Uranium Mining Projects In Tanzania: Progress...

Fundi Mchundo:

Kwa uzoefu wangu na kwa bahati yangu niliyopata ya kufanya kazi kwenye
mashirika ya kiufundi, nina amini kabisa kwamba maendeleo mengi ya kiteknologia
na sayansi yakwamishwa sana na masuala ya kisiasa na bajeti na sio ukosefu wa vichwa.

Kwa mfano viwanda vifuatavyo vingejengwa karibu ya machimbo ya chuma na makaa mawe
au kwenye ukanda wa reli ya Tazara, je Tanzania ingekuwa wapi?
-Nyumbu
-Mang'ula
-Ufi
-Kilimanjaro Machine tools

Nchi inayoongoza katika masuala ya NYUKI za umeme ni Ufaransa. Na hii inatokana
na sera zao walizifanya baada ya matatizo ya mafuta katika miaka ya 70.

Denmark na nchi zingine za Scandinavia, zimeendelea sana katika alternative energy
sio kwa sababu wanapenda au kwa sababu ni bei rahisi. Wanafanya hivyo kwa sababu sera
za nchi zao zinafanya hivyo. Na sera ikibadilika vichwa vinavyotengeneza alternative
energy ndio zitavyotumika kwa NYUKI au nguvu nyingine.

Na hakuna mtu anayeng'ang'ania Tanzania kuwa NYUKI katika kipindi cha sasa lakini kuna
umuhimu mkubwa wa watu kuanza kujifunza NYUKi kwa sababu sayansi yake haiishii katika
masuala ya masuala ya silaha au umeme.

NYUKI tech ina matumizi mengi. Watu wanatumia katika mambo ya medicine, forensic
analysis n.k.

Nchi zinazoongoza kwenye alternative energy hazikufunga milango katika research au
elimu ya NYUKI. Hawakufanya hivyo kwa sababu wanaelewa kabisa ufumbuzi wa matatizo
ya NYUKI utapatikana. Na utakapopatikana watakuwa katika nafasi nzuri kuitumia.

Masuala ya kuwa watanzania hawawezi kufanya vitu are pure prehistoric. Na hata
kama hawawezi kwa sababu za siasa au bajeti, milango isifungwe kwa wao kujifunza.
 
Mwanagenzi, nimeona Mkuu! Tofauti ni context. Wale ni waingereza na sisi ni watanzania. Mahitaji yao ya nishati ni makubwa mno na wanakokaa alternative nyingine ni haba. Sisi hatujafika huko na tunauwezo kabisa wa kukidhi mahitaji yetu kwa kutumia nishati mbadala. Kwa mazingira yetu nishati mbadala na kuongeza efficiency katika matumizi yetu makes more sense. Utaona hata waingereza hawataki kuingiza hata senti moja ya serikali katika mradi huu. Lakini kutokana na maendeleo yao na uwezo wao wa kusimamia vizuri mikataba, mashirika binafsi yanaweza kujitosa. Experience yetu ni kuwa hatuna uwezo huo ndiyo maana mpaka sasa wakina IPTL wanatuendesha.


Bin Maryam, Scandinavians wamewekeza zaidi kwenye nishati mbadala kutoka na concern zao kuhusu environment. Neno Sustainable Development lilipewa msukumo sana kutokana na ripoti iliyotayarishwa na kamati iliyoongozwa na aliyekuwa waziri mkuu wa Norway, Gro Harlem Brundtland mwaka 1987. Ripoti yenyewe iliitwa "Our Common Future". Toka wakati huo, sustainable development na impact ya matumizi ya nishati kwenye mazingira imekuwa mojawapo ya nguzo za sera za nchi hizi. Kitu kingine kilichochangia ni fall-out kutokana na Chernobyl disaster iliyotokea Ukraine mwaka 1986. Hii iliwafanya waangalie tena dependence yao kwenye matumizi ya Nyuklia. Kwa wakati huu, nadhani ni Finland peke yake ambayo inajenga kinu cha nyuklia katika nchi hizi. Hii inachangiwa kwa kiasi kikubwa na haja ya Finland kutaka kujitoa kuwa tegemezi wa vyanzo vya nishati, hasa kutoka Urusi. sera katika nchi hizi inasukumwa na utashi wa jamii na si otherwise. Hauwezi ukasema maamuzi yao yanatokana na sera na si kupenda kwao. Hii kwa kiingereza inaitwa Oxymoron.
 

