Mi najiuliza hii serikali ya chama cha mapinduzi ipo kutesa watanzania mbona imekaa kishetani haitapendi kuona kabisa watanzania wakiishi vizuri. Kulikuwa kuna haja gania ya kuvunja mifuko iliyokuwepo na kuunda mfuko moja wa PSSSF? Huu mfuko umekaa kishetani. Kulipokuwa na mifuko ya PPF, GEPF, PSPF na LAPF mambo ya mafao yalikuwa mazuri hasa mfuko wa LAPF ulikuwa unalipwa ndani ya mwezi moja. PSSSF ni mateso na majanga unakaa mwaka au miaka hakuna kulipwa. Jamani zile si pesa zetu tulizideposit? kwanini kuzi-draw inakuwa nongwa?