Urasimu, uzembe vinaongoza kukwamisha miradi mbalimbali ya Serikali

Urasimu, uzembe vinaongoza kukwamisha miradi mbalimbali ya Serikali

Joined
Apr 1, 2017
Posts
16
Reaction score
28
kijichi.png

Kutoendelezwa kwa miradi mbalimbali jijini Dar es Salaam, iliyogharimu mabilioni ya fedha za umma kumetajwa kuwa ni ufujaji wa fedha hizo.

Mwandishi wa habari hizi ametembelea baadhi ya miradi ya vyoo katika Halmashauri ya Kigamboni, Ilala, Temeke, Kinondoni, na Ubungo.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), kwa ufadhili wa benki ya dunia (WB), imejenga vyoo 30 katika Halmashauri zote jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuboresha hali ya usafi wa mazingira katika maeneo yenye msongamano wa watu hususani katika masoko, maeneo ya umma na vituo vya daladala.

Vyoo hivyo vimejengwa katika Wilaya ya Kigamboni vyoo vitano katika maeneo ya Kibada, Geza Kituo cha Mabasi, Buyuni, Tundwi Songani na Geza soko la mazao.

Wilaya ya Temeke vilijengwa vyoo sita katika maeneo ya Toangoma, Tandika Sokoni, Mbagala Kampochea na Mbagala Stendi, Sulele Mbande.

Wilaya ya Ilala vyoo vilijengwa vyoo sita katika maeneo ya Chanika Videte, Kimanga Kituo cha Mabasi, Kipunguni Sokoni, Kigogo fresh, Posta ya zamani na Chanika Zingiziwa.

Katika Wila ya Kinondoni, vyoo saba vilijengwa katika maeneo ya Coco Beach, Mwananyamala, Mwanamboka, Bunju Sokoni, Bunju Stand, Magomeni Gardeni, Mbweni Mpiji Sokoni.

Wilaya ya Ubungo vilijengwa vyoo sita maeneo ya Shekilango Sokoni, Mawasiliano Sokoni, Mabibo External, Mloganzila Kituo cha Magari, Manzese Sokoni na Mbezi Luis.

Hata hivyo, licha ya vyoo hivyo vilivyojengwa na mkandarasi Helpdesk Engineering Tanzania Limiteda kukamilika tangu mwanzoni mwa 2025. Uchunguzi wa mwandishi umebaini ni vyoo visivyozidi vitano ndivyo vinavyotumika .


Kwa mfano, choo kilichopo eneo la Mwanamboka Kinondoni Manyanya, kimekamilika kwa Zaidi ya miezi sita, lakini hakitumiki.

Mwandishi wa habari hizi amebaini kuwa kabla kujengwa kwa choo hicho tayari kulikuwa na choo pembeni yake ambacho mpaka mradi huo unakamilika choo hicho cha mtu binafsi kinaendela kutumika.

Mwananchi anayeishi eneo hilo na ambaye hakutaka kutajwa jina lake, amehoji, “Mwandishi nikupe mfano hai hapa choo cha Mwanamboka pembeni ya choo kipya cha kisasa cha Dawasa kuna choo cha zamani hali yake sio nzuri, lakini wewe unadhani kwanini mpaka leo choo kile kinaendelea kutumika ni upigaji watu wanataka miradi yao iendelee.”

Mwandishi wa habari hizi ametembelea choo cha Mwananyamara Hospital, Magomeni Gardeni, Toangoma na Tandika Sokoni bado havijaanza kutumika.


Akizungumzia ucheleweshaji huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa DAWASA, Everlasting Lyaro akizungumza na Mwandishi wa habari hizi amesema kuwa miradi hiyo inasubiri kuingiwa kwa makubaliano ya uendeshaji kati yao na Halmashauri husika.

“Hiyo miradi ipo kwenye Halmashauri zote jijini Dar es Salaam imekamilika, lakini tunasubiri makubaliano na wenzetu wa Halmshauri, kwa hiyo hakuna urasimu kama inavyodaiwa,” amesema.


Video ya baadhi ya miradi iliyokwama



Stendi ya Mabasi ya Kusini ya Kijichi


Katika kwenye standi ya mabasi yanayokwenda mikoa ya kusini (Lindi na Mtwara na mkoa wa Pwani-Kusini), ameshuhudia eneo hilo likigeuzwa soko hakuna gari hata moja inayoingia au kutoka.



Mradi huo ulioanzaOktoba 17, 2022 uliogharimu kiasi cha shilingi 3.9 bilioni ikiwa sehemu ya mradi wa uendelezaji wa jiji la Dar es salaam (DMDP).

Sababu ya kujenga stendi hiyo ilikuwa ni kuondokana na msongamano wa magari katika stendi ya Mbagala Rangi Tatu ambayo pia ni mali ya mtu binafsi.

Hata hivyo, stendi hiyo ilikoma mwishoni mwa mwaka 2024 ikiwa imedumu kwa muda wa miaka miwili pekee.



Miongoni mwa waliopinga matumizi ya stendi hiyo ni Umoja wa Madereva wa Mabasi Kanda ya Kusini, waliosema barabara za kuingia stendi ni ndogo hali inayofanya magari kusubiriana kupishana.