Fundi Mchundo:

Sijuhi unataka kupinga nini? Naona unaanza kuleta mambo ya utashi, kupenda kwao na sera.
 
Bin Maryam.Nikikujibu tutarudi kulekule. Nadhani tumeliongea suala hili kiasi cha kutosha. Tukubaliane kutokukubaliana. Asante kwa mjadala mzuri na mawazo na mtazamo ulionipa changamoto kubwa. Shukrani.
 

Ndugu Wananchi !
Napenda kuwafahamisha kuwa kitu katika kitu kikubwa ambacho kilimleta Rais Bush hapa kwetu ni kutokana na Taarifa za kijasusi kunifikia mikononi mwangu ya kuwa ni katika kuja kuweka mambo sawa na Mkuu wetu wa Nchi namana safi ya kuchukua hazina yetu hiyo na kujiwekea mazingira bora zaidi ya namna atakavyo weza kushindana na Wazee wa far East ambao wao wameonyesha usugu wa kutomuogopa kwa lolote.

Lingine ni namna atakavyo jiwekea mazingira ya kuendelea kuchukua Hazina ya vito mbalimbali vya thamani pale Congo ya Kabila ndio maana alikwenda Rwanda na kujidai kujenga barabara za mipakani tu kama kule Rukwa na Ruvuma hana lolote na ule mpango wa reli ya kutoka Rwanda hadi Bongo Bandari ya salama ni weka !

Sasa mkae mkao wa kuliwa tu ! Poleni sana !
 

This is what i expected to hear...especially after G.W. Kichaka kutembelea Bongo na kukaa siku4!!!
Utaisikia mikataba yake inasiniwa hukooooo....NY!DC etc
 
Haya wala si news tena yalisemwa humu JF na nakumbuka ikasemwa tutakumbushana.
 

Fanya tena hiyo homework yako mkuu, Dunia inajua juu ya Uranium ya Tanzania toka 1978, siyo leo. Hebu soma http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2005/07/19/44790.html halafu uanze upya kutafuta taarifa zako za kijasusi juu ya Kichaka.
 
...but Tanzania, rich in uranium, seriously wants to go atomic

By WILFRED EDWIN
THE EAST AFRICAN
October 26 2008


The Tanzania government is considering using uranium as alternative source of energy for the country, which has been hard hit by power shortages.

Prof Peter Msolla, Minister for Communication, Science and Technology, said the country, which is a member of the International Atomic Energy Association, is embarking on a study to establish the possibility of peaceful use of nuclear energy for development.

Prof Msolla said his ministry and the Ministry of Energy and Minerals are working together on the use of uranium for power.

“Along with better availability of electricity, nuclear energy would be used for medical purposes in treating cancer in four major hospitals — Ocean Road Cancer Institute, Muhumbili National Hospital, Bugando Hospital and Kilimanjaro Christian Medical Centre,” he said.

Despite the fact that Tanzania is endowed with over 30 per cent of the total uranium deposits in Africa, the government appears not to know what to do with them.

The uranium was discovered many years ago, leading to the enactment of Atomic energy Act of 2003. But the deposits fall under the Ministry of Science and Technology.

Mohamed Habib Mnyaa, a Civic United Front member and an opposition spokesperson for the Ministry of Energy and Minerals, said recently during a parliament session in Dodoma that the Atomic Energy Act should be amended to place the uranium under the Ministry of Energy and Minerals.

