Urambo: Ajinyonga baada ya kuandamwa na sauti zilizomtaka ajiue kwa muda mrefu

Urambo: Ajinyonga baada ya kuandamwa na sauti zilizomtaka ajiue kwa muda mrefu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Emmanuel Kasapa (60) Mkazi wa Mtaa wa Legezamwendo, Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora amejiua kwa kujinyonga baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na sauti za watu zikimwamuru ajiue.

Watoto wa marehemu wamesema baba yao amejaribu kujiua mara kadhaa akilalamika kusikia sauti za watu asizozielewa zikimuamuru ajiue.

Kaimu Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kariakoo, Fredrick Itogoza amesema marehemu alijaribu kujiua kwa sumu miezi mitatu iliyopita.

Chanzo: Cgfmradio
 
Watu wengi sana naimani wanasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia.
 
Maskini alipatwa na tatizo la afya ya akili. Angewahishwa Mirembe (au labda hospitali ya mkoa) angepewa tiba.

Ndugu wasipuuzie mtu anapojieleza na kutenda kama huyu.
 
Halafu kuna wapumbavu walitunga sheria kuwa kujiua/kujaribu kujiua ni kosa kisheria!!!
 
Nilishawahi pitia hili,kitu kilichokuwa kinanishangaza Ni kwamba sikuwa na matatizo makubwa ya kimaisha kiasi Cha kujiua.siku moja nilikuwa kwenye bodaboda umbali mrefu nikawa nasikia sauti 'ruka'.
Nilikuwa naona Ni ujinga,Sasa kama ilikuwa ndo matatizo ya saikolojia au ndo majini yatajua yenyewe Mimi siwezi jiua kwa upuuzi wowote ule.
 
Back
Top Bottom