Urembo wa Picco na Henna

Jimena

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2015
Posts
25,935
Reaction score
96,056
Urembo huu ni moja kati ya mitindo yenye kupendeza na kuvutia.

Ni mtindo maarufu sana kwenye maeneo ya pwani hususani ni Tanga, Unguja, Pemba Dar es salaam na Mombasa, na hata kwenye maeneo mengine pia fashion hii ila nadhani wote tutakubaliana ya kuwa kwa hakika ukanda wa pwani ndio kiboko yao.

Mtindo huu hutumika pia kwa mabibi harusi na hata wahudhuriaji maharusini na kwenye sherehe zozote zile au kwa ajili ya kujipamba tu. Ikiwa utapata mchoraji mzuri basi kwa hakika utavutia.

Ruksa na wewe kutupia picha zako mbali mbali zinazoonyesha mtindo huu wa Picco kama nawe ni mpenzi wa mtindo huu.

 
Kwa sisi wenye rangi adhimu ya kiafrika huo urembo unatuhusu? coz naona picha ni za watu wenye rangi za mitume tu, nahisi mm nikipaka itabid wananchi watumie microscope kuona hyo michoro.
 
Kwa sisi wenye rangi adhimu ya kiafrika huo urembo unatuhusu? coz naona picha ni za watu wenye rangi za mitume tu, nahisi mm nikipaka itabid wananchi watumie microscope kuona hyo michoro.
Mi pia ni mweusi na wala sijawahi hata kufikiria kupaka picco sio kila fashion inatufaa watu wote lakini ngoja wadau waje tuone wanasemaje kuhusu hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…