Mr Mnyaa said the time had come for a feasibility study to be undertaken on uranium because of its economic importance worldwide.

Recent explorations by international companies indicate that the Mkuju river basin in the southern Tanzania has uranium deposits on 2000 square kilometres inside the Luwegu and Ruhuhu valleys. The Luwegu valley alone is estimated to have over 30 per cent of all known uranium deposits in Africa.

Between 1978 and 1982, a German company, Uranerzbergbau Gmbh, undertook a reconnaissance exploration that revealed a huge deposit of the mineral in Makutupora area in Dodoma.

It also found that Tanzania had among the lowest costs of uranium exploration in the world, estimated at the time to be at $4 per square kilometre, compared with $16 in West Africa and $244 in the US.

Lawrence Masha, Deputy Minister for Energy and Minerals, said that despite the fact that nuclear technology is sophisticated, what hinders its application in Tanzania is the low demand for electricity.

Mr Masha said a single nuclear plant is capable of producing a minimal of 5,000MW of power, while demand in a country like Tanzania, does not reach even 1,000MW at peak.

But critics say it is political rather than technological reasons that have held back uranium research in countries like Tanzania.
 
Umeme wenyewe umetushinda ku-manage na kuusambaza kwa idadi kubwa ya Watanzania. Hivi kweli tekinolojia ya nuclear tutaiweza?
 
Umeme wenyewe umetushinda ku-manage na kuusambaza kwa idadi kubwa ya Watanzania. Hivi kweli tekinolojia ya nuclear tutaiweza?

Sasa hivi kipaumbele kingetolewa kwenye umeme wa jua. Tuna jua la kutosha mwaka mzima itapunguza sana gharama za Watanzania katika matumizi ya umeme.
 
Ili kutumia "uranium as a source of energy"....utahitajika usaidizi kutoka nje "kiteknolojia" .....kwahiyo...kuna "Ulaji" hapo.....
 

Kwa maneno mengine hilo mashine la umeme la Uranium ukiliwasha umeliwasha, halina ku regulate power output, wala kusema ujenge mtambo mdogo mdogo, au ku u feed huo mtambo Uranium kidogo kidogo ili usitoe hizo 5000MW ambazo hazihitajiki. Au ?

Maana kihabari hakiko cohesive. Sijui kama ni mtoa habari (hao mawaziri wawili ) au mleta habari (waandishi), lakini mwanzoni inaonekana inasemwa kwamba tunahitaji umeme zaidi. Mwishoni kahabari kanasema Waziri kasema umeme wa Uranium ni mwingi kuliko tunavyohitaji. Well, sasa hivi kila anaetaka umeme Tanzania (demand) anapata ? Kama jibu ni hapana, basi tujenge huo mtambo tuu-feed Uranium aste aste. Haiwezekani ? Kwa nini ?

Na kama mnatuambia mtambo wa Uranium ukishauwasha umeuwasha, yani scientifically haiwezekani ku moderate power output ya atomic energy plant, sasa wanacho explore cha zaidi hapa ni nini hasa, shimo la "kuzitupa" hizo extra 4000MW ? Maana si mmeshasema hatuhitaji that much power, and apparently huo mtambo ukiwashwa hauzimiki!!!

Na hizo political considerations mwandishi alizodokeza zinazozuia kuanzishwa kwa vyanzo hivyo vipya vya nishati ni zipi hizo? Zisipotajwa na kutuachiwa wasomaji tukatathmini maantiki zake inakuwa kama hadithi ya kidaku daku. Ya kutafuta mchawi. Yani huwezi kusoma taarifa ya chombo cha habari chochote Tanzania ukatoka unajua mawili matatu zaidi ya ulipoanza kusoma. Au kama mimi ndio sielewi, mtu anieleweshe hapo juu kinaelezwa nini hasa.
 
Handling ya uranium ni ngumu, achane wenyewe wajiume ila hakuna fisadi mwenye uwezo nao ndio maana hawana interest.

