Niseme tu kwamba kwa Tanzania 90% ya watu wanaopimwa na kuambiwa wana UTI, hawana maradhi hayo.
Ni vizuri vipimo vya UTI vifanywe kwa ufasaha ili kuepusha watu kutumia dawa ambazo hazikuhitajika
Vituo vingi vya afya vinapima UTI kwa kuangalia wingi wa epithelia cells katika mkojo. Hii si sahihi.
Njia ya kuotesha mkojo ndiyo sahihi na hasa ikifanywa kwa umakini kuanzia kusafisha (disinfect) kiungo chenyewe, aina ya mkojo-first, mid, or last stream, chupa yenyewe iwe sterilized, ujuzi wa mtaalamu wa maabara, vitendea kazi na vitendanishi.
Mgonjwa apimwe kwa siku tatu mfulilizo
Hivyo uoteshaji utaonyesha kama kuna bacteria au fungi kwenye mkojo
Antibiogram itaonyesha ni contaminant au pathogen
Kama ni pathogen itaonyesha dawa gani inafaa kuitibu