Zanzibar 2020 Urais Zanzibar: Kwanini nampa nafasi Mhandisi Hamad Yusuf Masauni

Zanzibar 2020 Urais Zanzibar: Kwanini nampa nafasi Mhandisi Hamad Yusuf Masauni

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Habari JF Siasa,

Humu ndani kumekuwa na maoni au chapuo mbalimbali juu ya wagombea Urais Zanzibar. Kuna mmoja wetu humu jukwaani amekuwa wazi kwa kuwapa chapuo Dr Hussein Mwinyi na Prof Makame Mbarawa.

Naomba nami niseme ama kutoa maoni yangu kutoka moyoni Kama walivyofanya wengine.

Kwanza kabisa, Hamad Yusuf Masauni ni Mhandisi ktk nyanja ya ujenzi. Uhandisi ni taaluma muhimu Sana ktk ujenzi wa jamii imara. Mfano wa majengo, umeme, barabara, Reli nk. Miundo mbinu hii ni muhimu ktk kukuza uchumi katika taifa lolote lile duniani. Huenda Masauni akawa mlevi au akapenda zaidi miundo mbinu mbalimbali na hivyo kuipaisha Zanzibar kiuchumi.

Pili, Mheshimiwa Masauni amehudumu ktk wizara ya mambo ya ndani ya JMT kwa miaka mitano licha ya mawaziri watatu kutumbuliwa. Yeye amekuwa Naibu waziri kwa kipindi chote hicho na huenda akawa anawafundisha kazi mawaziri wapya wajao wizarani.

Tatu, Hamad Y. Masauni ni mtiifu mkubwa kwa Rais Magufuli ambaye ni bosi wake Sasa na hata atakapokuwa Rais ajaye Zanzibar. Inasemekana Masauni anamheshimu na pia kumuogopa Sana Rais Magufuli na hivyo hii itakuwa afya njema kwa Muungano.

Nne, Naibu waziri Masauni ni Mbabe kiasi fulani ikizingatiwa siasa za Zanzibar hazimuhitaji mtu mpole Sana kwani wale kina Yakhee watamnasa kibao usoni. Hata Rais shein ni mpole lakini ni mkali Sana ofisini na ndiyo maana Zanzibar imesonga ktk utawala wake.

Tano, Masauni anatoka Unguja na hivyo ili kuimarisha mashirikiano ya dhati Zanzibar, ni vyema Rais kipindi hiki ataloke Unguja kwa kuwa wa Sasa anatoka Pemba.

Sita, Masauni Yusuf ni kijana buheri wa afya na hivyo atahimili mikiki ya siasa za Sasa ambazo zahitaji vijana huku wazee wakiwa washauri wakuu.

Saba, Masauni Yusuf hana nasaba na familia za viongozi wakubwa huko Zanzibar. Sahivi kuna kelele juu ya kiimarika siasa za usultani au ufalme visiwani Zanzibar. Watu wanadai wanadai kumekuwa na tabia za familia za Marais wa zamani Zanzibar kujiona wao Wana uwezo zaidi ya wanafamilia wengine Wazanzibari ya kuiongoza Zanzibar. Zipo pia familia za mawaziri hapo kale kutoa wagombea wenye ujivuni wa kuiweza Zanzibar na sio wanafamilia wengine. Masauni hana nasaba hizi na atazizima kelele zinazopigwa hivi Sasa na Wazanzibari walio wengi.

Rais ajaye Zanzibar ni Hamad Yusuf Masauni na Zanzibar itashuhudia mabadiliko makubwa Sana kimaendeleo. Naamini muda sio mrefu uzi huu utafufuliwa.
 
Ana kashfa ya kuingiza ndugu zake kwenye Jeshi la Polisi. Hata Rais alilizungumzia.
 
Umeshasema huyo kijana anamuogapa mwanaume mwenzake kupita kiasi mtu kama huyo hafai, pia hoja ya kusema kuwa ametoka Unguja ni hoja ya kipuuzi pia kwani kati ya marais Saba waliotawala Zanzibar sita tena mfululizo wametoka Unguja sasa leo kuna ubaya gani rais anayemfuatia Dr. Shein akitoka Pemba? Na kuhusu kuwa na nasaba na viongozi huyo kijana Baba yake amewahi kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar ambayo imekuwa ikilalamikiwa tokea mfumo wa vyama vingi uanze kwahiyo naye ni wale wale tu.
Mimi naona ni vyema Urais huko uende kwa kuzongati Pemba na Unguja ili kupunguza migongano. Ya kale kuwa walifululiza sita Unguja tuyaache.
 
Hao wote ni msafala wa mamba,lakini mwisho wa siku ni mtoto wa Raisi wa zamani Mzee mwinyi, kumbuka Mgombea anachaguliwa kutoka Tanganyika, na mzee mwinyi alishasema katiba ibadilike ili Raisi aliyepo atawale milele (siyo aongoze )
 
Masauni Bado Mhuni fulani awezi, aliwahi kudanganya umri awe Mwenyekiti wa vijana akaokolewa na JK
 
yakhe huyo huyo atufaa ati, wazenji tushikilie hapo! tusikubali machogo watuchagulie rais toka bara aje kutumia kanisa kutuongoza na kutumalizia mapembe yetu bure ati!
 
Umesema ni mhandisi wa majengo.Isijekuwa uhandisi wake ni wa kununua vyeti.Kwani mhandisi wa majengo hawezi kusema kuwa kuna watu wanakaa mapangoni kule Amboni Tanga.

Tena watu hao walikuwa wakali mpaka jeshi la nchi akalipeleka huko kupambana nao.Waliowahi kwenda huko wanasema mapango hayo hayana huduma hata mtu mmoja kujificha kutwa nzima bila kutoka akaingia kijijini kujikimu.

Vyenginevyo huyu Masauni ni mtu anayedanganywa kirahisi na mabeberu.Hawezi kuongoza nchi ya watu wanaotaka kuelekea mbele.
 
Back
Top Bottom