Jamaa wa kweli wakija hawataki mahusiano na ccm ndo maana wanaona hakuna maslahi. Hiki chama ni cha majambazi tuu
 
Hata kuwauzia nchi jirani inawezekana, lakini Bongo ndio hivyoo, viongozi wetu ni Blah blah tuuu.
 
Sounds good, a lot can be done if implemented correctly, including selling the excess power to the Southern African electricity pool.

But here in lies a problem: Hatuwezi hata kutunza mazingira yanayochafuliwa na takataka za ndani na viwandani mwetu sasa hii itakuwajekuwaje jinsi ya kuhandle nuclear waste?

Kwa mtazamo wangu wa harakaharaka, we already have the necessary tools in place to take care of our electricity needs:
1. Mvua za kutosha ili kujaza mabwawa yote ya kuzalisha maji. Chanzo cha mto Ruaha kimeweza kuzinduka na sasa kinatoa maji ya kutosha kushughulikia catchment area yote ya mabwawa makubwa Tanzania - Mtera, Kihansi, Kidatu

2. Gas ya Songosongo na Mnazi Bay. tumeanza kuuza hadi Kenya, viwanda fulani fulani in Dar vimeanza kutumia gesi hii, na miji ya Mtwara na Lindi wanapata umeme kwa kutumia gesi hii. Things are looking up!
3. Makaa ya mawe. Ukiacha mradi wa raisi mstaafu, Kiwira, kuna makaa ya mawe TZ hapa hakuna mfano. Viwanda vya kuzalisha umeme kwa makaa ya mawe vyawezekana vipo outdated lakini kwa kuongeza pesa kidogo kama 30% hivi inawezekana kujenga coal plants that are better on the environment than before.

4. Mengineyo - Upepo, Jua, bio gas, nk. Mmoja hapo juu amezungumzia umeme wa jua nao ni possible. Tusisahau wind power kwani kuna sehemu kibao za Tanzania kuna upepo sio mchezo, km between Mombo and Same, Chimala area in Mbeya/Iringa border etc. Ukipata nafasi ukiwa Tanga, mtafute jamaa mmoja anaitwa Shamte akuelezee jinsi mabaki ya katani yanaweza kuzalisha umeme wa kutosheleza mkoa wa Tanga, Kilimanjaro na Arusha, na pilot project imeshaanza na looks promising.

Tatizo ni jinsi ya ku-align solutions zote hizi ili ziweze kuleta maendeloeo yanayotakiwa. Penyewe hapo pagumu hapo, wee acha tuu! Ufisadi, incompetence, lack of thinking out of the box etc unatukwamisha sana hapa TZ!!
 
Ukaribu wa Rais wetu na Marekani unatokana na hii URANIUM?
 
Utafiti huu wa Uranium balaa tupu Tanzania!

Johnson Mbwambo Oktoba 29, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo


PAMOJA na kwamba nchi yetu imegeuka kuwa shamba la bibi kizee ambapo wawekezaji wa kigeni huja kuchuma, na kisha kuondokazao; lakini uwekezaji unapogusa suala la usalama wa afya za wanavijiji wetu wasio na hatia; bado baadhi yetu tunashawishika kuhoji busara za watawala wetu.

Nazungumzia hatua ya serikali kuruhusu makampuni ya kigeni kufanya utafiti (exploration) wa madini ya Uranium nchini, kwa madhumuni ya kuruhusu baadaye uchimbaji wake.

Ni kweli kwamba mwisho wa yote zitapatikana ajira chache migodini, ni kweli pia kwamba dunia inahitaji madini ya Uranium kwa ajili ya kutengeneza nishati na silaha, lakini pia ni kweli kuwa uchimbaji wa madini hayo ni hatari kwa wachimbaji wenyewe, na kwa wananchi wa maeneo ya karibu; kuliko uchimbaji wa madini mengine yoyote.

