Ni vigumu sana kutofautisha UTI na STI iwapo tutachukulia mambo kiujumla jumla sana..lakini pia ni rahisi sana kama tutazingatia kanuni ya elimu ya utabibu(medicine)
Kuna njia mbili kuu za jinsi gani bakteria wa UTI wanavyoweza kufika eneo husika:
1. Kusambaa kwa njia ya damu(hematogenous spread) - hapa bakteria wanakuwa kwenye damu kisha wanaingia,kwa mfano ktk figo na kusababisha ugonjwa kwenye figo.
2. Ascending route - hapa bakteria wanatoka nje wanapandisha kupitia tundu la mkojo kuingia ndani..sasa hoja hapa ni jinsi gani wamefika pale kwenye tundu? Iwe ni mama amejisafisha vibaya na kuhamisha bakteria kutoka tundu la choo na kuwaacha mlangoni pa tundu la mkojo, au mtu mwenye mikono isiyo salama ameshika tundu la mkojo na kwaacha pale; au pengine ni uume wa mpenzi umezama kwenye chemba ya dawasco kisha kabla ya kuusafisha ukagusa tundu la mkojo la mama..yote yanawezekana.
Lakini jambo moja ambalo halina ubishi ni kwamba medicine imeweka wazi ni wadudu gani tunatakiwa kusema wanasababisha STI. Bila kujali kama wapo kwenye mfumo wa uzazi,au kwenye mfumo wa mkojo,au mdomoni na hata kwenye ngozi..popote utakapowakuta wanahesabiwa ni STI..na hapa lazima tuwekane sawa,sio kila mwenye STI ameipata kupitia kujamiiana..kwa mfano ukiongezwa damu yenye kaswende,utaugua kaswende (STI) bila kujali kama ulijamiiana.
Lakini pia Medicine haikusahau kutaja wadudu gani wanasababisha UTI..sasa tofauti ndogo iliyopo kati ya UTI na STI ni kwamba,ili ugonjwa uitwe UTI ni lazima wadudu wanaosababisha wakutwe kwenye mfumo wa mkojo.. huwezi kukuta E.coli kwenye damu ukasema hiyo ni UTI, wala usiwakute kwenye uke wa mama ukasema hiyo ni UTI, hapana..
Sasa urethritis imesumbua hapo juu kwamba ni UTI au STI? Kama nilivyotangulia kusema,STI itabaki kuwa STI bila kujali wapi umeikuta au imepatkanaje..medicine inasema neno urethritis linatumika kumaanisha STI; imegawanya urethritis ktk makundi mawili:
1. Gonococcal urethritis - hii inasababishwa na na wadudu wa gonoria
2. Non-gonococcal urethritis - hii inasababishwa na wadudu wote ambao si wa gonoria,lakini wanaohesabika ktk kundi la wale wanaosababisha STI.
Kwa hiyo kusema kiujumla jumla kwamba urethritis ni UTI eti kwa sababu tu kwamba kilichoathirika ni mfumo wa mkojo,si sahihi.
Sasa je kujamiiana kunaweza kusababisha UTI? Jibu litategemeana wewe unaelewa vipi tafsiri ya magonjwa ya kujamiiana (STI) ila kama tutazingatia tafsiri ya STI kwa maana ya wadudu wanaosababisha, jibu litakuwa HAPANA kwa kuwa STI itabaki kuwa STI tu regardless umeikuta wapi,hata kama ndani ya kibofu cha mkojo,bado itabaki kuitwa STI na si UTI. Ila kama kila kinachopatikana ndani ya mfumo wa mkojo ni UTI,basi hata gonociccal urethritis ni UTI..kwa maana hiyo,jibu litakuwa NDIO kujamiiana kunasababisha UTI.
Vipi,tunapomtibu mgonjwa wa UTI lazima na mwenzie atibiwe?
