Wanabodi tuwe tunaweka kumbukumbu pamoja na kusoma "between the lines" anapoandika mtu uzi wake. Tuongeze uwezo wa kutafakari na kudadisi ili kupata faida kuepuka ramli.
Siku za hivi karibuni nikiandika uzi humu ndani nikieleza kuwa Urais wa Kassim Majaliwa unasukwa na SG wa CCM Dk. Bashiru Ally lakini bila baraka za Mkulu ambaye amekuja kustukia. Nikasema kwamba Bashiru ukomo wake ni 2022 kwenye Uchaguzi Mkuu ndani ya Chama wanapopanga safu za uongozi. Nikadhani nilieleweka.
Kifo cha Balozi John Kijazi kikaleta ahueni katika kummaliza kisiasa Bashiru. "Adui msogeze ubavuni". Kwa sasa Bashiru hawezi tena kufanya harakati za siasa za kumwandaa Majaliwa. JPM ana akili sana. Kamtoa kwenye reli pamoja na kwamba aliwahi kusema, "sitogombea nafasi yoyote wala kukubali uteuzi WOWOTE" baada ya huu Ukatibu Mkuu wangu'.
Kifupi ni kwamba vita ya Urais 2025 inarindima ndani ya CCM na Serikali. Mitandao inaundwa kwa gharama kubwa. Yetu macho!!