Ureno kupeleka wanajeshi Msumbiji

Ureno kupeleka wanajeshi Msumbiji

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Ureno itapeleka wanajeshi nchini Msumbiji katika kipindi cha nusu ya mwanzo ya mwezi Aprili kufuatia shambulizi la wanamgambo wa itikadi kali lililofanywa dhidi ya mji wa Palma.

Screen-Shot-2021-03-31-at-10.13.20.png

Wanajeshi hao wa Ureno watakuwa na jukumu la kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Msumbiji kwa mujibu wa ripoti iliyotangazwa na shirika la habari la Lusa ambalo limenukuu chanzo kutoka wizara ya ulinzi.

Shirika hilo la habari la Ureno limesema makubaliano ya pande hizo mbili yanakamilishwa na kikosi maalum cha Ureno kitakuwa na wanajeshi 60 watakaopelekwa Msumbiji.

Mapigano kati ya magaidi wa kundi linalojiita dola la kiislamu na wanajeshi wa Msumbiji yameingia siku ya saba baada ya wapiganaji hao wa itikadi kali kuutwaa mji wa pwani wa kimkakati kaskazini mwa nchi hiyo.Mkurugenzi wa kampuni binafsi ya usalama,DAG, Max Dyck amesema mapigano yaliyoanza Jumatano wiki iliyopita bado yanaendelea.

Kadhalika duru zimearifu kwamba maelfu ya wakaazi wa Palma bado wamekwama katika mji huo wakiwa wamejificha wakihangaika kutafuta njia kuondoka kwenye mji huo unaoshikiliwa na wapiganaji hao.
 
Hao ISIS wanafugwa,dawa yao ni ndogo sana!Hakuna dawa nzuri nzuri kama airstrike kwa magaidi.Wale ISIS wa Syria na Iraq walipigwa airstrike wakapoteana!
Hata wakipigwa airstrike wakapoteana lakini hawajawahi kushindwa na kupotea.Hii ni kwa vile hiyo kitu ni danganya toto tu.
Elewa kuwa huko wameleta vurugu lisilokwisha sasa wanataka kuhamia jirani yetu na kugeuza uwanja wa vita kugombea kitu kidogo tu mafuta na gesi.
 
Hao ISIS wanawafuga,dawa yao ni ndogo sana!Hakuna dawa nzuri nzuri kama airstrike kwa magaidi.Wale ISIS wa Syria na Iraq walipigwa airstrike wakapoteana!
Sasa ndugu ufanya mashambulizi ya anga wakati unaambiwa wameshikilia mji, si utaua na raia
 
Kwa kweli inasikitisha sana kuona moja ya nchi ya afrika watu wanaleta vurugu na jeshi Lao linaonekana kushindwa lakini nchi zingine za afrika haziwezi saidia,
Wewe kwa kutumia akili yako unaamini Jeshi kamili ya Mozambique limeshindwa kukisambaratisha kikundi hicho? Ni kama Nigeria tu hao wanajeshi wao hugoma kwa kuogopa kufa.. ndio unadhani kuna nchi itakubali kupeleka jeshi lao? Kwa nchi yenye wanajeshi wasio wazalendo? Tunaona even Marekani sehemu nyingi hukodi wapiganaji kwenda front line na wao wakodi basi waache upumbavu uliopitiliza... waoneshe wao njia wasaidiwe...
 
Hao ISIS wanawafuga,dawa yao ni ndogo sana!Hakuna dawa nzuri nzuri kama airstrike kwa magaidi.Wale ISIS wa Syria na Iraq walipigwa airstrike wakapoteana!
Na kweli mkuu wale mnatafuta kipoli walicho jificha linatupwa bomu pale wanapoteana [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]sema wanawafuga tu.
 
Back
Top Bottom