busy bees
JF-Expert Member
- Aug 26, 2016
- 2,249
- 1,340
- Thread starter
- #61
Hakika ninazidi kuelimika kotekote chanzo na tiba/suluhisho ....Imeshamiri sana kutokana na kuto kunywa maji mengi, kushea ndoo na kopo hasa kwa vyoo vyetu vya uswazi, pili wanawake wengine kupenda kujifucha kunako na kujisafisha ndani kwa sabuni zenye kemikali hii hufanya kuuwa bakteria wazuri wanaokinga na maradhi,
Na kutokana na umasikini tuliokuwa nao vyoo vya shimo ndio bomu kabisa kutokana na maumbile ya mwanamke alivyo na choo chenyewe kilivyo halafu aende achutame pale bahati mbaya choo kipumue ukiwa mule bakteria wasioonekana wanamwingia moja kwa moja kwenye maungio na wale wenye mzio sio kuwashwa huko ma dr wapo humu watatusaidia mengineyo.
but hebu tushauriane ni nini kifanyike kwa wale ambao wanatumia choo cha shimo ili waepuke haya maambukizi?