Kwa yeyote anayefahamu, japo kidogo, unyeti wa Uranium na hatari ya mabaki yake (residual) kwa afya ya binadamu, atakubaliana nami kwamba haya ni madini ambayo pengine tunapaswa kuyaacha yaendelee kukaa ‘kwa amani’ chini ya ardhi yetu! Angalau kwa sasa.

Nasema hivyo kwa sababu, si tu kwamba Uranium ndiyo madini yanayotumika kutengeneza silaha za nyuklia, na tusingependa kujihusisha na uchimbaji wa madini hatari kiasi hicho, lakini pia mabaki yake yasipodhibitiwa vyema husababisha kansa za aina mbalimbali kwa watu wanaoishi karibu na maeneo hayo. Vumbi la mabaki ya Uranium likipeperushwa na upepo na kisha watu wakavuta hewa yenye vumbi hilo, uwezekano wa kupata kansa ni mkubwa mno.

Kwa hiyo ni muhimu mno mabaki ya Uranium migodini yakadhibitiwa kwa utaalamu na teknolojia ya kisasa; kwani tafiti zinaonyesha kwamba mabaki hayo hubaki na hatari hiyo kwa zaidi ya miaka bilioni 4!

Waliopata kutembelea mji wa Halle wa Ujerumani watakuwa wanafahamu ni kiasi gani serikali ya nchi hiyo inahangaika kuhakikisha inayadhibiti vyema mabaki ya Uranium katika machimbo yaliyoachwa na Warusi enzi ambapo mji huo ulikuwa ni sehemu ya Ujerumani Mashariki (GDR) iliyokuwa rafiki mkubwa wa Urusi.

Eneo la machimbo hayo, nje kidogo ya mji wa Halle, limetengwa kabisa kwa kuwa ni hatari kwa wananchi kupita karibu na hapo. Aidha, Serikali ya Ujerumani hutumia mabilioni ya pesa kudhibiti mabaki ya Uranium katika machimbo hayo ili kuepusha wananchi wasiathirike na radiation.

Na itabidi udhibiti huo ambao ni ghali uendelee kwa miaka nenda rudi; kwani, kama nilivyosema mwanzo, mabaki hayo huendelea kuwa hatari kwa miaka zaidi ya bilioni nne!

Lakini pia wanaopenda kufuatilia habari za uchimbaji wa Uranium sehemu mbalimbali duniani watakuwa wanaufahamu mkasa uliowakumba waliokuwa wafanyakazi wa Mgodi wa Uranium wa Arizona nchini Marekani. Kati ya wafanyakazi 1,500 wa mgodi huo, tayari wafanyakazi 1,112 wameathirika kwa kupata kansa na wamefungua kesi mahakamani kudai fidia. Wale ambao tayari wameshafariki, watoto wao au ndugu zao wanaendelea na kesi hizo.

Nimetoa mifano miwili tu ya balaa lililoletwa na uchimbaji Uranium katika nchi mbili kubwa na tajiri duniani – Ujerumani na Marekani; lakini ukweli ni kwamba ipo mifano mingine mingi tu sehemu mbalimbali duniani.

Jambo la kukumbuka, hata hivyo, ni kwamba Marekani na Ujerumani ni nchi tajiri zenye wanasayansi waliobobea na asasi zenye nguvu na teknolojia ya kisasa ya kuyadhibiti mabaki ya Uranium; je kwa nchi masikini za Dunia ya Tatu kama Tanzania?

Ndiyo maana ninashangaa kwamba pamoja na hatari yote hiyo, Tanzania tumejitosa kichwakichwa katika kukaribisha makampuni ya kigeni kufanya utafiti wa madini hayo, kwa lengo la kuruhusu kuanzwa kwa uchimbaji rasmi .

