JosephElly
JF-Expert Member
- Jun 5, 2012
- 2,432
- 1,035
Familia iliyofiwa itagawana mirathi kulingana na aidha itikadi/imani ya dini yao, au watatumia mahakama kuhamua jinsi ya kugawana mali, wakati mwingine sheria za kimila utumika katika kugawana urithi. Kumbuka kwamba urithi ni haki ya kila mtoto aliye hai.Endapo baba akifariki akaacha watoto wawili wakike (18+) na wakiume (18+), lakini hajaacha wosia uridhi wa ardhi ya marehemu itaridhiwa na mtoto yupi? Au watoto wote?
Je endapo marehemu akiacha wosia wa kumuachia mali yote mtoto mmoja tu wakiume, mahakama inaweza vunja wosia endapo watoto wengine wa marehemu wakifungua kesi ya madai?
Opps... Naona nimeipost hapa kwa bahati mbaya .... Msaada mod kunihamishia jukwaa :sorry:
but ninaongelea endapo sheria za mahakama zitatumika
kuna dalili za kuchakachua wosia hapaEndapo baba akifariki akaacha watoto wawili wakike (18+) na wakiume (18+), lakini hajaacha wosia uridhi wa ardhi ya marehemu itaridhiwa na mtoto yupi? Au watoto wote?
Je endapo marehemu akiacha wosia wa kumuachia mali yote mtoto mmoja tu wakiume, mahakama inaweza vunja wosia endapo watoto wengine wa marehemu wakifungua kesi ya madai?
Mahakama inaamuwa? mahakama haiamui mahakama inahukumu. Mjiamulie nyie mnataka sheria ipi itumike, mkishindwa kujiamulia, mahakama itaamuwa kutokana na sheria ya Dola. Mahakama kama mahakama haina sheria.
Wewe acha kupotosha mahakama inafanya maamuzi kwenye makosa ya madai na inahukumu kwenye makosa ya jinai......na kuna maamuzi yanayofanywa na mahakama ni sheria(PRECEDENT) kuna mazingira flani mahakama inatoa mwongozo unaofanana na kutunga sheria...ZOMBA kama hujakaa darasani kusoma sheria usijaribu kupotosha watu umu sheria is a noble proffessional don dare to put your politics.
Ni vizuri hii mada ungeipost JF jukwaa la sheria,nadhani ungepata ushauri,kwani kule ndio mahala pake.
Wewe ndio katika wale waliojazwa Ubaguzi wa Ujinga. Mahakama inahukumu haiundi wala kutunga sheria, maamuzi ya mahakama ni hukumu, mahakama inaweza kuweka kanuni lakini si sheria au sharia. Usitake kupoteza watu.
ndugu kama kingereza kinapanda na si mvivu wa kjisomea unaweza kupitia hapa chinihapo nimeongelea kesi mbili tofauti, endapo wosia haupo. Na endapo wosia ukiwepo.. mpalu
but napenda kufahamu endapo mahakama ndo itahusika na utoaji wa maamuzi
Ulikuwa unajazwa Ubaguzi wa Ujinga kwenye kuta nne, mwenyewe unajiona ndio umesoma. Ungekuwa unajuwa maana tu ya neno "mahakama" kuwa ni panapotolewa hukumu, usingeyasema yote hayo. Labda Kenya ndio mnatunga sheria mahakamani, nyang'au wahed wee!Wewe ni mbumbumbu wa sheria siwezi bishana na mimi nimekaa darasani wewe ni BUSH LAWYER.
inategemeana na aina ya sheria itakayotumika kugawa mirathi hiyo. kuna aina tatu zinazotumika, kwa kifupi, kuna mirathi inayogawanya kwa dini ya kiislam, mirathi kugawanywa kimila na ile kiserikali. yaani either kutumia sheria ya kiislam, kutumia sheria za kimila na kutumia sheria ya kiserikali yaani Indian succession Act ya mwaka 1885. kama watawaganya kwa kutumia sheria ya kiselikali, basi wasichana na wavulana watagawanywa kihalali bila kubaguana kwenye gender.hii ndo sheria isiyo na matatizo. kama ni kiislam itagawanywa kwa quran, kama ni kimilia, kwa kifupi ni kwamba, wanawake huwa hawamiliki ardhi/nyumba ila wanaweza kuruhusiwa kuishi ndani hadi pale watakapoolewa. sheria ya kimila ina matatizo sana. kuchagua sheria huwa kuna kipimo kupima kama marehemu alikuwa anaishi maisha ya aina gani. watu wengi wa vijijini huwa wanadhaniwa kuwa waliishi kwa kimila labda utoe ushahidi mpya kubatilisha hilo, wale walioishi miijini muda mrefu na hawakuwa wanafuata mila na desturi katika maisha yao huchukuliwa kama waliishi maisha ya kisasa hivyo sheria ya kiserikali itatumika, wale waliokuwa wanaishi maisha ya kiislam sheria ya kiislam itatumika. mjane anapata 1/8 na iliyobaki wanagawana warithi wengine kama watoto na ndugu wa karibu. sheria ya kiserikali inaweza isigawe mali kwa ndugu wakati mwignine, mali zikaenda kwa watoto.
ndugu kama kingereza kinapanda na si mvivu wa kjisomea unaweza kupitia hapa chini
dah... Ahsante sana kwa hii info broinategemeana na aina ya sheria itakayotumika kugawa mirathi hiyo. Kuna aina tatu zinazotumika, kwa kifupi, kuna mirathi inayogawanya kwa dini ya kiislam, mirathi kugawanywa kimila na ile kiserikali. Yaani either kutumia sheria ya kiislam, kutumia sheria za kimila na kutumia sheria ya kiserikali yaani indian succession act ya mwaka 1885. Kama watawaganya kwa kutumia sheria ya kiselikali, basi wasichana na wavulana watagawanywa kihalali
Eeeh! Kwani hili ni jukwaa la nini?