Jibu nalo ni kama hapo juu..inategemeana uelewa wako juu ya STI..mgonjwa mwenye STI sharti aje na mwenzie watibiwe..kwa hiyo kama STI ipo ndani ya mfumo wa mkojo, lazima atibiwe na mwenzie..kwa mfano ikiwa ana gonococcal au non-gonococcal urethritis ni lazima atatibiwa na mwenzake..lakini tiba ni kwa sababu ana STI na si kwa sababu ya UTI! Ila kama kila kinachopatikana ndani ya mkojo ni UTI basi NDIYO atatibiwa pamoja na mwenzake kwa kuwa ana UTI!
My take:
1. Kujamiiana hakusababishi UTI,kwa maana kwamba mwanaume amkojolee mwanamke majimaji yenye wadudu kama ilivyo kwa gonoria..au labda maambukizi kupitia michubuko kama ilivyo kwa kaswende au HIV..ila kujamiiana ni tabia hatarishi(risk factor) hasa kwa wale wanaofanya anal sex kwa maana ya uwezekano wa kuhamisha wadudu kutoka tundu la nyuma na kuwaweka ktk tundu la mkojo la mwanamke au kile kitendo tu kuingiza uume ndani ya chemba ya dawasco wadudu wanaweza kuingia moja kwa moja ndani ya mfumo wa mkojo wa mwanaume..na hapa kiukweli tutasema sex imeleta balaa!
2. Ikiwa sex itafanyika ktk mazingira ya usafi na kufuata utaratibu wa kawaida yaani uume-uke,si rahisi kuambukizwa UTI..kumbuka hii ni tofauti kwa STI,ambapo bila kujali partner yuko safi kiasi gani,bila kinga mathubuti lazima utaambukizwa,gono,syphilis HIV etc.ili mradi tu umesex na mtu mwenye ugonjwa.
3. Tunaposema unaweza kupata UTI kwa kusex na mwenye ugonjwa huo maana yake ni kwamba kwa mfano,mwanaume apate maabukizi wakati wakati akifanya tendo na mwanamke mwenye UTI iwe ni kwenye kibofu cha mkojo au figo za mama! Au mwanaume mwenye UTI amwambukize mwenzie kupitia maji maji ya shahawa zake au kupitia michubuko? Kwa kufanya hivyo ndipo tafsiri sahihi ya maambukizi ya UTI kwa njia ya ngono inavyopatikana..lakini je inawezejana kweli kupitia njia hizo?
Sasa kupitia anal sex maambukizi ni wazi yanawezekana..ila je,kumtibu mgonjwa na mwenzi wake ina maana yoyote kisayansi?
Kumbuka wadudu karibu ya wote wanaosababisha UTI wanapatikana kwenye mtumbo yetu bila kusababisha tatizo lolote(normal flora). Sasa fikiria mwanaume ameruka ukuta amevunjika mguu,mkewe mzima wa afya,can someone please tell me, sababu ya kumtibu mkewe ni nini? Au,kuwatibu wote,kisha baadaye usiku wakagonga lisilochacha,imewasaidia nini?
Mtaani hiki kitu kinachoitwa UTI kimekuwa fashion.. mara utasikia UTI sugu,kila ukipima unaambiwa una UTI na mbwembwe nyingine nyiiingi..jamani,sio kila mara tunakuwa tunaumwa UTI.. lakini pia lazima tukubali kwamba hata tumesababisha wenyewe..kama jamii tumefika mahali,mtu ukipimwa maabara ukaambiwa ugonjwa haujaonekana,unaondoka umenuna ile mbaya..utasikia "ah,dokta fulani, hovyo sana,ameshindwaje kuona ugonjwa?" Kwani lazima kila ukipima ukutwe unaumwa? Au kuwa na ugonjwa ni sifa? Ndio maana wajasiriamali wanachangamkia fursa,kila ukipima tu,lazima tukute UTI,typhoid na malaria 7+..unapigwa hela hapo kisha unaondoka umefurahi kweli kweli..kumbe hata pengine majibu halisi ni negative achilia mbali kwamba pengine hata vipimo vyenyewe havikufanyika kabisa! na je,tunaamini vipi vipimo hivi na uwezo wa wapimaji wake? Au sisi tunajisifia tu mitaani na maUTI yetu sugu bila kuzingatia maswala mengine ya msingi?!