Kwa mujibu wa tovuti ya Marketwire: press release distribution, newswire, public relations, investor relations, breaking news, media monitoring , kuna makampuni karibu 20 ya kigeni ambayo, hivi sasa, yanafanya utafiti wa Uranium katika Tanzania; hususan maeneo ya Kati na Kusini.

Kwa hakika, makampuni manne kutoka Australia na Canada ya Uranex, International Gold Mining Ltd, Mantra Resources Ltd na Atomic Research Ltd, yamefikia hatua ya mbali katika utafiti wao huo nchini; kiasi kwamba baadhi yameshaanza kusaka mitaji mikubwa kwao kwa ajili ya uchimbaji rasmi!

Baadhi ya maeneo ambayo utafiti huo unafanyika na ambayo, kama udhibiti wa hali ya juu hautafanyika, wananchi wanaweza kudhurika katika kipindi hiki cha utafiti, na hata baadaye uchimbaji kamili utakapoanza, ni Wilaya za Bahi mkoani Dodoma na Tunduru mkoani Ruvuma.

Habari kutoka wilayani Bahi, kwa mfano, zinasema kwamba baadhi ya utafiti huo wa awali unafanywa karibu na mito na vyanzo vya maji. Kama uchimbaji wa majaribio unaofanyika huko ni ule wa kitaalamu zaidi unaojulikana kama in-situ, basi, hatari ni kubwa zaidi; kwani kemikali hutumika kutenganisha madini ya Uranium kutoka kwenye miamba au udongo.

Njia hii husababisha uchafuzi wa mazingira na maji; kwani mabaki ya kemikali huelekezwa kwenye vyanzo vya maji wakati mvua zinaponyesha; na hivyo uwezekano wa wananchi kupata radiation, na hatimaye kuugua kansa ni mkubwa.

Ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba uchimbaji wa Uranium unahitajhi umakini wa hali ya juu mno na uwepo wa asasi imara zinazoaminika za kufuatilia na kuhakiki usalama wa afya za wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya uchimbaji. Unahitaji wanasayansi waliobobea watakaokuwa wakipima mara kwa mara viwango vya radiation katika mashimo yaliyoachwa ya machimbo ya Uranium.

Sina hakika kwamba katika zama hizi ambapo ufisadi umekita mizizi kila sekta ya Tanzania, tuna sifa hizo au utashi wa kuhalalisha kujitosa katika uchimbaji wa madini hayo hatari.

Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba ufisadi na kiwewe chetu cha kutafuta pesa za wawekezaji wa kigeni kitatusukuma kutoa, hivi karibuni, vibali vya uchimbaji rasmi wa Uranium katika maeneo hayo; bila kuzingatia usalama wa afya za wananchi wetu.

Mwisho wa yote ni kwamba wageni hao watakuja, watachimba Uranium, watatengeneza mapesa yao, na kuondoka zao; huku wakituachia, si tu mashimo makubwa; lakini pia wanavijiji watakaougua kansa miaka michache baadaye na watakaoathirika na radiation!

Kwa mtazamo wangu, hatupaswi kuwa na haraka ya kuwakaribisha wageni kuchimba madini hayo ya Uranium ambayo ni ya hatari kweli kweli kwa afya za watu wetu. Mungu ameijalia nchi yetu kwa kuipa ardhi na miamba yenye madini mengi tu ya thamani yasiyo na hatari kubwa kama Uranium.

Kwa sasa tuelekeze nguvu zetu katika madini hayo yasiyo na hatari kubwa. Tuachane na Uranium yanayotengeneza silaha za nyuklia; madini ambayo wala hayawezi kutuondoa katika umasikini; kwani ingekuwa hivyo, nchi ya Niger isingekuwa miongoni mwa nchi zenye umasikini wa kutupwa barani Afrika.

Ni wajibu wetu sote kuwalinda Wasandawi wa Bahi na Wayao wa Tunduru dhidi ya hatari ya kupata kansa endapo migodi ya Uranium itaanzishwa kishaghalabaghala katika wilaya hizo.

Tafakari!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…