Asilimia kubwa ya Watanzania hawaujui vizuri ugonjwa wa UTI. Kumekwepo na maelezo kutoka kwa watu mbali mbali na wakati mwingine hata kwa wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa huu lakini bado watu wengi wanakanganyika na ukweli halisi.Leo nitajaribu kutoa maelezo walau kwa kina ili jamii iujue ugonjwa huu kinagaubaga.
Kwanza kabisa kirefu cha cha herufi UTI ni URINARY TRACT INFECTION ikimaanisha maambukizi kwenye njia ya mkojo.
Msomaji anapaswa kujua njia ya mkojo ni ipi, inaanzia wapi na inaishia wapi. Kwa ujumla njia ya mkojo inaanzia kwenye mrija wa mkojo kwa mwanaume na mwanamke. Mrija huu unajulikana kama URETHRA na ukishapata maambukizi ugonjwa sehemu hii unaitwa URETHRITIS.Njia ya mkojo inayofuata baada ya urethra ni BLADDER yaani kibofu.
Kibofu kikipata maambukizi ugonjwa unajulikana kama CYCITITIS. Baada ya kibofu inafuata mirija miwili inayokwenda kwenye figo mbili. Mirija hii inaitwa URRETERS na ikishaambukizwa inajulikana kama URRETITIS.Na mwisho wa njia ya mkojo ni figo mbili yaani KIDNEYS na hizi figo zikishaambukizwa ugonjwa unajulikana kama NEPHRITIS.Sasa basi ni lazima tujue ni vimelea wa aina gani wanaoleta ugonjwa wa UTI.
Hapa nitajaribu kuonisha na kupanga vimelea katika makundi maalum.
Vimelea vinavyojulikana ni kama ifutavyo:
1. BACTERIA eg Streptococci, Staphylococci, E.Coli, H.Influenza, Proteus sp.Pseudomonas etc.
2. VIRUSES eg Clamydia tracomatis
3. FUNGI eg Candida albicans
4. TRICHOMONIASIS
5. SCHISTOSOMIASIS (kichocho)
6. PARASITES
7. GONORRHEA (kisonono).
Watoto wadogo mara nyingi wanapata UTI kutokana na kutobadilisha nepi kwa wakati na hivyo unyevu wa mikojo na mavi huvuta vimelea na kuleta maambukizi. Kwa watu wazima hasa wale wanaofanya ngono zembe wanapata magonjwa ya zinaaa kwa urahisi na hivyo wanakuwa tayari wana UTI. Kuna fikra kubwa imejengeka miongoni mwa jamii kuwa UTI inaletwa kwa urahisi kwenye vyoo vya kuchangia.
Dhana hii kwangu naweza kusema si sahihi hata kidogo kwa sababu wanaume wanakojoa kwa kuagiza mkojo kwa mbali kama risasi kwenye tundu la choo, sasa hao vimelea wanafuata mkondo wa mkojo kama unavyofanya umeme? Au wanaruka na kuja kuingia kwenye tundu la mkojo? Jibu ni hapana.Kwa wanawake wao wanajisaidia kwa kuchuchamaa, wakimaliza hawatoezi au hawasoteshi nyeti zao kwenye sinki au shimo la choo na wala vimelea vya magonjwa vilivyomo chooni haviambukizi kamwe kwa ya mvuke.
Dalili za UTI zinaonekana kulingana na aina ya maambukizi.Lakini dalili kuu kwa watoto na watu wazima zinafanana nazo ni maumivu wakati wa kukojoa na pengine kutoka uchafu au usaha kwenye njia ya mkojo. Kichocho dalili zake ni kukojoa damu na maumivu. Complications za UTI nazo ziko nyingi na zinategemeana na aina ya maambukizi. Matibabu nayo yako mengi na tofauti kulingana na aina ya maambukizi.