Urembo: Kabati limejaa na bado huoni nguo ya kuvaa

Urembo: Kabati limejaa na bado huoni nguo ya kuvaa

aaamuk

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2015
Posts
707
Reaction score
209
Walimbwende mpumzike siasa kidogo.

Hivi inakuwaje nguo ulinunua mwenyewe moja baada ya nyingine mpaka kabati likajaaa, halafu unapata tukio kama harusi unatoa nguo zote kabatini halafu bado huoni nguo ya kuvaaa.

Karibuni kwa michango.
 
Sio tu Harusi, hata siku za kawaida. Unashangaa mdada analalamika hana nguo, ukiangalia kabatini kwake zipo kibao na hakuna hata moja mbaya, sasa sijui huwa wanatakaga nini. Labda wanachoka baada ya kuzivaa kwa muda.

Ni bora wawe wana empty kabati kila baada ya muda na kuleta stock mpya ndani
 
Hamjui ni shida gani tunapata.......mnadhani kuona nguo ni rahisi eeeh.........asubuhi tunachelewa kazini kwa sababu nguo huwa hazionekani.........
Hapa najua hamtaelewa ila wanawake tutaelewana...........
 
Hilo nalenyewe ni jibu kiukweli ukitoka huko unakuja mikoba mdada ananikoba zaidi ya nane cjui hizo pesa wanatoaga wapi hawa viumbe nakumiwa sasa awavitumii nikuonyesha kuwa MNA maisha mazuri kuliko wanaume au kuliko wengine
 
Nguo ukiivaa mara 5 au 10 inakukifuu na mitumba kuutwa mabeli mapya yanazibuliwa iwe ya viatu,pochi,waleti,gauni,skati nk. Jamani kupendeza na kuonekana mpy rahaaa... sipendi mtu anizoee na kusema love more ... anavaaga hivi napenda ni waaaaoo daily
 
Huwa inatokea, mie mwenyewe leo hadi nimechelea kazini, kisa nguo ya kuaa
 
Hili jambo ni kwa wanawake wengi jamani mimi huwa nawaza nasimama kwenye kabati sioni kama unakuwa umezichoka nguo zako
 
My situation kabati limejaa sijui nivae nini kesho job,nguo zile zile unazichokaa na hapa nshaamua sinunui nguo for a while
 
Mie kwa mwezi napanga nguo mara 3 yani uwa nakosa kabisa nguo ya kuvaa namwaga zote chini nachagua moja baada ya nyingine na bado sipati........dah sijui tuna ugonjwa gani.
 
Hamjui ni shida gani tunapata.......mnadhani kuona nguo ni rahisi eeeh.........asubuhi tunachelewa kazini kwa sababu nguo huwa hazionekani.........
Hapa najua hamtaelewa ila wanawake tutaelewana...........
Hawawezi kukuelewa ila mimi nimekuelewa yaani ni shida! Mimi nikitaka kuwahi ibadani nguo huwa naandaa jumamosi
 
Hehehe!, hili jukwaa linatugusa wengi.

Hii ni common kwa w'wake wengi, 'jamani sioni nguo ya kuvaa' hata kama ana nguo za kumtosha miezi bila kurudia. 🙂
 
Back
Top Bottom