Hivi umefika Nyumbu, Kibaha au unasimuliwa? Pamoja na kuwa well-intended, mradi wa nyumbu ni failure. Wametengeneza APC ( sidhani kama wametengeneza Tank),gari la zima moto na maarufu zaidi lile lilotumika kuubeba mwili wa Mwalimu (RIP). Baada ya kuona matatizo ndiyo maana wakaelekeza kwenye biashara ya dhahabu na sisi hii tunayosikia ya bio-gas (ambayo carmatec wamejihusisha kwa miaka mingi). Ukiangalia critically, hatuna military industry ya kuweza kusustain mradi kama huu. Wenzetu (wamarekani, warusi, waafrika kusini n.k) wanategemea mauzo ya nje ya bidhaa zao kusustain industry zao. Wengine unaowasikia (India, China n.k.) walianza kubuild under licence. Hakuna mtu anayejisumbua kugundua gurudumu. Sasa sisi tumeshindwa kutengeneza baiskeli( Mwenge) tungeuweza kweli huu mradi?
Sasa unachotaka kutuambia kuwa tukitaka kutengeneza DVD na sisi tuanze from scratch? Au twende kwa hao wenye hiyo teknoloji na tuitumie?
Hivi kwa sababu tuna vijana wana uwezo wa kuassemble kompyutas na sisi tujione magwiji kwenye hii industry? Sera ya kupinga na kuzuia TVs na Kompyuta ilikuwa based kwenye uwezo wa watu kununua na siyo kama tunaviweza kiteknoloji. Sasa vipo, vimeruhusiwa na vimejaa bwelele tuko wapi kwenye kuelekea kuviunda pale nyumbani?
Again, unaspin. Unataka kuniambia seriously kuwa hatuhitaji maabara katika shule zetu za sekondari? Hao physicists unaowataka watatokea wapi? Unarudia makosa yaleyale tuliyoyafanya kusisitiza kuwa Kiswahili na Siasa ndiyo basis ya elimu yetu. Tunahitaji maabara ili vijana waanze mazoea ya kutafiti. Haitoshi kugugl peke yake. Wahindi, wapakistani na wengine wali invest kwenye basic education kwanza. Hawakuanza na nuclear physics primary school. Mfundishe mwanafunzi kupenda elimu, kumdadisi na mchunguzi na mengine yatafuata.
Tanzania ina kitengo cha masuala ya atomic. Tanzania ina physicists wazuri tuu. Hawa wote wanaweza kuelekeza nguvu zao kwenye hiki unachokitaka. Reality, however, ni kuwa kama tutahitaji tutanunua utaalam kutoka wenye nao na hatuta anza kwenye basics. Wairan imebidi wafanye hivyo kwa sababu soko limefungwa kwao. Tusikazanie hii mind-set ya kupenda SUVs wakati uwezo wetu ni baiskeli, kusafiri First Class wakati uwezo wetu ni kwenda economy. Tupange priorities zetu na yote haya tutayapata. Sio kesho lakini hatimaye tutayapata. Kwa kuzania huku unakotaka tunapunguza resources kwenye sehemu zenye umuhimu zaidi. Na mwisho, sidhani ulikuwa serious kwenye jibu lako kuhusu Calories. Au ulikuwa?
Nyumbu nimepita lakini kuna washikaji kutoka Mchundo walifanya kazi pale. Hivyo stori nyingi ninazo. Hata Nyumbu nao walifanya kama walivyofanya wengine watu wengine (under licence). Injini za mwanzo zilikuwa kutoka ujerumani mashariki kama sikosehi. Hawakufanya vitu vyote kutoka mwanzo.
Failure ya Nyumbu haitokani na matatizo ya kiufundi. Inatokana na Business Model waliyofuata, ndio maana naupenda UBEPARI. Kwa bahati nzuri nimeishi nchi za Ulaya mashariki. Na matatizo yaliyoikumba Nyumbu ni matatizo yaliovikumba viwanda vingi katika nchi za Ulaya mashariki.
Nyumbu haikuwa na Business Model yoyote hili. Misheni yao ilikuwa ni kutengeneza magari na vifaru na waliweza kufanya hivyo. Na hawakuwa na misheni ya kutengeneza gari na vifaru vya kuuza. Unapotoa maamuzi ya kutengeneza kitu kwa ajili ya kuuza, unaangalia masoko kwanza.
Katika university ranking, wa-marekani wanaongoza vizuri sana katika masuala ya Business Admin. Financial na Marketing. Technologia yoyote haiwezi kuuzwa na kuleta faida kama haitakuwa na watu wazuri wenye Acumen ya Business Admin. Financial na Marketing.
Hata kama Tanzania ina physicists, engineers wazuri lakini wakakosekana watu wazuri wenye ujuzi mzuri katika Business Admin. Financial na Marketing, ambao wanaweza ku-glue kile physicists na engineers wanachoweza kukifanya hakutakuwa na maendeleo yoyote.
Kama nitakuwa sijavuka mipaka na kuingilia taaluma za watu wengine, VALUE ni thamani ya kitu ambacho mteja yupo tayari kulipa. Hivyo unapofanya biashara ya aina yoyote nia yako kuweka VALUE ya huduma au vitu unavyoouza inayoweza kuwafanya wateja wanunue. Kwa mtaji huu nchi ulizotaja (wamarekani, warusi, waafrika kusini n.k) hawategemei mauzo ya nje ya bidhaa zao kusustain industry zao. Wanachotegemea ni VALUE gani iliyopo katika bidhaa zao itakayomfanya mteja kununua bidhaa hizo. Wateja wa nje wana-choice ya kununua bidhaa kutoka nchi mbalimbali. Lakini factor wanazoangalia wateja ni bei, ubora, support n.k.
Tukurudi kwenye mada, NYUKI ya Iran imeanza toka Shah akiwa madarakani. Wa-iran wa utaifa kuzidi udini. Hivyo program za taifa bado zinaendelea japokuwa madaraka yamebadilika.
Wako katika ujenzi wa taifa.
BM