Msemaji wa Wamiliki wa Mabasi yaendayo Mikoani (Taboa), Mustapha Mwalongo, amesema hawakushirikishwa katika ujenzi wa stendi ya Kijichi, bali waliiona ilipokamilika na kuelekezwa kupelekwa mabasi huko.



Amesema kwa muda mrefu wamekuwa hawashirikishwi kwenye masuala ya yanayowahusu, yakiwamo ya ujenzi na uhamishaji wa stendi.



“Nakumbuka kabla ya kuhamishwa stendi ya Ubungo na kupelekwa Mbezi, tulishauri isihamishwe badala yake iongezwe kwa nyuma kwa sababu kulikuwa na eneo kubwa, lengo ikiwa kuwarahisishia wananchi kupata huduma katikati ya mji, lakini tulipuuzwa.

“Ni kutokana na hilo unaona hivi sasa ofisi nyingi za mabasi zipo Shekilango jambo linaloifanya Serikali kuingia gharama ya kufanya ukaguzi stendi ya Magufuli na stendi ya Shekilango. Kama mawazo yetu yangezingatiwa yasingetokea haya leo,” amesema.

Akizungumzia stendi hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Jomary Satura amesema badala ya kuwa stendi ya mabasi ya mikoani, itakuwa stendi ndogo kwa ruti za magari ya ndani na wameamua kuweka vitu ambavyo vitashawishi watu kwenda huko, ikiwamo michezo ya watoto na maduka makubwa.

“Mwanzoni stendi ya Kijichi ilidhaniwa ingekuwa ni kituo kikubwa, lakini kwa sasa itabadilishwa matumizi.

“Ili kushawishi watu kwenda kule ni lazima uweke vitu vya kuvutia na moja ya mambo tunayoyafikiria kuyafanya ni kuweka michezo ya watoto. Mpaka sasa tunaendelea kukusanya mawazo kufanya uwekezaji ambao hautasababisha gharama, bali uwe na faida,” amesema.

Amesema walishawahi kupendekeza kuwe na stendi maeneo tofauti pembezoni mwa mji, yaani ya magari ya Nyanda za Juu Kusini ingekuwa Mbezi, mikoa ya Kaskazini Bunju na mikoa ya Kusini iliyopo Mbagala iboreshwe na kumlipa mmiliki fidia aiachie Serikali, lakini nayo yalipuuzwa.


Katibu wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa), Shifwaya Lema, amesema watendaji huwashirikisha wadau baada ya kujenga miradi, badala ya tangu kufanya hivyo awali ili watoe mawazo yao ya nini wangependa kifanye.

“Tulishaanza kupeleka magari kule lakini mwisho wa siku tulikuwa tukipata hasara, kwani mtu anaenda na abiria anarudi mtupu,” anasema.

Licha ya kusudio la kubadilishwa matumizi stendi ya Kijichi, anasema bado haoni kama yanaweza kuleta tija kwa kuwa mwisho wa siku daladala zitakwenda kubeba watoto, ambao hawatakuwepo kila siku.

Ameshauri ni vema kukawekwa soko la jumla akisema: “Wakiweka soko la jumla huku, mtu anayetoka Kigamboni, Mbagala Chamazi na maeneo mengine ya jirani hataona haja ya kuingia gharama ya kwenda Temeke Stereo au Tandika kwa kuwa anajua akifika Kijichi atapata kila kitu na baada ya hapo atapata usafiri wa daladala wa kumpeleka anapokwenda,” amesema.




Video inayoonesha Stendi na Soko la Kijichi ilivyotelekezwa



Septemba 16, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albart Chalamila, aliomba wananchi kutoa taarifa ya miradi iliyokwama.


“Natoa rai ukigundua mahala popote unapoona mradi wa serikali umekwama basi waniambie moja kwa moja ili tuweze kushughulike na baadhi ya watumishi wa serikali ambao kwa muda wote wanaona fedha ndio jambo zuri kuliko kukamilisha miradi ya Watanzania,” alisema.


View: https://www.youtube.com/watch?v=iaayRVT3wyE

Nawasilisha kama Changamoto kwa Mamlaka tukiwa ndio kwanza tumeuanza mwaka mpya na ndio tukiwa na viongozi wapya tukiamini kuwa wana ari mpya hawatachukulia habari hii kama ina lenga kuwabeza au kuwasuta badala yake watafikiri namna ambavyo miradi iliyofanywa bila utafiti ibadilishwe iwe fursa nyingine bila aidha kusibuniwe mradi mpya bila kuhakikisha kuwa ina maslahi ya muda mrefu kwa umma.
 

Attachments

  • Choo Mwananyamala.png
    Choo Mwananyamala.png
    1 MB · Views: 32
Yule aliejenga choo pale sehemu fulani karibu na kituo cha usafiri ambae ameruhusu abiria wajisaidie bure Mungu amuongezee sana, nilifika nikaambiwa hapa vipo vyoo vya kulipia ila ipo sehemu moja hapo kujisaidia haja zote ni bure na kuoga ni bure
 
kumbe hata vyoo tunajengewa na WB, very sad!
 
Back
Top Bottom