ya MUCCOBS

Usibishane na wapambafu usije upambafu wao ukakujia...

Wenye akili timamu wanajadili changamoto za maisha na jinsi ya kukabiliana nazo poteza muda kutafuta fursa na si kwa mafunza yasiyo na athari yoyote kwako....
 
Hahahah SAUT LL.B wanachukua vilaza ajabu nina rafiki yangu ana iii.17 yuko pale SAUT yaani hiki chuo cha SAUT kinadhalilisha kozi ya LL.B wanachukua wanafunzi vilaza sana yani uelewa wao ni mdogo sana kwenye SHERIA kuna siku nilikuwa MAHAKAMANI kulikuwa na wanafunzi wa SAUT LL.B (wahitimu) ,walikuwa wanajadili general defences against criminal liability walikuwa hawazijui kabisaaa duh nikajiuliza hili swali mbona rahisi sana? nikahisi kama wana certificate kumbe ni degree SAUT(LL.B) duh nikasema kweli SAUT ni chaka la vilaza

Uwe unapenda kutumia sana kichwa cha juu kuliko cha chini kufikiri kabla hujacomment!!!!
 
WanaSAUT walihitaji rais bora wa kuwaongoza na si Mwalimu ama Mwanasheria,rais amepatikana apewe nafasi afanye yake
 
Hahahah SAUT LL.B wanachukua vilaza ajabu nina rafiki yangu ana iii.17 yuko pale SAUT yaani hiki chuo cha SAUT kinadhalilisha kozi ya LL.B wanachukua wanafunzi vilaza sana yani uelewa wao ni mdogo sana kwenye SHERIA kuna siku nilikuwa MAHAKAMANI kulikuwa na wanafunzi wa SAUT LL.B (wahitimu) ,walikuwa wanajadili general defences against criminal liability walikuwa hawazijui kabisaaa duh nikajiuliza hili swali mbona rahisi sana? nikahisi kama wana certificate kumbe ni degree SAUT(LL.B) duh nikasema kweli SAUT ni chaka la vilaza

Umemaliza Wewe Mnyero???????????????????????????????
 
chadema kimeanzishwa kanisani kwenye kigango cha katoliki, kinaongozwa na padri alieasi na kupora mke wa mahimbo

Umesahau kuwa mbowe ni lutheran...mtei lutheran...makani mwislamu....katoliki wapi apo??? Au slaa ndo mkuu wa chama
 
Back
Top Bottom