inategemeana na aina ya sheria itakayotumika kugawa mirathi hiyo. kuna aina tatu zinazotumika, kwa kifupi, kuna mirathi inayogawanya kwa dini ya kiislam, mirathi kugawanywa kimila na ile kiserikali. yaani either kutumia sheria ya kiislam, kutumia sheria za kimila na kutumia sheria ya kiserikali yaani Indian succession Act ya mwaka 1885. kama watawaganya kwa kutumia sheria ya kiselikali, basi wasichana na wavulana watagawanywa kihalali bila kubaguana kwenye gender.hii ndo sheria isiyo na matatizo. kama ni kiislam itagawanywa kwa quran, kama ni kimilia, kwa kifupi ni kwamba, wanawake huwa hawamiliki ardhi/nyumba ila wanaweza kuruhusiwa kuishi ndani hadi pale watakapoolewa. sheria ya kimila ina matatizo sana. kuchagua sheria huwa kuna kipimo kupima kama marehemu alikuwa anaishi maisha ya aina gani. watu wengi wa vijijini huwa wanadhaniwa kuwa waliishi kwa kimila labda utoe ushahidi mpya kubatilisha hilo, wale walioishi miijini muda mrefu na hawakuwa wanafuata mila na desturi katika maisha yao huchukuliwa kama waliishi maisha ya kisasa hivyo sheria ya kiserikali itatumika, wale waliokuwa wanaishi maisha ya kiislam sheria ya kiislam itatumika. mjane anapata 1/8 na iliyobaki wanagawana warithi wengine kama watoto na ndugu wa karibu. sheria ya kiserikali inaweza isigawe mali kwa ndugu wakati mwignine, mali zikaenda kwa watoto.